CHADEMA, Kikwete uso kwa uso 27th Nov 2011

Status
Not open for further replies.
walishazoea kusema kuwa njia bora ni kutoka nje,, sasa wanaingia ikulu kufanyanini? Ni genge la kihuni linalotumia mgongo wa siasa kupotosha umma, maana ni wa2 wasikuwa na maadili, wasioheshimu viongozi wenzao,wanadharau police, mahakama, jeshi , tume ya uchaguzi na kila ki2, kuwa na wanasheria kibao kwenye chama chao ndo wanatufumbia macho kuwa kigezo cha kututetea?

Wasijidanganye kwa kuwa na washabiki wengi lakini kama hawawaelezi ukweli na dhamira yao ipo cku watatupwa kama umbwa na kuwasahau palepale.

Mkuu, maadamu tumekubali siasa ya vyama vingi, ni vizuri kutolalamika na yale yanayotokea ali mradi wasivunje amani ya nchi na raia wake. Tunahitaji uvumilivu wa kisiasa hususani upande wa serikali. Katika vyama vingi tutaona na kusikia mengi ambayo tusingeweza kusikia katika nchi ya chama kimoja. Amini usiamini.
 
Kile kikao kilichoombwa na CHADEMA kukaa na JK kuzungumza kuhusu katiba mpya hatimaye leo kitafanyika.

Habari zinaendelea kudadavua kuwa kikao hicho kitahusisha ujumbe wa CHADEMA na JK na forum yake huku vyama vingine vya siasa kutokuwepo tofauti na ilivyopendekezwa na NEC ya CCM ambayo inaongozwa na JK.

Jamani pindi kikao kikianza kwa yeyote atakayepata kinachoendelea kikaoni atujuze. Naomba kuwasilisha.
:spy:

Source; Mwananchi newspaper

Sina tatizo na JK, tatizo langu ni hao wapambe, watakachofanya ni kujionesha kwa JK kuwa wao ni brightest aliowachagua na matokeo yake watakuwa ni watetezi zaidi ya uoza uliopitishwa zaidi ya kusikiliza hoja za CHADEMA na kuzifanyia kazi.

Nitafurahia kuwa kama kikao hiki kitakuwa cha kusikilizana badala ya kurumbana na kuoneshana nani zaidi.
 
walishazoea kusema kuwa njia bora ni kutoka nje,, sasa wanaingia ikulu kufanyanini? Ni genge la kihuni linalotumia mgongo wa siasa kupotosha umma, maana ni wa2 wasikuwa na maadili, wasioheshimu viongozi wenzao,wanadharau police, mahakama, jeshi , tume ya uchaguzi na kila ki2, kuwa na wanasheria kibao kwenye chama chao ndo wanatufumbia macho kuwa kigezo cha kututetea?

Wasijidanganye kwa kuwa na washabiki wengi lakini kama hawawaelezi ukweli na dhamira yao ipo cku watatupwa kama umbwa na kuwasahau palepale.

ni punguani tu anayeweza kuandika matusi kama haya!
 
Kikao kitachukua masaa mangapi? Mi ningependa kiwe cha masaa mengi ili kila kitu kijadiliwe kwa kina. Nisingependa kusikia kwa sababu ya muda mchache ajenda zimepitishwa juujuu.
 
Nafurahia maana tim ile ni nzuri sana zaidi wawe makini na hewa wanayovuta maana ccm ni wauaji sana wameua watu wengi sana na wengine kuwaharibia ngozi angalia mwakyembe, ona kombe, angalia kolimba, angalia amina chifupa, angalia akina karume wenyewe list ni kubwa na inaendelea. Mhim kamanda wawe tayari na wawe na soft inteligent mask to detect and take away sumu

Thibitisha
 
mzee ukilijadili hili kwa undani unaweza kupokea matusi makubwa sana.....
Wabe, jf tunajadili kila kitu bila kujali tutapokea nini, haswa ukweli mchungu!. Kesho au keshokutwa JK anausaini!. Mimi sisubiri matokeo ya kikao, jamaa watatoka wamelainishwa na kulainika kama maini!.
 
Kama ni kweli EL ana mpango wa kuhamia CDM,

Basi JK itabidi ampiku kwa kuwakubalia mapendekezo yao otherwise mambo yanaweza kuja kumgeuka jumla,hivi anajuwa EL ana nguvu kuliko yeye ndani na nje ya chama cha magamba.
 
Hivi CDM watakuwa tayari kumpokea EL?
 
Kuna nyimbo 3 za Prof. Jay zinaendana na hali halisi. ilianza NDIYO MZEE, ikafuata KIKAO CHA DHARARU na mwishowe ..... NANG'ATUKA!
Unabashiri nini?Kung'atuka kwa mkulu? itakuwa ni heshima kubwa kwake.
 
Nilisikia kuwa CHADEMA wanakuta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Napenda kuelewa wanakutana lini na agenda yao ni ipi? nikitazama "deadline" aliyowekewa Rais kuwa awe ameshasaini sheria mpya ya kusimamia mchakato wa kukusanya maoni ndiyo inafikia ukingoni.

Kuna mwenye habari za huu mkutano, nilisikia sikia kwa mbali kama wamepangiwa leo. Naomba tujuzane yanayojiri. Ikiwezekana basi tupate habari live kuelekea mkutano kwani nimezowea humu kuwasoma chadema wakirusha habari za maandamano "live". Kulikoni?

Kwa upande wangu naomba Rais asiusaini na aunde tume ndogo ikiwashirikisha wajumbe kutoka CHADEMA na awape mwezi mzima hiyo tume waje na mapendekezo yao mapya. Wakimaliza aitishe kikao cha bunge cha dharura wajadili hayo mabadiliko na waurudishe usainiwe haraka iwezekanavyo kwani natamani kuona Kikwete akiweka rekodi nyingine tena kuhusiana na katiba mpya maana mpaka sasa anashikilia rekodi chungu tele katika uongozi wake uliotukuka.
 
Naona FF sasa hivi unaanza kuandika thread zenye akili.
Hongera kwa kubadilika..
 
kwani ameingia kwenye guiness world record kwenye uongozi wake uli...
 
1 Amevunja rekodi kwa kuleta Richmond aliyezaa Dowans Dowans naye kazaa Symbion,Kagoda,EPA na nk
2 Amevunja rekodi ya kutorosha wanyama nje ya nchi na mikataba mibovu ya Madini
3 Amevunja rekodi ya kuamrisha askari waue wananchi wasiona hatia huko Arusha,Mbeya,nyamongo nk
4 Ametumia Dini kuwagawa Wa-Tanzania aliwaita Kafu wana Udini na sasa Kawaita Chadema watu wake wametumia mpaka HIJAB jujipatia kura huko Igunga
5 Na sasa baada ya kumtumia NAPE anataka kumweka Msalabani ili Asulubiwe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom