Mwanza ni jiji la miamba lililokwamishwa kuwa mwamba wa majiji?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Ni mji mzuri uliozungukwa na miamba. Wanapaita "Rock City". Hilo ndilo jiji la Mwanza.

Nakubali, ni jiji zuri, lakini pangeweza kuwa pazuri zaidi.

Kuna maeneo yaliyopangiliwa vizuri, kwa namna bora na ya kuvutia. Lakini kuna maeneo ambayo yanaashiria Mipango Miji walikuwa likizo pindi yakiendelezwa! Chukulia mfano, kwa wale waliofika Mwanza, maeneo ya Mabatini na Kitangiri!

Inasemekana, kama maeneo ya milimani - Mabatini, n.k., yangejengwa kisasa, yangeweza kupafanya Mwanza kuwa jiji lenye mvuto wa kipekee ndani na nje ya Afrika. Wanadai, pangefanana na Uswizi. (Sijui Uswizi palivyo, bado sijafanikiwa kutia miguu yangu huko).

Miaka ya nyuma, inavyosemekana, aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kipindi hicho, alitaka kulitekeleza hilo wazo la kupafanya Mwanza jiji la kipekee kutokana Jiografia yake. Alitaka mji wa Mwanza uwe "mwamba" wa majiji.

Alianzisha mkakati wa majengo ya kifahari maeneo ya milimani. Kwa kuwa watu wengi walikuwa hawajajenga maeneo hayo, alitaka wale wasiokuwa na uwezo wa kujenga nyumba za kifahari milimani wafidiwe ili kupisha wenye uwezo huo. Lakini kabla ya kuifanikisha ndoto yake, wanasiasa walipeleka malalamiko chamani kuwa RC anataka kuwakosesha kura kwa kuwazuia wananzengo maskini kujenga milimani.

Kilichofuatia? Alipigwa "stop" na hiyo ndoto ikaishia hapo.

Sikatai kuwa Mwanza ni pazuri, lakini wazo la RC wa wakati huo lingetekelezwa, pangekuwa jiji la kipekee.

Sidhani kama wakazi wa kipato cha chini wanafurahia kuishi milimani jijini Mwanza.

Kwanza, baadhi ya nyumba zipo juu sana milimani kiasi kwamba hazifikiki kwa gari.

Pili, baadhi ya nyumba zipo kwenye mawe ambayo yanahatarisha usalama wao. Kuna mwaka jiwe lilimeguka na kwenda kuparamia watu waliolala ndani, nafikiri alikufa mtu mmoja.

Najiuliza, Serikali haiwezi kuwafidia watu wanaoishi milimani halafu maeneo hayo yafanyiwe uwekezaji wa majengo ya kifahari?

Ndoto ya kufanya maeneo ya milimani jijini Mwanza kuwa na majengo ya kifahari yatakayopapendezesha itakaa ije kutimia?

Itawezakana Mwanza, jiji la miamba kuja kuwa "mwamba" wa majiji barani Afrika?
 
imeshindikana kwa jengo la uwanja wa ndege ambalo lingekuwa icon ya jiji sembuse....
 
Watu wa pale wa Hali duni ndo wameua ukuaji wa Jiji Lao wao wenyewe, ukiwa mgeni ukaenda Mwanza kuanzisha mradi, wafanyakazi wako lazima wakukomoe maana kwanza wataiba faida Kisha watakula mtaji hadi mradi ufe uondoke! Akili za kimaskini zimejaa watu wengi kule!
 
Back
Top Bottom