CHADEMA Ianzishe mabadiliko ya Ndani, Vinginevyo kuiondoa CCM 2015 ni ndoto - Sehemu ya 1

Labda niseme kitu kimoja, na kupongeza kwa kutoa mawazo mazuri sana yenye nia ya kukijenge chadema, nimawazo bora sana yanayo paswa kufanyiwa utekelezaji kama si baadhi basi yote!

Ukweli ni kwambie CHADEMA mnashida moja, kusahau kuwa kila kitu hakikosi mapungufu. Ukijisahau hilo ukajiona kuwa wewe uko sahihi kwa kila jambo basi 100 percent utashindwa kufikisha malengo yako uliyo yapanga! chadema mkijiona mko 100 percent correct kwakila mnacho kifanya the result will be mass failure! kubalini kukoselewa pale panapo hitaji kukosoleka
 
Mwakani hakuna wa kumsaidia mwenzake,polisi wa kutoa mkoa mmoja kwenda mwingine hakuna,fungu na mbinu chafu toka lumumba itakuwa haifui dafu,Hakuna kupanga matokeo.Mechi zote siku moja.

Wagombea wa magamba watajifia wenyewe

Hapa tutaheshimiana.

mkuu lama umenena kila mtu atabeba furushi lake mwenyewe ndio kutokuwepo kilio na kusaga meno kwa maccm
 
Mwakani hakuna wa kumsaidia mwenzake,polisi wa kutoa mkoa mmoja kwenda mwingine hakuna,fungu na mbinu chafu toka lumumba itakuwa haifui dafu,Hakuna kupanga matokeo.Mechi zote siku moja.

Wagombea wa magamba watajifia wenyewe

Hapa tutaheshimiana.

Hata 2010 mlisema haya haya! tushazoea ngonjera zenu. Team ya ushindi haipo CHADEMA.
 
Utajaelewa siku ya kutangaza matokeo kila Kata na Jimbo kwa za Kura Udiwani,Ubunge na Urais utakaposikia Wakitajwa walioshinda ni CHADEMA! CHADEMA! CHADEMA! hapo labda bongo yako itazinduliwa nakujua ni Ikulu ipi inazungumziwa.

Hii ndoto inaonekana ni tamu sana, ukiendelea kuiota unaweza kupitiwa na kukojoa kitandani.
 
Yamkini wewe ndio u kikojozi mpaka leo kutoka enzi zako za utoto mpaka sasa mnaifanya ardhi ya Nchi yetu kuanza kupokea Damu zisizokuwa na hatia kwa kuwakata shingo ili kubakia madarakani kwa hila,Vitisho na Mauaji.

Sasa mwisho u Karibu sana kuliko tulikotoka.
 
Huu ni Ushauri wangu kwa CHADEMA kwa kuorodhesha Mambo ya muhimu 12 (KUMI NA MBILI).

CCM Wanakuja na Pumba zao za mazoea ya Kimagamba;
Kama mnao sababu za maana zakuwafanya CHADEMA Njia yao ya kwenda Ikulu isiwe Nyeupe Pingeni kwa Hoja.
 
daftari , katiba mpya , tume huru ya uchaguzi hivi ndiyo kaburi la ccm ! Sina wasiwasi na polisi najua 90percent wameathirika kabisa kimaisha na mfumo uliopo .


Najua CDM wako kazini watatenda kwa busara ili kuhakikisha Mabadiliko ya kweli yanatokea Nchini.
 
daftari la kura likiboreshwa litatunufausha sana ACT. chadema imeshachokwa na vijana
 
Mkuu ni Maoni mazuri sana.Mengine yanatekelezwa ingawa mikakati yake haiwekwi public.Hongera sana kwa mtazamo huu mpana Mkuu.

Babu majanga kashakurudisha kazini nn?? Baada ya kutishia utamwaga mboga...ha ha sarakasi za chadomo ha ha ha
 
Ni bayana tena ni kweli tupu wala hakuna Ubishi kuwa Chama kikuu cha Upinzani kwa sasa ni CHADEMA.

Nimeona nitoe yangu ya Moyoni kuwapa ushauri mapema kabla Jua halijachoea.
Maana Rafiki umpendaye kamwe hutakaa kumsema pembezoni bali utaketi kwa mazungumzo naye uso kwa uso.

Njia yangu ya kipekee ya kuwasilisha mashauri yangu ni kwa njia ya Mtandao maana sina kadi wala sina cheo ndani ya chama hiki Makini Japo nakipenda kwa mwenda kasi wake unainyima usingizi CCM kila kukicha kama sio kila kukichwa.


YAFUATAYO SIO YAKUPUUZA VINGINEVYO NITAJUA KUMBE CHADEMA NAO WAMEKUWA
SIKIO LA KUFA:-

kuna kila dalili kuwa CHAMA CHA MAENDELEO NA DEMOKRASIA Nguvu yake ya kushika Dola 2015 haizuiliki kirahisi vile.

KAMA UNABISHA WAULIZE CCM WATAKUAMBIA MAANA WANAUJUA UKWELI HUU.Aisifuye mvue imemnyeshea si wote mnajua Kinana na Nape wameimba Nyimbo wa CHADEMA Majukwaani kuliko hata kuimba nyimbo za CCM chama chao kinachowafanya mkono uende kinywani.
Hilo halina Ubishi.

Mambo haya CHADEMA ikiyafanyia kazi itashinda kabla ya kuanza ushindani wa Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015:-

1.Msibweteke jinsi mnavyokubalika na kuwakusanya watu bila hata ya kuwapa Tisheti,Khanga,Fedha au Masinio ya Nyali,Bali fikirini zaidi Hatima Njema ya Chama chenu.

