Katika vitu ambavyo chadema imefanikiwa ni kuwa na watu wenye fikra za kisiasa na wanazitumia kujenga na kufanya strategies kubwa. Nilikuwa na mkuu mmoja wa chadema nikamuuliza ana maoni gani kuhusu gamba la Lowassa. Yeye alichosema ni kwamba kimkakati chadema wanamuunga mkono Lowassa akiwa ndani ya ccm na wapo tayari kumsaidia apitishwe kugombea urais.
Faida za Lowassa kugombea ni mbili. Kwanza itakuwa ngumu sana kwa ccm kumuuza kwani wao wenyewe ndio waliosema kuwa ni fisadi na gamba na ipo kwenye record. Pili, ndani ya ccm kuna makundi hasimu sana kiasi kwamba watu kama akina Sitta hawawezi kubaki ndani Lowassa akigombea. Hivyo ccm itagawanyika mapande na itakuwa faida kubwa kwa chadema.
Na mbaya zaidi wanahofia atalipiza kisasi kwa wana ccm waliokuwa wanampinga hivyo watakuwa tayari kuona chadema ikishinda kuliko kushinda Lowassa. Wanachosema ambacho hata mimi nakiona hivyo, ccm watapata faida sana kama akiteuliwa kugombea mtu msafi na ambaye hana makundi.
Naomba niliyezungumza nae asinilaumu kwa kuanika mikakati ya chadema, ni kwa ajili ya mjadala tu