CHADEMA imepiga HATUA

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
1. Kitendo cha kusimamisha wagombea katika Kata zote 29 katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani ni suala jipya.Nyuma kidogo,wagombea wengi wa CCM walikuwa wanpita bila kupingwa.

2. Kutetea Kata 2 na kuongeza 2. Sisi CCM tumeshindwa kutetea kata zetu zote.

3. Kuzidiwa kwa takribani kura 8000 kwa Kata zote ni hatua kubwa mno

4. Kukubali kushinda na kushindwa ni jambo la kupigiwa mfano. Tungekuwa sisi CCM tumeshindwa hiyo pasingekalika.Green Guards walipewa kazi nzito sana: kuiba kura na 'kulinda' kura zilizoibwa.Sisi wa ngazi ya juu chamani tunajua.

5. Kushinda katika mikoa tofauti ni jambo jema.Ingekuwa Kaskazini tu,mngetupa la kusema.Ni kata za Morogoro,Iringa,Kilimanjaro na Arusha.

Mimi kama kada wa ngazi ya juu wa CCM nawapongeza CHADEMA na kutamka kuwa sasa Tanzania ina vyama vingi vyenye nguvu hasa CHADEMA wanaotunyima usingizi
 
Mzee tupatupa kama kweli hukuamua kuja kutupatupa kauli hizi ili upepo upite hakika umeonyesha ka ukomavu ka kisiasa ambako naamini hekima zake zimemshinda hata yule sisi tunaye muita vuvuzela. Bandiko lako limemuacha vuvuzela umbali wa kilometa elfu moja kwa masaa kadhaa.
 
matokeo unaweza kuyasoma ktk mixture result i.e pos/neg inategemea uko upande gani lakini kama mimi ni cdm matokeo haya ningeyachukulia ni challenge ingawa kuna some sort of positiveness ndani yake. haya maeneo niliyoanguka k=ningerudi au ningetuma kikosi kasi kufanya reseach ya nguvu kujua ni nini hasa kilituangusha kwahiyo nageuza matokeo in a positve way for future use. ingawa rushwa na yenyewe inaweza kuwa ni kikwanzo kwa ushindi lakini ningependa nijiakikishie kiushahidi kwa hard evidence kwamba hasa hilo lilikuwa ni tatizo na kuwa si kitu kingine.

in short matokeo haya inabidi chadema iyafanyie in a positive way kwakujua nini hasa kilitokea kwa sababu sio kwamba si progress bali kila mwana chadema atakubaliana nami kuwa ilikuwa kinyume na matarajio ya wengi.
 
Mzee tupatupa,

Nakupongeza sana kwa jinsi ulivyotoa mawazo yako kama mdau wa demokrasia nchini. Na pia kwa kujua kwamba kumbe demokrasia inapanuka, hata mimi nimeliona hili hasa kupitia chaguzi ndogo. Kwa kuwa hapo nyuma ilikuwa vigumu sana kwa vyama vya upinzani kupata kiti kupitia uchaguzi mdogo lakini kwa CDM kwa jinsi wanavyofanya sasa ni jukumu letu kuwapongeza na kuwatia moyo kuwa wanapata mafaniki ya Kisiasa.
 
Kama kuna mtu hajaona hatua CDM iliyopiga ktk uchaguzi huu basi atakuwa anajifanya ni kipofu tu. But kinachojadiliwa na wamependa mabadiliko wengi hapa, ni uwiano wa rasilimali/mbinu zilizotumika na matokeo yaliyopatikana
 
Ikiwa hatua zenyewe ndio hizo na 2015 ndio hiyo, sijui mtafika lini mwisho wa safari?
 
Poleni endeleeni kujifariji. Kampeni kuubwa kuambulia viti vi 5 tu ni aibu. Wenye pesa wataanza nuulizia faida. Hizi sangara yaelekea kuna maneno
 
Mzee Tupatupa we siyo mwanachama mwenzetu...........sisi ccm tunajipongeza kwa kushinda kata nyingi....hizo zingine siyo kwamba tulishindwa.......bali tumewahurumia chadema waambulie japo..............hahaaaaaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Chadema wanatamani kulia lakini ndio hivyo, maji yamewafika shingoni, machozi hayatoki, kinywa hakicheki.