2.Chadema ihakikishe Wasaliti na Mizizi yao ya Usaliti wameing'oa mapema ili pasiwe na masalia yoyote ya waasi ndani ya chma kabla ya 2015.

3.Msibakie kushughulikia matatizo yanayosababishwa kwa makusudi na CCM yenye lengo la kuwatoa kwenye Dira yenu.

4.Kujenga ama Kuendeleza Mfumo Imara wa Masiliano na Mahusiano kati ya Viongozi wa Kitaifa na Viongozi wa Ngazi za chini ili kuwathibitishia Wanachama waliopo na Wananchi kwa Ujumla kuwa CHADEMA ni Mahali Sahihi na Salama kwa kuleta Mabadiliko ya Kweli Nchi hii.

5.Kuwepo na Mipango mahususi na Endelevu ya Kuvuna Magamba zaidi na kuwafanya washabiki na wakereketwa wenu kuwa Wanachama Wapya wakudumu wenye Kadi za Chama.

6.Watenge Fedha na Kuandaa Watu wenye nia ya Kweli ya kukijenga chama kisha wawatume waende kila Kijiji ambacho Hamjakifikia ili Kutoa Elimu ya Uraia juu ya Umuhimu wa Kujiandikisha na Upigaji wa Kura,Pia hio itakuwa njia bora ya Kujitangaza na kuongeza wigo na kuleta Ongezeko la Kura za Ushindi hadi Ikulu 2015.


7.Fanyeni Madiliko ya Uongozi Mapema iwezekanavyo hasa kwenye baadhi ya maeneo machache ndani ya Chama pale ambapo kuna Uhitaji huo wa Lazima.

8.Fanyeni Uchaguzi Huru na wa Haki ndani ya Chama ili Kuziba Vinywa vya Ujinga na Kutoa Darasa kwa Mkongwe CCM na UMMA wote pia.
Kufanya hivyo itawasaidia sana kumzuia Mshindani wako kukosa mianya ya kukushambulia kwa Propaganda Zisizokuwa za Lazima.

9.Sio lazima kufanya mabadiliko ya Kiuongozi hasa kwenye nafasi ambayo mnaona yule aliyeko anaimudu ipasavyo na una uwezo wa kuwavusha salama salimini 2015 kwa kuwasababishia Ushindi wa Kishindo.

10.Ni muhimu sana Msiache wala Msikome Kujipanua kwa kuongeza idadi ya wetu wenye Uwezo wa Kielimi na Kiuchumi kutoka kada mbalimbali Vyuo vikuu,kwenye Makampuni,Ndani ya Idara na Wizara zote.

11.Endeleeni kuonesha kwa Matendo mkiudhihirishia UMMA wa Watanzani na Dunia yote Ijue jambo hili CHADEMA sio chama:-

a.UKABILA-wachaga.

b.UDINI-Wakristo.

c.UKANDA-Kaskzini

d.UGAIDI-Ryakatare.

Hii itawasaidia kirahisi kukomesha uzushi wa watu aina ya Akina Mwigulu na ccm yao.

12.Ili Mfunge Mabao ya Style zote Uchaguzi Mkuu ujao,

Bao la Kisigino.

Bao la Kichwa.

Bao la Penalty n.k

Lazima Mhakikishe katika kupata wateule watakaosimama kupeperusha Bendera ya chama chenu kwa Nafasi ya UDIWANI UBUNGE na URAIS ni Waadilifu mbele ya jamii inayowazunguka.
Hii itawarahisishia kazi ya kufanya Kampeni Mapema Uchaguzi Mkuu ujao.

MKIFANYA HAYO NILIYOWAUSIA BILA KUPUUZA HAKI A NANI NAWAAMBIENI MAPEMA CHADEMA NJIA ITAKUWA NYEUPEEE KUINGIA IKULU 2015.
ikulu ipi ? Labda ikulu ya nyumbani kwako ! Chuki ya Mbowe kwa Marehemu Chacha Wangwe Ndio inakidhoofisha chama Mzimu wa Chacha umecharuka wale wote waliokuwa na chuki nae ndani ya Chadema 2015 jawabu watazipata ! Kwani Mbowe alipiga Marufuku kwa Wanachadema makao makuu kumkumbuka chacha wangwe hata kwa sala ya nusu dakika tu ! Sasa Mzimu umehamia pale makao makuu upo umesimama wima unamlilia Mbowe
 
Ukabila ukanda udini ufujaji pesa za misaada ukiwemo Ruzuku na Vioja chungu mzima ,vikiwemo vya Rushwa ya Ngono ktk uteuzi viti maalum . Hivi Vioja vya akina Mbowe na wenzake havihitaji Elimu ya juu kubaini Majanga ndani ya CDM hata wa darasa la kwanza tu atabaini Vioja vya CDM kiufupi tu kwa kweli Chadema hawana cha Kuigwa kwa sasa chini ya Mbowe wamekwisha chuja na wanazidi kuchuja zaidi. RIP chacha wangwe
 
Haya ni Mazungumzo baada kunywa gongo na kuvuta bangi. Kalenga imewashindwa ndio mtaweza kushika nnchi?

Endeleeni kuota tu ikulu mtaisikia kwenye redio

R.I.P chacha wangwe ni Vigumu kwa Chadema kuingia ikulu Kama ilivyokuwa vigumu kwa Chacha wangwe kufufuka na Kuwa hai tena ! Na siku huo muujiza wa ikulu ukitokea basi Rais atakuwa Deus malya makamu mbowe
 
Back
Top Bottom