CHADEMA furahieni kupoteza umeya wa jiji la Mwanza, ni bahati sana kwenu

Nidhamu ni muhimu sana, bila nidhamu hakuna kitu cha maana kinaweza kufanyika. Ni heri kukosa Umeya laikini kudumisha nidhamu ambayo itasaidia kujenga chama imara kwa mustakabali wa taifa.
 
Mtoa mada hongera sana kwakutoa mawazo yako kama wewe, safi sana.
jambo la msingi hapa ilikuwa kuungoa huo umeya toka kwa hao magamba na kufanya kile CDM inacho hubiri kila siku kwa wanachi juu ua utendaji mbovu uliopo katika halmashauri zetu,hususani hapo MWZ.
kusema wafurahi kukosa Umeya ni kuwanyima mengi watu wa MWZ na maeneo mengine likiwamo swala zima uwajibikaji kwa viongozi tuanowachagua.
hapa naona kabisa kwamba cdm inatakiwa ikubali uzembe ulifanyika/upo kwao pia, na hasa sala zima la kutueleza nini kinakwamisha hayo ulosema na wao wamefanya nini kwa kipindi walichopewa hiyo nafasi japo kwa huo mwaka 1.
Elezeni ukweli wa tatizo na utatuzi wake unapatikanaje. siyo mpaka mshindwe ndo mankuja na nyuzi nyiiingi za kujipoza hapa.
 
Sizitaki mbichi hizi...
Kwanini ugombee kama hutaki?
Baraza la madiwani lina nguvu kuliko Mkurugenzi, kama Mkurugenzi kikwazo kwanini baraza lisitumie nguvu zake kumtoa?
Again, sizitaki mbichi hizi...
 
Yale yale ya "Sungura na sizitaki Mbichi hizi". Yanayosemwa na mleta mada ndo uozo unaopigiwa kelele na upinzani upo kila sehemu.

Unaaminisha kuwa CDM imeshindwa kihalali? Kama hapana, kwa nini ukubali kupoteza haki ya kuwatumikia waTz wanaokabiliwa na uozo ulioutaja? Kama ndiyo, CDM inafanya mbio za sakafuni ambazo huishia ukingoni tu ambapo magamba wanazidi kupaa angani.

Hili ni funzo kwa CDM kujiassess wapi wamekosea, katika msafara uliojaa matumaini tele ya kutwaa dola lakini kumbe waTz hawajawakubali kama mnavodhani.

watanzania bado wanaiamini cdm. Aliyechagua meya sio watanzania ni madiwani. So cdm bado,iko,miyoyoni mwa watanzania
 
Kama aliyosema mtoa mada hii ni kweli, basi nawasikitikia sana wakazi wa Mwanza, kwangu nipo kinyume kidogo naye. bora Chadema wangepata na katika msuguano ndipo mambo yangeenda, lakini kwa hali hii (kama ni kweli) Mwanza haitakuwa na hadhi ya kuitwa jiji.
 
Hakika mtoa mada, wewe umetufungua. tunakushukuru sana, mungu yuko pamoja na CDM, yule mkurugenzi alikuwa anadhani anaikomoa chadema, eti wanainchi waichukie chadema, hakuna cha maendeleo mpaka ccm wapewe umeya, haya mmepewa, ni ngumu kunielewa nameandika nini. sasa kabwe leteni maendeleo jijini ww si ndiyo mwakilishi na msimamizi wa ..M?, na wale Madiwani wa CUF mmeusaliti upenzani kwa kuiunga nkono ccm, watz wameona rangi yenu subirini 2015. tushukuru hata kwa kuyafukuza yale mapandikizi
Kunya anye kuku akinya bata kaarisha!
 
