Elections 2010 Chadema Hamjachelewa

Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Napenda kuushauri uongozi wa CHADEMA watenge kama shilingi milioni 12 na kuweka matangazo yasiozidi dakika moja kwenye redio angalau tatu. Matangazo hayo kwa kila redio yatangazwe angalau mara nne kila siku mpaka tarehe 30/10/2010. Lengo kuu la matangazo hayo liwe ni kumshawishi na kumhamasisha kila mpiga kura kumchagua mgombea wa CHADEMA katika ngazi zote tatu za Urais Ubunge na Udiwani.
 
Wahusika wataiona ssa hivi na kupima applicability yake!...Thanx and Keep such good ideas flowing in!
 
Wahusika wataiona ssa hivi na kupima applicability yake!...Thanx and Keep such good ideas flowing in!

Naamini itawasaidia sana hasa kwa upande wa vijijini na mijini pia. Wachague redio tatu kati ya Radio One, Radio Free Africa, TBC Taifa na Clouds FM.
 
Ahahahahahaa...good idea but "ngumu sanaaaa banaaaaaaa"...kwa maana ya kwamba ukiritimba wa serikali ya ccm hautotoa hiyo nafasi....tbc=ccm tv & radio, star tv & radio= dialo's property ambaye pia ni mbunge wa ccm, clouds fm=radioya ccm, itv & radio one=vibaraka wa ccm...labda waanzishe ya kwao
 
Wazo la kuanzisha ya kwao ni zuri lakini kwa sasa ni muhimu sana wakazitumia hizo zilizopo. Kwa kuwa watalipia hayo matangazo sioni kama kutakuwa na tatizo lolote. Ni bora kujaribu kuitumia njia hii katika kuwafikia wapiga kura wengi zaidi kuliko kuacha.
 
Ahahahahahaa...good idea but "ngumu sanaaaa banaaaaaaa"...kwa maana ya kwamba ukiritimba wa serikali ya ccm hautotoa hiyo nafasi....tbc=ccm tv & radio, star tv & radio= dialo's property ambaye pia ni mbunge wa ccm, clouds fm=radioya ccm, itv & radio one=vibaraka wa ccm...labda waanzishe ya kwao

Wiki iliyopita nilikuwa mikoani, ATN ni wazuri sana hawana upendeleo, na inaonekana wameanza kufanya kazo kibiashara, wanaweza kuwatumia hawa!!
 
Back
Top Bottom