CHADEMA imemkosea nini huyu mwandishi?

Ni mwandishi nguli na mwana JF maarufu CV yake haina mashaka popote na ana heshima yangu kubwa tu. Ni mmojawapo wa watu aliyenihamasisha kujiunga na JF hasa kule jukwaa la intelligence

Simhukumu vibaya lakini nadhani ana tatizo binafsi na CHADEMA kama ilivyokuwa kwa Prince Bagenda na Augustine Lyatonga Mrema mzee wa Kirachacha

Kuna mengi ya kusimuliwa kati ya wawili hawa.. Ya sirini na ya upenuni, Lakini yanayojulikana zaidi ni pale siasa za Mageuzi zilipoingia nchini mwaka 1992 na baadae Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Lyatonga Mrema alipojivua nyazifa zake zote na kukiacha chama chake na kujiunga na NCCR-Mageuzi kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo

Kujitoa kwa Mrema ccm kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana kwakuwa kwa wakati huo ndio waziri pekee aliyekuwa na uthubutu uliorejesha nidhamu serikalini na kuwa tishio kwa wazembe., wala rushwa majambazi na wapiga dili wengine

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu akasimama kugombea nafasi ya urais kupitia NCCR- Mageuzi chini ya timu ya
Mabere Nyaucho Marando wakili msomi
James Mbatia
Dr. Masumbuko Lamwai wakili msomi RIEP
Prince Bangeda mwandishi nguli na wengine wengi

Moto ule wa NCCR hiyo uliwatisha mno ccm na wakaona kitisho cha wazi kama wataiacha NCCR istawi, hivyo baada ya uchaguzi ule NCCR ilifitinishwa na kumeguka mapande mawili kila kundi likilishutumu lingine kwa usaliti

Baada ya hapo yalitokea mengi sana, lakini la kukumbukwa zaidi ni namna Prince Bangeda alivyotumika kumshambulia Mrema kupitia magazeti ya Rai na Mtanzani kwenye safu ya :Kalamu ya Bangeda' nadhani.. Yaani ilikuwa kama project maalum ya kumchafua mzee wa Kirachacha.. Prince Bagenda aliandika na kuandika na kuandika, aliandika mabaya tupu. Hakuna siku aliandika jema la Mrema na kwa baadhi ya mada akitoa ushauri wa kinafiki kabisa

Inawezekana pengine kuna siku Jenerali Ulimwengu atakuja kutuambia ule mradi ulikuwa wa nani na ulikuwa na lengo gani, lakini juu ya yote mwisho wa project hiyo ya Bangeda aliasisi gazeti lake na akiwa kwenye mchakato wa kuanzisha TV yake. Ofisi yake iliyokuwepo pale jengo la ushirika Lumumba iliwaka moto na kila kitu kikaishia pale.. Prince Bagenda hakuwahi kusimama tena na huku mzee wa Kirachacha ambaye hata mara moja hakuthubutu kumjibu Bagenda akidunda mpaka Leo hii na kigoli kaoa hivi karibuni

Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania

Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema

Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni

Mungu ibariki CHADEMA...!!!
You deserve my honor!!
 
Hii nadhani ni nje ya mada.. Ila kama ni kutangaza maslahi mimi ni SIMBA damu na ni CHADEMA kindakindaki
Na hapo ndiyo kwenye tatizo!

Nje ya mada;
Ningetamani kidogo utueleze pia kuwa zitto ameikossa nini chadema maana hakuna mwanachadema asiyemtaja zitto kiuhasi kila baada ya maneno mawili.
 
Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni
Mimi huyo mwandishi nguli ambaye hakutajwa simjui, lakini katika kukadiria kwangu, kama mtu huyo hushiriki kwenye jukwaa hili la Siasa, JF; basi huyo ninayemjua mimi siwezi kamwe kumpa sifa ya "uandishi nguli."

Huyo tokea mwanzo kabisa kukutana naye hapa JF, na kusoma maandishi yake kadhaa nilihitimisha kuwa siyo mwandishi, ni kanjanja tu!
Kwa bahati mbaya sana ndani ya nchi yetu hii, nadhani tumeishiwa watu wenye upeo ambao tunaweza kuwatolea mifano ya sifa kama hizo ulizompa huyo mtu.
Mimi baada ya kumjua kuwa hana kitu kabisa, hasa baada ya kufahamu kuwa hana popote anaposimamia katika maandishi yake, nilimpa sifa ya kuwa "Popo"ambaye hana sifa za kuitwa mnyama moja kwa moja, ama kufahamika kuwa ni ndege.

Baada ya kumtambua hivyo, sikujishughulisha tena na kusoma mabandiko yake humu marefu, ambayo niliyapa sifa ya kuwa "magazeti".