Nikiwa kama mkazi wa kudumu wa Mwanza na ninayeitakia mema CDM katika harakati zake nimefurahishwa sana na CDM kupoteza kiti cha umeya wa jiji. Hii itawapa furs nzuri sana CDM kuepukana na lawama za hali ya juu huko tuendako. Jiji la Mwanza chini ya mkurugenzi aliyepo sasa Bw Wilson Kabwe kupata maendeleo ni ndoto za mchana, hata kama Meya atakuwa Tundu Lissu au my favorite Mnyika. Ili Meya wa jiji afanye kazi yake vizuri anatakiwa kuwa na timu nzuri na yenye mtazamo wa maendeleo toka upande wa halmashauri, kwa Mwanza hilo halipo. Ukienda jiji la Mza utashangaa sana kuona wafanyakazi waliojaa mtazamo wa rushwa na uvivu wa hali ya juu. Kiburi kiko kwa muhudumu wa ofisi hadi mkuu wa idara, mkurugenzi ndio muasisi wa kiburi. Huyu jamaa ana nguvu kuliko waziri mkuu Pinda, anachoamua yeye hakuna wa kuuliza au kupinga. Madiwani wote wa CDM wallop ajitokeze mmoja humu jukwaani na kusema alipingana hadharani na Kabwe!!
Jiji lina ofisi za hovyo, wafanyakazi wamebanana ofisini, wanazurura kutwa nzima kwenye makorido, hakuna customer service kabisa, vyoo ni vichafu hadi aibu... Meya gani ataleta ,maendeleo katika mazingira hayo, heir kuwaachia CCM waendelee kushindwa. Wakuu wa idara jiji pale hawakai ofisini wanakimbizana na posho tu kila siku! Nani atakaa na madiwani wa CDM kupanga na kutekelezeka mipango ya maendeleo wakati watendaji ni wavivu na wabinafsi namna hiyo. Furahieni kupata fursa nzuri ya kujitenga na utendaji mbovu wa Kabwe hadi wakati muafaka utakapofika. Meya na mkurugenzi wanatakiwa kufanyakazi kama timu, umeona wapi timu inayochanganya Mwizi na Mkimbiza Mwizi au mpambanaji wa ufisadi.

Sidhani kama CDM wanalo la kujivunia katika mwaka mmoja na nusu wa umeya, Kama lipo naomba nikosolewe. Barabara ni za mavumbi na nyingi hadi Leo greda halijapita toka mvua zilipoisha. Wakati Pinda kaja Mza nilikutana na greda linatengeza barabara ya Buswelu Kiseke saa 4 usiku na madiwani wa CDM huenda walishiriki kuhalalisha huu usanii Kama walivyoshiriki kuhalalisha ujenzi wa barabara ya lami kwenda kwenye hotel moja tu ya Malaika yenye urefu wa Kilometa 10 kwa ajili ya hotel ya vyumba 24 wakati maelfu ya wakazi wa Buswelu hawana barabara hata ya kiwango cha vumbi. Mkandarasi jasco yup hadi leo site anajenga barabara kwa fedha za msaadanwa benki ya dunia kwenda kwenye hotel ya tajiri mmoja

Ni kwa mazingira hayo Mimi Ulukolokwitanga Ng'wizukulunzungu nimefurahishwa na nafasi kifisadi kurudisha kwa mafisadi hadi katiba mpya itakapoweka wazi nafasi ya meya na mkurugenzi[/

Wengi mmesema sana, naomba niwaunge mkono kwa aibu Watanzania tunayoipata tukiwa Mwanza. Naomba nijikite kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza! Kwa kweli uwanja ule ni aibu sana, kale ka nyumba mpaka leo ndiyo kanatumika na viongozi wa CCM wanapita kila siku. Siku moja nikiwa nasubiri ndege kurudi Dar, pembeni mwangu niliwasikia watu wawili raia wa kigeni-bila shaka walikuwa wa-nigeria kwa rafusi yao, wakibeza kwamba itawezekana vipi aka kachumba ndiyo ofisi ya uwanja wa ndege katika jiji kubwa la Mwanza???? Mimi nilivyosikia hivyo nikakaa kimya nikajifanya siyo mtanzania ili kukwepa hiyo aibu! Sasa wewe jiulize inamaana tatizo hilo huyo mkurugenzi wa jiji na viongozi wao hilo hawajaliona?????????
]
 
but all in all this shall remain as a critical challenge to CDM and they do suppose to accept it for future prosperity!
 
