CHADEMA Arusha yatoa mkono wa pole kwa jeshi la polisi Arusha

JESHI la Polisi nchini limekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuonyesha ukomavu wake kisiasa kulikodhihirishwa na kitendo chake cha mchango wa sh 200,000 za rambirambi kwa ajili ya askari Kijanda Mwandu mwanzoni mwa wiki iliyopita mkoani Arusha.

Akipokea mchango huo wa rambirambi kutoka kwa viongozi wa CHADEMA, mkoa wa Arusha, jana, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa mkoa, Thobias Andengenye, alisema kitendo cha CHADEMA kujitokeza na kushiriki nao katika msiba wa askari wake, kitafungua upya ukurasa wa mshikamano baina ya pande hizo mbili.

Kamanda Andengenye alisema pamoja na polisi kufarijika kwa kitendo cha CHADEMA kuungana na familia, ndugu na jamaa wa marehemu, hatua hiyo imedhihirisha kuwa jeshi hilo na marehemu Mwandu wanajituma kuwatumikia wananchi kwa moyo na kwamba hakuna chuki baina ya pande hizo mbili.

"Licha ya tukio hilo kudhihirisha kuwa makundi mbalimbali ya kijamii yanatambua na kuthamini mchango na umahiri wa marehemu kiutendaji wakati wa uhai wake, jambo kubwa ambalo litafungua ukurasa mpya kati ya polisi na CHADEMA ni kwamba mchango huu umedhihirisha kwamba hakuna chuki wala uhasama kati ya jeshi letu na chama hiki kikuu cha upinzani kama watu wengine wanavyofikiri," alisema Kamanda Andengenye.

Alifafanua kuwa wakati mwingine polisi na CHADEMA wamekuwa wakihitilafiana katika utekelezaji wa harakati, shughuli zao za kila siku na usimamizi wa sheria ambapo wakati mwingine hujikuta wakikabiliana bila kukusudia.

Kamanda Andengenye alisema fedha hizo zitaandikiwa taarifa na kuwasilishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema, ambaye atapanga utaratibu wa kuzifikisha kwa familia ya marehemu Kijanda Mwandu aliyezikwa nyumbani kwao Magu, mkoani Mwanza, wiki iliyopita.

Msafara wa viongozi wanne wa CHADEMA waliokabidhi ubani huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, aliyeongozana na Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA katika Baraza la Madiwani Manispaa ya Arusha, Isaya Doita; Mwenyekiti wa Baraza la wanawake (Bawacha), wilaya ya Arusha, Gloria Shio; na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wilaya, Sarah Fundikira ambao kwa pamoja walielezea kusikitishwa na kifo cha askari huyo aliyejitolea maisha yake kupambana na kudhibiti uhalifu.

Nanyaro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi alisema CHADEMA kama wadau wa amani, utulivu na ulinzi wa raia na mali zao mkoani Arusha, wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha askari huyo pamoja na kujeruhiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Faustine Mafwele, katika tukio lililotokea Januari 3, mwaka huu, eneo la Shangarai, wilayani Arumeru.

"Fedha hizi kidogo ni mchango wa viongozi, wanachama, wapenzi wa CHADEMA na wananchi waliohudhuria mkutano wetu wa hadhara kuadhimisha kumbukumbu ya waliouawa na kujeruhiwa katika tukio la maandamano ya Januari 5, mwaka jana," alisema Nanyaro.

SOURCE:TANZANIA DAIMA
 
Ni sawa. Wakati mwingine Polisi ni watu wazuri na wakawaida kabisa rohoni mwao. Ubaya wao mara nyingi ni pale wanapoteleleza amri za walio nje ya tukio halisi. Ndo mana katika machafuko ya Arusha wapo polisi waliowasaidia baadhi ya waandamanaji kutokukamatwa.
 
Nimeipenda hii inaonyesha ni jinsi gani CHADEMA inajenga mahusiano mema kwa jamii inyoizunguka Big up Chadema Arusha
 
Viva CDM chama cha watu makini!!!
Adengenye afanye awezavyo amwamishe kikazi yule mjinga wake OCD zuberi.
 
Jeshi la polisi Tz huwa hawana tatizo na CDM. Tatizo ni kwamba wanatumiwa na mafisadi kwa kujua au kwa kutokujua ili kuizima harakati za cdm za kudai uhuru wa nchi kutoka kwa mkoloni mweusi. Mungu si Athumani polisi wetu wameanza kuelewa soma mwisho wa siku watasimama na kutetea maslahi ya waliowengi.
Mungu Ibariki Tz, Mungu ibariki cdm. Amen!!!
 
Nimeipenda hiii ya CHADEMA kutoa mchango siku zote mtu akifanyia ubaya mlipe kwa wema .

Nawaomba Polisi wote waliosalia kuiga mfano mzuri wa Kijanda maana alikuwa mtu wa watu na asiyependa maovu, imeniuma sana..jamani nimerudi leo baada ya kuwa kifungoni kwa siku kazaa... cjui akina FF na Ms wameendelea kuwapo au ni mimi tu nimeonewa?:poa
 
Usifikiri hiyo ndio Rushwa eti Mkiandamana bila kibali na POLISI wakisema acha kama hamtiii RISASI kwa kwenda mbele. Cha msingi ni mfuate taratibu na sheria za nchi.

Acha ujinga wewe mtoto wa kimasai, usiwatishie watu mabomu na risasi. Hayo mabomu na risasi mboma wengi tunajua kutumia. Hujajifuna kitu kwa yale yanayotokea Misri, Tunisia, Libya na Siria. Fikiri mambo kwa kutumia ubongo wako na siyo masaburi yako.
 
Tatizo la polisi liko kwa wakubwa zao(mwema na wenzake) kuwa na kadi za ccm na kutii kila kitu wanachosema. HONGERENI CDM KWA KUONYESHA UBINADAMU KWA RAIA WENZENTU
 
Back
Top Bottom