Tofautisha. huyo si mwandishi. Mwanakijiji, pamoja na kukengeuka kwake, lakini anapopanga hoja zake, hata kama hukubaliani nazo unaona taaluma ya uandishi kutoka kwake. Huyu unayemleta hapa, makala zake hazina sifa za uandishi. Awe anasifu au anaponda, maandishi yake hayana vinasaba vya uandishi wa habari.

Na kuhusu mzee wa kirachacha, hiyo nayo ni habari nyingine kabisa. Mfano wa mwanasiasa asiyekuwa na 'bearing'. Sijawahi kumchukulia Mrema kuwa mwanasiasa wa kutolea mfano kwa wengine.
 
Uzuri ni kwamba HAKUNA WAKALA WA SHETANI ALIYEWAHI KUPAMBANA NA CHADEMA AKASHINDA , labda wakala huyu atakuwa wa kwanza .
Unatofautishaje wakala wa shetani na asiye wakala wa shetani miongoni mwa wapinzani wa chadema au kila mwenye upinzani na chadema ni wakala wa shetani?
 
Ifikie hatua akili zetu zikue na zikomae kuendana na falsafa ya kile kinachopiganiwa....... Demokrasia ni pamoja na kuvumiliana, kuheshimiana kwani tupo kwenye ulimwengu ambao kila mtu ana maoni yake..........

Usitarajie kuyakuta tu yanayokufurahisha tu.....

Mtiririko wa mada zinazozungumzia mtu ambaye ametofautiana na watu maoni ni dhahiri kuwa tuna safari ndefu kuelekea kwenye demokrasia....
Mkuu nadhani ujamwelewa vizuri mtoa mada, ebu fikiria unatambua kabisa Mji wa Abuja lipo Nigeria ila unawaambia watu kua lipo Namibia. He hiyo ndiyo demokrasia au upotoshaji? Tena baada ya masaa mchache unawambia watu mji wa Lagos lipo Mali na si Nigeria. Je unajua na tatizo binafsi na nchi Nigeria au ndiyo demokrasia yenyewe?
 
Mimi huyo mwandishi nguli ambaye hakutajwa simjui, lakini katika kukadiria kwangu, kama mtu huyo hushiriki kwenye jukwaa hili la Siasa, JF; basi huyo ninayemjua mimi siwezi kamwe kumpa sifa ya "uandishi nguli."

Huyo tokea mwanzo kabisa kukutana naye hapa JF, na kusoma maandishi yake kadhaa nilihitimisha kuwa siyo mwandishi, ni kanjanja tu!
Kwa bahati mbaya sana ndani ya nchi yetu hii, nadhani tumeishiwa watu wenye upeo ambao tunaweza kuwatolea mifano ya sifa kama hizo ulizompa huyo mtu.
Mimi baada ya kumjua kuwa hana kitu kabisa, hasa baada ya kufahamu kuwa hana popote anaposimamia katika maandishi yake, nilimpa sifa ya kuwa "Popo"ambaye hana sifa za kuitwa mnyama moja kwa moja, ama kufahamika kuwa ni ndege.

Baada ya kumtambua hivyo, sikujishughulisha tena na kusoma mabandiko yake humu marefu, ambayo niliyapa sifa ya kuwa "magazeti".

Tofautisha. huyo si mwandishi. Mwanakijiji, pamoja na kukengeuka kwake, lakini anapopanga hoja zake, hata kama hukubaliani nazo unaona taaluma ya uandishi kutoka kwake. Huyu unayemleta hapa, makala zake hazina sifa za uandishi. Awe anasifu au anaponda, maandishi yake hayana vinasaba vya uandishi wa habari.

Na kuhusu mzee wa kirachacha, hiyo nayo ni habari nyingine kabisa. Mfano wa mwanasiasa asiyekuwa na 'bearing'. Sijawahi kumchukulia Mrema kuwa mwanasiasa wa kutolea mfano kwa wengine.
Unguli hana , namfahamu huyu mtu tangu Simba Grill Kilimanjaro Hotel , akiwa MC tu kwenye kipindi cha Kitimoto , hana lolote
 
Na hapo ndiyo kwenye tatizo!

Nje ya mada;
Ningetamani kidogo utueleze pia kuwa zitto ameikossa nini chadema maana hakuna mwanachadema asiyemtaja zitto kiuhasi kila baada ya maneno mawili.
Wakati Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo wanapanga mapinduzi haram ndani ya Chadema ulikuwa darasa la ngapi? Unawajui MMM?

Jeshini adhabu ya Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo ni kifo tu hakuna mbadala.

Ona damu ya Usaliti huko ACT Kitila Mkumbo kamsaliti msaliti mwenzanke na kufuata ulaji CCM, huko nako 2025 atasomeshwa namba za kirumi na wenye chama chao.
 
Back
Top Bottom