Elections 2010 CHADEMA Campaign Machinery

Dr wewe ni mchunga kondoo wa Bwana nafahamu ya kwamba unafahamu nguvu ya maneno na jinsi inavyoweza kuyeyusha mioyo ya watu! Cha kwanza kabisa lazima kampeni ziwe na msisimko! Tafuteni kila mbinu ya kuwavuta watu wahudhurie mikutano ili watakapo kuja ujumbe waupate sawasawa!
Pili wapatikane vijana wa kujitolea wapite kaya kwa kaya! Hili pia lisiwe lile la kawaida kama ni mafunzo hata ya wk moja wapatiwe wapeleke ujumbe maalum ambao chama kinadhamiria watanzania waupate hapa ikiwezekana kwa posho ya mlo mmoja wapewe! Hili litasaidia sana ku-mobilize vijana wenzao, pili wananchi watapata nafasi ya kujadiliana ana kwa ana katika vikundi vidogo vidogo! Lengo hapa ni kuifikia hadhira kubwa zaidi Hasa hasa vijana walioko mashuleni na katika vyuo! Hii ilifanikiwa sana kwa Obama.

Kingine ambacho ni cha muhimu zaidi ni fund! Obama kampani ilikuwa fueled na vimichango kidogokidogo kutoka kwa watu wenye mapenzi mema! Yes we can do it watanzania tuko tayari kuchangia hizo sh mia tatu kinachohitajika ni uhamasiji tu!

Mwisho kabisa ni kwamba, Katika mapambano only the best ndo hushinda mbinu, mipango makini inahitajika . Hakuna kisichoshindikana! Yes we can!!
Asante E the T ni kweli nguvu ya chama ni vijana. Chadema isilale time is not on our side. CCM wana uwezo wa kipesa kampeni yao inaongozwa na nguvu ya pesa na ukubwa wa chama lakini si scientific campaign.

Najua Chadema uwezo wakipesa si mkubwa lakini wakitumia the little resources walizonazo kwa makini inaweza ikazaa matunda mengi zaidi ya CCM. Kampeni za CCM ni sawa na shamba kubwa bila mbolea mazao yake yanaweza kulingana na shamba dogo lenye mbolea.

Kama Chadema wakiigawa nchi kikanda za uchanguzi inaweza kusaidia kuliko ku centralize kampeni. Kwa mfano kuwe na kanda sita kama nilivyoshauri, kila kanda wachaguliwe vijana kama 100 au 200 wapewe mafunzo ya kukampeni nyumba kwa nyumba hii inafanyika hata katika nchi zilizoendelea Obama alifanya na Cameron pia alifanya.

Kama alivyosema E the T hao vijana wapewe nyezo kama vipeperushi baiskeli nk ikiwezekana hata posho ya siku. Kuwe na center ya kampeni kwa kila kanda, kama Chadema hakina ofisi sehemu hizo ikiwezekana kigharamie kukodi vyumba au hata nyumba kwa kipindi cha miezi minne hadi sita , na hicho kiwe kituo cha kupatia informations zote za kanda hiyo to and from the Headquarters Office HQ.

Ninacholenga ni effective and scientific campaign, mawasiliano yawe ya hali ya juu na ya haraka, wasitegemee sana mawasiliano ya simu, effective communication is physical contact. Kama Chadema watakuwa na uwezo wa kupata helicopta mbili au tatu, wakati zingine zikiwa kwenye presidential campaign team helikopta moja iwe ya kitengo cha communications kazi yake ni kukusanya informations tu kutoka sehemu mbalimbali hasa kwenye vituo vya kanda za uchaguzi. Hii inawezekana.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Sabi Sanda Hongereni sana kwa kazi kubwa mnayofanya ya kuikomboa nchi yetu.

Kama Mtanzania naomba, PAMOJA NA MAMBO MENGINE, mniruhusu kupendekeza yafuatayo ili yawasaidie katika kutimiza ndoto ya kushinda uchaguzi mwaka huu wa 2010.

1. ANZISHENI NA FUNGUENI VITUO NA SEHEMU MAALUMU KILA KONA YA NCHI YETU ZA KUKUSANYA MICHANGO YA FEDHA TASLIMU TOKA KWA WATANZANIA AMBAO HAWAWEZI KWENDA BENKI KUWEKA FEDHA KWENYE AKAUNTI ZA CHADEMA. Katika mpango huu lengo linapendekezwa liwe ni kukusanya ANGALAU shilingi elfu moja kila wiki toka kwa kila Mtanzania. Sehemu hizo zinapendekezwa ziwe wazi kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa tisa mchana ili fedha itakayokusanywa siku husika iweze kupelekwa benki siku hiyohiyo kabla ya saa kumi jioni. Sehemu hizi ziwe na MAKASHA maalumu yaliyo na kufuri maalumu ambapo kila mchangiaji atakuwa anatumbukiza mchango wake. Kwa upande huo huo mnaweza pia kuongea na benki za CRDB na NMB ili katika kila tawi la benki hizo kuwe pia na HAYO MAKASHA MAALUMU ambapo kila mchangiaji badala ya kupanga foleni atakwenda tu kuweka mchango wake katika KASHA MAALUMU na kisha kuondoka. KILA IJUMAA AU JUMAMOSI YA WIKI HUSIKA MAKASHA HAYO YAWE YANAFUNGULIWA NA KISHA FEDHA ZILIZOPATIKANA KUWEKWA BENKI KWENYE AKAUNTI HUSIKA NA TAARIFA RASMI KUTOLEWA KWA WATANZANIA WOTE.

2. CHADEMA inunue muda wa angalau saa 5 kila wiki katika redio zetu hasa TBC Taifa, Radio One na RFA ili kuweza kuzungumza na Watanzania moja kwa moja kila siku kwa angalau nusu saa. Na kila siku asubuhi kwa muda usiozidi dakika 7, Dr. Slaa awe anazungumza na Watanzania kupitia Televisheni na Radio.

3. Pindi kampeni zitakapoanza rasmi CHADEMA iwe inafanya matembezi ya mshikamano kila Jumamosi ya Kilomita MBILI ambapo kila mshiriki ataombwa awe anachangia shilingi elfu tano tu toka kwake na toka kwa wadhamini wake.

NITASIKITIKA SANA KAMA JAKAYA ATASHINDA UCHAGUZI MWAKA HUU. BINAFSI NIMEMWANDIKIA SANA KWA NJIA WA EMAIL NA BARUA ZA KAWAIDA KAMA RAIS WANGU. ILA NASIKITIKA SANA MAWAZO YANGU HAYAJAFANYIWA KAZI. NITASHUKURU SANA KAMA ATAWEKA HADHARANI EMAILS NILIZOMWANDIKIA NA BARUA YANGU YA TAREHE 03/03/2006 ILI RAIS AJAE AWEZE KUYAFANYIA KAZI HAYO MAWAZO, AMBAYE KWANGU MIMI NI WEWE DR. W. SLAA

Shukrani Sabi Sanda
 
Back
Top Bottom