Mtoa uzi laiti Dr Slaa angejua unapatikana wapi angekufuata akunyanganye na kadi yenyewe ya CDM.

Hivi wewe nikuulize uliwahi kusikia wapi cdm wakilalamika kuhusu meya wa mza alipo pigwa chini ? tafakari chukuwa hatua

ndio utajua nini maana ya akili ndogo kuongoza akili kubwa
 
Hao madiwani inawezekana siyo watanzania kweli, maana yeyote aliye mtanzania na mwenye kupenda maendeleo asingeweza kuipigia kura CCM (Mafisadi), mwaka 2015 tutapambana sana na lazima tuikomboe nchi yetu.
 
Mods msiunganishe hii uzi na zile nyingine hii inajitegemea na najua Dr Slaa ataiona na kukubaliana na mimi kwani ni muungwana

Thank you for bringing this info. In fact for those who don't know Kabwe, the guy while in Mbeya City managed to accumulate a lot of wealth through fishy transactions and the least of his belongings is a mansion (ghorofa 2) in SAE area Mbeya hired to Marie Stopes. I agree with you this guy is a mess to all the people in Mwanza.
 
Haina haja ya kuleta ushabiki kwny mambo muhimu wakuu.
CDM ina haja ya kujiangalia kilichopelekea kushindwa. Ikiwa wapiga kura walewale waliomuweka meya wa CDM madarakani, wamemuweka GAMBA, something is wrong within CDM itself.

Kushindwa ni kushindwa, kauli zinazotolewa humu na wanajamvi hazitoshi kuficha mapungufu yaliyojitokeza. Aidha CDM ipinge matokeo hayo kama anavotaka kufanya Dr. Slaa au kukubali kuwa kelele za CDM ni za debe tupu, hazijatosha kuwashawishi waTz walio wengi kama inavoonekana kinadharia hivyo ikija tokea hivi 2015 wasije kumtafuta mchawi...

Huu ni ukumbusho tu, utawafaa wenye kukumbuka.
 
next time tu bila shaka. Heri lawama kuliko fedheha

Sawa kabisa! Uchafu / uozo wa Mkurugenzi ndo ulimfanya Manyerere kuonekana dhaifu akiwa Meya, matokeo yake Madiwani wa CDM wakaliona hilo na kulifanyia kazi japo na CCM waliamua kudaka hoja na kuivalia njuga.
Kosa walofanya CDM ni kutokuwa na solidality katika kuhakikisha makosa hayo wanayakemea na si kuyachukulia maamuzi kama yaliyochukuliwa; na hapo ndo tunapowaona madiwani wawili ambao au walikuwa wamepandikizwa na CCM au ni njaa zao ndo zimeleta hiki tunachokiona leo.
 
Jiji la mwanza kwetu linasikitisha sana hasa ukizingatia tunakila kitu cha kujivunia kuna aina nyingi za viwanda, ziwa, pamba, lakini nikiangalia mbeya hakuna kitu cha maana nje ya kahawa na chai ambayo si wananchi kwa asilimia kubwa ni wawekezaji lakini sisi ndio kwanza tunazidiwa mapato na Mbeya ni aibu kwa mkurungezi kwa maoni yangu ni bora aondoke aje mwingine.
 
Haina haja ya kuleta ushabiki kwny mambo muhimu wakuu.
CDM ina haja ya kujiangalia kilichopelekea kushindwa. Ikiwa wapiga kura walewale waliomuweka meya wa CDM madarakani, wamemuweka GAMBA, something is wrong within CDM itself.

Kushindwa ni kushindwa, kauli zinazotolewa humu na wanajamvi hazitoshi kuficha mapungufu yaliyojitokeza. Aidha CDM ipinge matokeo hayo kama anavotaka kufanya Dr. Slaa au kukubali kuwa kelele za CDM ni za debe tupu, hazijatosha kuwashawishi waTz walio wengi kama inavoonekana kinadharia hivyo ikija tokea hivi 2015 wasije kumtafuta mchawi...

Huu ni ukumbusho tu, utawafaa wenye kukumbuka.

Tumia akili kidogo tu uliyonayo,kuna nini cha ajabu hapo wakati inajulikana kura za ccm na ccm B,lazima zingewafanya
washinde ccm.Labda ingekuwa hata ni udiwani ingeshtua kwani anachaguliwa na wananchi wote.Bora kukosa huo umeya
lakini nidhamu kwenye Chama iwepo kuliko watu wengine toka wameanza kupiga kelele za kujivua gamba hakuna mtu,
amejivua au kuvuliwa ndiyo kwanza haohao mafisadi wanachaguliwa kuingia kwenye Nec ya chama.Think Twice"
 
sawa kama unayoongea yanatoka rohoni, isijekuwa ni "sizitaki mbichi hizi"
Nikiwa kama mkazi wa kudumu wa Mwanza na ninayeitakia mema CDM katika harakati zake nimefurahishwa sana na CDM kupoteza kiti cha umeya wa jiji. Hii itawapa furs nzuri sana CDM kuepukana na lawama za hali ya juu huko tuendako. Jiji la Mwanza chini ya mkurugenzi aliyepo sasa Bw Wilson Kabwe kupata maendeleo ni ndoto za mchana, hata kama Meya atakuwa Tundu Lissu au my favorite Mnyika. Ili Meya wa jiji afanye kazi yake vizuri anatakiwa kuwa na timu nzuri na yenye mtazamo wa maendeleo toka upande wa halmashauri, kwa Mwanza hilo halipo. Ukienda jiji la Mza utashangaa sana kuona wafanyakazi waliojaa mtazamo wa rushwa na uvivu wa hali ya juu. Kiburi kiko kwa muhudumu wa ofisi hadi mkuu wa idara, mkurugenzi ndio muasisi wa kiburi. Huyu jamaa ana nguvu kuliko waziri mkuu Pinda, anachoamua yeye hakuna wa kuuliza au kupinga. Madiwani wote wa CDM wallop ajitokeze mmoja humu jukwaani na kusema alipingana hadharani na Kabwe!!
Jiji lina ofisi za hovyo, wafanyakazi wamebanana ofisini, wanazurura kutwa nzima kwenye makorido, hakuna customer service kabisa, vyoo ni vichafu hadi aibu... Meya gani ataleta ,maendeleo katika mazingira hayo, heir kuwaachia CCM waendelee kushindwa. Wakuu wa idara jiji pale hawakai ofisini wanakimbizana na posho tu kila siku! Nani atakaa na madiwani wa CDM kupanga na kutekelezeka mipango ya maendeleo wakati watendaji ni wavivu na wabinafsi namna hiyo. Furahieni kupata fursa nzuri ya kujitenga na utendaji mbovu wa Kabwe hadi wakati muafaka utakapofika. Meya na mkurugenzi wanatakiwa kufanyakazi kama timu, umeona wapi timu inayochanganya Mwizi na Mkimbiza Mwizi au mpambanaji wa ufisadi.

Sidhani kama CDM wanalo la kujivunia katika mwaka mmoja na nusu wa umeya, Kama lipo naomba nikosolewe. Barabara ni za mavumbi na nyingi hadi Leo greda halijapita toka mvua zilipoisha. Wakati Pinda kaja Mza nilikutana na greda linatengeza barabara ya Buswelu Kiseke saa 4 usiku na madiwani wa CDM huenda walishiriki kuhalalisha huu usanii Kama walivyoshiriki kuhalalisha ujenzi wa barabara ya lami kwenda kwenye hotel moja tu ya Malaika yenye urefu wa Kilometa 10 kwa ajili ya hotel ya vyumba 24 wakati maelfu ya wakazi wa Buswelu hawana barabara hata ya kiwango cha vumbi. Mkandarasi jasco yup hadi leo site anajenga barabara kwa fedha za msaadanwa benki ya dunia kwenda kwenye hotel ya tajiri mmoja

Ni kwa mazingira hayo Mimi Ulukolokwitanga Ng'wizukulunzungu nimefurahishwa na nafasi kifisadi kurudisha kwa mafisadi hadi katiba mpya itakapoweka wazi nafasi ya meya na mkurugenzi
 
Back
Top Bottom