Halafu Kikwete anakwenda huko-huko wanakojidai ndio ngome yao, nisikilizie akishaondoka huko.
 
kikubwa ni kusogea hata kama ni kwa hatua1,hatujafanya vizuri sana ila tunazidi kumtafuna Mgeu,tokea 2000 CDM inagain
 
si vitongoji,kata mpaka majimbo,kubwa hapa ni kuzidisha mikakati iwe ya kisasa zaidi na izame ndani kwa mda wa kutosha
 
No.
KATA
CCM
CDM
Jumla
Tofauti
Tofauti Asili mia
1
Magomeni (Pwani)
1,478.00
479
1,957.00
999
51.047522
2
Bangata
1,117.00
881
1,998.00
236
11.811812
3
Daraja mbili
1,324.00
2,193.00
3,517.00
-869
-24.70856
4
Mahenge
710
444
1,154.00
266
23.05026
5
Mtibwa
1,372.00
3,096.00
4,468.00
-1,724.00
-38.5855
6
Mtele
995
297
1,292.00
698
54.024768
7
Mpapai
1,443.00
280
1,723.00
1,163.00
67.498549
8
Luwumbu
565
25
590
540
91.525424
9
Malangali
1,247.00
1,418.00
2,665.00
-171
-6.41651
10
Lwezera
1,317.00
925
2,242.00
392
17.484389
11
Makata
808
38
846
770
91.016548
12
Mlelomiembeni
818
138
956
680
71.129707
13
Minyenze
378
167
545
211
38.715596
14
Karitu
854
354
1,208.00
500
41.390728
15
Kiloleni
648
166
814
482
59.213759
16
Ipole
365
568
933
-203
-21.75777
17
Bugarama





18
Mwananza
794
575
1,369.00
219
15.997078
19
Lubili
1,108.00
620
1,728.00
488
28.240741
20
Kitagiri
1,416.00
157
1,573.00
1,259.00
80.038144
21
Kikokona
1,149.00
367
1,516.00
782
51.583113
22
Nanjaraneha
1,128.00
2,370.00
3,498.00
-1,242.00
-35.506
23
Kilema Kusini
784
734
1,518.00
50
3.2938076
24
Vugiri
1,460.00
337
1,797.00
1,123.00
62.493044
25
Tamota
1,060.00
772
1,832.00
288
15.720524
26
Msalato
869
450
1,319.00
419
31.76649
27
Mpwapwa
1,722.00
1,189.00
2,911.00
533
18.309859
28
Myovizi
1,726.00
1,498.00
3,224.00
228
7.0719603
29
Mpapa
903
310
1,213.00
593
48.887057

JUMLA
29,558.00
20,848.00
50,406.00
8,710.00
17.279689


Ongzea na hii
 
1. Kitendo cha kusimamisha wagombea katika kata zote 29 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ni suala jipya.nyuma kidogo,wagombea wengi wa ccm walikuwa wanpita bila kupingwa.

2. Kutetea kata 2 na kuongeza 2. Sisi ccm tumeshindwa kutetea kata zetu zote.

3. Kuzidiwa kwa takribani kura 8000 kwa kata zote ni hatua kubwa mno

4. Kukubali kushinda na kushindwa ni jambo la kupigiwa mfano. Tungekuwa sisi ccm tumeshindwa hiyo pasingekalika.green gurads walipewa kazi nzito sana: Kuiba kura na 'kulinda' kura zilizoibwa.sisi wa ngazi ya juu chamani tunajua.

5. Kushinda katika mikoa tofauti ni jambo jema.ingekuwa kaskazini tu,mngetupa la kusema.ni kata za morogoro,iringa,kilimanjaro na arusha.

Mimi kama kada wa ngazi ya juu wa ccm nawapongeza chadema na kutamka kuwa sasa tanzania ina vyama vingi vyenye nguvu hasa chadema wanaotunyima usingizi



acha kumeza meza maneno ndugu
hiko chama kinahitaji kufanya kazi ya ziada na kuondoa kasumba yake ya ukanda ili kiweze kuiondoa ccM madarakani,,tujuze kanda ya kusini kule lindi na mtwara wameambulia kitu gani??
Ushabiki usio na tija twaufananisha na ulimbukeni
 
Back
Top Bottom