Manager
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 531
- 73
Jeshi hili limejikusanyia issue za mauaji na mateso ya raia za kutosha kwa mwaka huu. Watu walioanza na Mungu hawatarudi nyuma!I hate the Tanzanian Police Force
Jeshi hili limejikusanyia issue za mauaji na mateso ya raia za kutosha kwa mwaka huu. Watu walioanza na Mungu hawatarudi nyuma!I hate the Tanzanian Police Force
This is the climax huwezi kuwa unaua watu kama zama za ukoloni!
Ivi hawa polisi hawajui kuwa we are customers to them
Tatizo hili naona ni kubwa kwa cdm.Pia hawajui matokeo halisi ya hicho wafanyacho.Haya hata kama cdm wakajua kwa asilimia mia kuwa it is a well planned stratregy to kick their ass,cdm watafanya nini
What cdm is prepared to do,say if their party is deregesterd.To me it looks cdm is short of stratergies.
Hakikufutwa UNITA, chama cha savimbi, pamoja na mauaji halisi kichofanya kwa wananchi wa msumbiji! ije kufutwa chadema kwa mauaji yanayofanywa na polisi!!! KUWA MUELEWA, NI WANANCHI NDIO HATUITAKI CCM, HATUBADILISHI LUGHA.
CDM watakaa na kuanza kutoa hotuba zao zilizochoka; it is about time to confront evil!! Ikibidi kuitisha siku ya mgomo baridi!! Kwamba Said Mwema na Chagonja waondolewe na serikali ikikataa basi utakuwa ni mgomo wa nchi nzima. Hadi auawe mbunge wa CDM ndio watajua kuwa tulipofika ni 'tipping point'?
Mzee Mwanakijiji,kwanza pole kwa kupoteza ndugu yako katika tasnia ya habari,ndugu yetu,mwananchi mwenzetu...nashukuru kwa bandiko hili pia,pengine tutapata maoni ya wananchi nini kifanyike.Nilianzisha thread ambayo nilitaka wananchi watoe maoni yao ni kivipi wanaweza kujilinda.
Ni wazi hatuwezi tena kutegemea ulinzi wa polisi.Polisi walikuwa wakiwauwa raia wema toka kitambo tu,sema hii ni kwasababu wameanza kuuwa kwasababu za kisiasa wazi wazi!
Maandamano ya kulilaani jeshi la polisi ni mwanzo tu.Lakini siyo solution ya tatizo.
SAVIMBI - UNITA - MSUMBIJI!... Hii historia yaelekea ipo mabwepande!..
Mkuu Mzee Mwanakijii pole kwa kuandika hii thread ambayo inanizidishia uchungu jinsi hii nchi inavyoendeshwa kibabe wamemaliza kuuza rasilimali sasa za nchi sasa wameanza kututoa uhai
Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.
Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.
a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!
b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.
c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!
Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.
Nitadharau nikisikia tena viongozi wa CDM wanazungumzia mambo yale yale, kuhusu jeshi lile lile na kwa namna ile ile!! hawatokuwa tofauti na watawala wa sasa!
Kamanda Precise pangolin;
wacha kamba kama ungekuwa unasikia uchungu ungekuwa Mufindi kuziba pengo la kamanda Mwangosi (R.I.P), inasikitisha na kuhuzunisha sana kuona kijana wa watu amepoteza maisha kwa sababu ya upuuzi wa mtu kam Dr. Slaa kulikuwa na ulazima gani wakati serikali ilishakataza, kama haitoshi baada ya tukio hili badala ya kuungana na familia ya marehemu bado alijitia kudai Chadema watafanya mkutano hivi tuseme angekufa mtoto wake au kaka yake Josephine bado angeyasema hayo? Leo kuna wazazi hawatalala, kwa majonzi, leo kuna watoto maisha yao yatabadilika kwa kumkosa baba, yote sababu ya nini kwa sababu ya mshenzi mmoja aliyekosa busara; mtailaumu polisi lakini kama huo ushindani wa kipuuzi usingeshinikizwa na mpumbavu Dr. Slaa Mwangosi (R.I.P) angekuwa hai, yeye amaeshinikiza akiwa hotelini kazi nyake ni kutoa vyambo watoto watu.
Makamanda akili kichwani mwenu hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na nguvu ya serikali.
Chama
Gongo la mboto DSM
CDM watakaa na kuanza kutoa hotuba zao zilizochoka; it is about time to confront evil!! Ikibidi kuitisha siku ya mgomo baridi!! Kwamba Said Mwema na Chagonja waondolewe na serikali ikikataa basi utakuwa ni mgomo wa nchi nzima. Hadi auawe mbunge wa CDM ndio watajua kuwa tulipofika ni 'tipping point'?