CHADEMA jitathiminini suala la Muungano

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,502
19,302
Ifike Mahali Chadema waitimize hamu ya Watanganyika, kwa kupigania maslahi ya Watanganyika pia. ukweli mchungu ni kwamba, kura zote mnaweza kupata ni za bara, Zanzibar hawaipendi chadema, na hawatakuja kuipenda kwasababu huwa wanaamini ni chama cha wakristo. siongelei udini, ila ukweli ni kwamba hata chadema ikiamua kuachana na zanzibar leo, kura zitabaki zilezile.

Ukiwaangalia wazanzibari, kwenye kila kitu, wanategeana sana wao kwa wao na wanatetea taifa lao. hata kitu kidogo kama cha feitoto tu umeona namna wote walivyoungana. hili ni somo kwetu watanganyika. nashauri chadema, sio kwamba itugawanye, ila ifanye yafuatayo:

1. next election, njooni na idea ya kutetea maslahi ya Tanganyika, bila kujali kama hamtapewa kura visiwani, kwasababu mpewe kura msipewe kura kule haibadilishi kitu.

2. mkitaka kupata kura za kutosha na kuidondosha mazima ccm, gusa masuala ya msingi yanayoiumiza Tanganyika kama ardhi, (wazanzibar wanamiliki huku, sisi kule hatumiliki).

3. gusa pia ajira, wazanzibar wanapata ajira hapa tena kwa usawa kimuungano, lakini Mtanganyika hawezi kupata kura zanzibar.

4. kuweni watetezi wa Watanganyika, ambao ndio wenye uchungu zaidi na Tanganyika hata kwenye uongozi.
 
Unafaham maslah ya taifa mkuu?

Zanzibar ni bi mdogo sana.. sio mtu wa kumzungumzia....
 
Unafaham maslah ya taifa mkuu?

Zanzibar ni bi mdogo sana.. sio mtu wa kumzungumzia....
ila anaweza kuwa na athari, pale raia wake anapokuwa kiongozi wa wote, tunatakiwa kuwawekea mipaka kama sisi walivyotuwekea mipaka kama hawapo hapa kwa ajili ya kubebwa. ni Mtanganyika pekee ana uchungu na Tanganyika, asikudanganye mtu.
 
ila anaweza kuwa na athari, pale raia wake anapokuwa kiongozi wa wote, tunatakiwa kuwawekea mipaka kama sisi walivyotuwekea mipaka kama hawapo hapa kwa ajili ya kubebwa. ni Mtanganyika pekee ana uchungu na Tanganyika, asikudanganye mtu.
Upo Sawa.
Lakini sio kumjadili kwa namna ya ubaguzi na kuweka Uzanzibar na Utanganyika mbele, tunawez pambana nao bila kujali asili yao .

Nawaonq kina Fatma na hisia za ubaguzi linapokuja suala la Uzanzibar ..

Sisi ni wakubwa tunaweza fanya bila kuwabagua.
 
Bila Katiba mpya hakuna mabadiliko CHADEMA agenda yetu ni Katiba Mpya bora kwanza.

Hii Katiba ya sasa ni ya Chama kimoko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom