CHADEMA furahieni kupoteza umeya wa jiji la Mwanza, ni bahati sana kwenu

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
Nikiwa kama mkazi wa kudumu wa Mwanza na ninayeitakia mema CDM katika harakati zake nimefurahishwa sana na CDM kupoteza kiti cha umeya wa jiji. Hii itawapa furs nzuri sana CDM kuepukana na lawama za hali ya juu huko tuendako. Jiji la Mwanza chini ya mkurugenzi aliyepo sasa Bw Wilson Kabwe kupata maendeleo ni ndoto za mchana, hata kama Meya atakuwa Tundu Lissu au my favorite Mnyika. Ili Meya wa jiji afanye kazi yake vizuri anatakiwa kuwa na timu nzuri na yenye mtazamo wa maendeleo toka upande wa halmashauri, kwa Mwanza hilo halipo. Ukienda jiji la Mza utashangaa sana kuona wafanyakazi waliojaa mtazamo wa rushwa na uvivu wa hali ya juu. Kiburi kiko kwa muhudumu wa ofisi hadi mkuu wa idara, mkurugenzi ndio muasisi wa kiburi. Huyu jamaa ana nguvu kuliko waziri mkuu Pinda, anachoamua yeye hakuna wa kuuliza au kupinga. Madiwani wote wa CDM wallop ajitokeze mmoja humu jukwaani na kusema alipingana hadharani na Kabwe!!
Jiji lina ofisi za hovyo, wafanyakazi wamebanana ofisini, wanazurura kutwa nzima kwenye makorido, hakuna customer service kabisa, vyoo ni vichafu hadi aibu... Meya gani ataleta ,maendeleo katika mazingira hayo, heir kuwaachia CCM waendelee kushindwa. Wakuu wa idara jiji pale hawakai ofisini wanakimbizana na posho tu kila siku! Nani atakaa na madiwani wa CDM kupanga na kutekelezeka mipango ya maendeleo wakati watendaji ni wavivu na wabinafsi namna hiyo. Furahieni kupata fursa nzuri ya kujitenga na utendaji mbovu wa Kabwe hadi wakati muafaka utakapofika. Meya na mkurugenzi wanatakiwa kufanyakazi kama timu, umeona wapi timu inayochanganya Mwizi na Mkimbiza Mwizi au mpambanaji wa ufisadi.

Sidhani kama CDM wanalo la kujivunia katika mwaka mmoja na nusu wa umeya, Kama lipo naomba nikosolewe. Barabara ni za mavumbi na nyingi hadi Leo greda halijapita toka mvua zilipoisha. Wakati Pinda kaja Mza nilikutana na greda linatengeza barabara ya Buswelu Kiseke saa 4 usiku na madiwani wa CDM huenda walishiriki kuhalalisha huu usanii Kama walivyoshiriki kuhalalisha ujenzi wa barabara ya lami kwenda kwenye hotel moja tu ya Malaika yenye urefu wa Kilometa 10 kwa ajili ya hotel ya vyumba 24 wakati maelfu ya wakazi wa Buswelu hawana barabara hata ya kiwango cha vumbi. Mkandarasi jasco yup hadi leo site anajenga barabara kwa fedha za msaadanwa benki ya dunia kwenda kwenye hotel ya tajiri mmoja

Ni kwa mazingira hayo Mimi Ulukolokwitanga Ng'wizukulunzungu nimefurahishwa na nafasi kifisadi kurudisha kwa mafisadi hadi katiba mpya itakapoweka wazi nafasi ya meya na mkurugenzi
 
Mods msiunganishe hii uzi na zile nyingine hii inajitegemea na najua Dr Slaa ataiona na kukubaliana na mimi kwani ni muungwana
 
naunga mkono hoja kwa kuzingatia .... point ya ' a blessing in disguise'

Jiji la Mwanza kwa ukubwa wake na vyanzo vya mapato kwa sasa linazidiwa na Mbeya katika ukusanyaji mapato, then ung'ang'anie kuongoza jiji la namna hiyo kweli. Utaweka credibility ya chama in jeopardy
 
Naungana na mtoa hoja,pale jiji pameoza na panatoa harufu mbaya ya rushwa. Kuna mtu alinisimulia yaliyomtokea na yanayotokea kwenye upande wa idara ya elimu.NITAREJEA NIANIKE KINACHOTOKEA PALE,sasa naangalia mpira wa azam na jkt. Halimashauri ya JIJI MWANZA its a damn ass i can dare 2 say!
 
Kwa hiyo wasikate rufaa wananchi wa mwanza wanasemaje na uchaguzi huu
 
Umefanikisha w.end yangu asante mungu akubariki dr, slaa relux hatujapoteza kitu ndo kwanza kazi imeanza
 
Isije ikawa sizitaki mbichi hizi!? Upuuzi anaofanya meya wa Arusha, natamani halmashauri zote ziongozwe na cdm!
 
Mkuu,hapana mimi binafsi sikubaliani na hoja yako juu ya upotevu wa nafasi ya umeya jijini Mwanza. Why are we retreating and surrendering so easly and so early just like that? What's cooking on over there in Mwanza? Never show your weakness to your opponent.
 
haha!!,hapa patam!,sasa imekua cdm washkur kukosa umeya!,makubwa!!!,wangepata JEEEE!!!!!!!!!!!!,mh!!!!!!!!!!! KAZI KWEL KWELI!
 
haha!!,hapa patam!,sasa imekua cdm washkur kukosa umeya!,makubwa!!!,wangepata JEEEE!!!!!!!!!!!!,mh!!!!!!!!!!! KAZI KWEL KWELI!
Mtoa mada ameeleza vizuri washukuru kwa kukosa na sababu amezitoa lakini kama wangepata kwa maana ya mtoa mada bado chama kingeendelea kupata lawama na manung'uniko kutoka kwa wananchi wa Mwanza kutokana na uongozi mbaya uliopo halmashauri ya jiji Hususani Mkurugenzi, nini ambacho haujakielewa hapo hadi unakuja na vijembe.
 
Mtoa uzi laiti Dr Slaa angejua unapatikana wapi angekufuata akunyanganye na kadi yenyewe ya CDM.
 
Hakika mtoa mada, wewe umetufungua. tunakushukuru sana, mungu yuko pamoja na CDM, yule mkurugenzi alikuwa anadhani anaikomoa chadema, eti wanainchi waichukie chadema, hakuna cha maendeleo mpaka ccm wapewe umeya, haya mmepewa, ni ngumu kunielewa nameandika nini. sasa kabwe leteni maendeleo jijini ww si ndiyo mwakilishi na msimamizi wa ..M?, na wale Madiwani wa CUF mmeusaliti upenzani kwa kuiunga nkono ccm, watz wameona rangi yenu subirini 2015. tushukuru hata kwa kuyafukuza yale mapandikizi
 
Yale yale ya "Sungura na sizitaki Mbichi hizi". Yanayosemwa na mleta mada ndo uozo unaopigiwa kelele na upinzani upo kila sehemu.

Unaaminisha kuwa CDM imeshindwa kihalali? Kama hapana, kwa nini ukubali kupoteza haki ya kuwatumikia waTz wanaokabiliwa na uozo ulioutaja? Kama ndiyo, CDM inafanya mbio za sakafuni ambazo huishia ukingoni tu ambapo magamba wanazidi kupaa angani.

Hili ni funzo kwa CDM kujiassess wapi wamekosea, katika msafara uliojaa matumaini tele ya kutwaa dola lakini kumbe waTz hawajawakubali kama mnavodhani.
 
Kwa point hiyo nimekupata,nilifikiri unajoke.ccm wasi furahie nafasi ya umeya mpaka wakajiona kama wamechukua urais,
 
Back
Top Bottom