CHADEMA Arusha tishio kwa CCM Serikali za Mitaa

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa Wa Arusha kimekutana na kujadili changamoto za urejeshwaji wa fomu za wagombea wake Katika nafasi ya Serikali za Mitaa Kitongoji na Vijiji.

Aidha, chama hicho kimebaini kuwa zoezi hilo lilifanyika bila kuwepo kwa demokrasia kwani wagombea wake walikuwa wananyanganywa fomu na kuchanwa kwa kutumia mabavu huku wakitishiwa kwa bastola kupitia kwa makada Wa CCM

Akizungumza na vyombo vya habari Katibu wa CHADEMA Arusha Innocent Kisanyage Amesema kwamba makada wa chama chamapinduzi CCM wamekua wakitumia nguvu kubwa kunyanganya Fomu za wagombea na kuchana kwa kushirikiana na wasimamizi wa vituo huku watendaji wa Kata wakikimbia vituo vyao vya kazi .

Amesema kitendo hicho kinaonyesha kwamba CHADEMA Mkoa Wa Arusha bado ni tishio kubwa kwakua inatumika nguvu nyingi kuhakikisha kwamba wanashindwa kuwaweka wagombea.

Aidha Baadhi ya wagombea walio nyanganywa fomu zao na kupigwa mapanga na wengine kunyooshewa bastola wamesema walifika kituo kikuu cha Polisi jijini Arusha lakini walijibiwa watoe fomu za kugombea ndio wapate P 3 ili waweze kupatiwa matibabu.

Sakata la urudishwaji wa fomu kwa wagombea wa vyama vya siasa limebubujikwa na sintofahamu kwani watendaji wamekua wakiwarudisha wagombea wa upinzani kwa kile wanacho dai kwamba hawana sifa za kugombea nafasi hizo.

Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema amesema kwamba kitendo hicho nicha kihuni kwani CCM wanatumia nguvu kubwa kuaharibu uchaguzi na kama wanataka upinzani wajitoe waseme kwamba uchaguzi ni wa chama kimoja tu.

Lema ameongeza kwamba, awapo tayari kuona uchaguzi mdogo unatumika nguvu kubwa kuwaumiza wagombea kwa kunyooshewa bastola mapanga kwani nchi hii ni ya kila Mtanzania na sio mtu mmoja peke yake.

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elisa Mungure amesema mpaka sasa vijiji vyote katika jimbo la Arumeru Magharibi na mashariki Munduli akuna mgombea aliyefanikiwa kurejesha fomu na kumekuwepo na uhuni mkubwa kwa kutishiwa na wengine kukimbiwa na watendaji wa kata.

Uchaguzi huo Mdogo kabla kuelekea uchaguzi mkuu mwakani tayari umeonyesha kwamba CCM aikubaliki ndio maana wanatumia jeshi la Polisi kuvuruga uchaguzi huo

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha Msena Bina amesema akuna malalamiko yoyote walio pokea kutoka kwa CHADEMA wala wagombea wa nafasi hizo .
IMG_20191102_124838_5.jpeg
IMG_20191102_125110_5.jpeg
IMG_20191102_130035_1.jpeg
 

Attachments

  • IMG_20191102_130035_1.jpeg
    IMG_20191102_130035_1.jpeg
    37 KB · Views: 1
Arusha walisha jitambua zamani, tangu mfumo wa vyama vingi ccm haijawagi kushinda chaguzi yoyote Arusha, wanazo shinda huwa WANATANGAZWA WASHINDI lakini si kushinda kwa gaki, viongozi wanaogopa kutumbuliwa kwa aibu watayoipata wameamua kuleta upumbavu, msweeee..
 
Watashindana lakini hawatashinda, Chadema ni Mpango wa Mungu kwa nini Magufuli
ni mgumu sana kuelewa mambo mepesi hivi?

Anaendeea kushupaza shingo
 
nimeoteshwa kwamba CCM itashinda kwa 97% uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na mitaa yote Arusha kuchukuliwa na CCM
 
Watashindana lakini hawatashinda, Chadema ni Mpango wa Mungu kwa nini Magufuli
ni mgumu sana kuelewa mambo mepesi hivi?

Anaendeea kushupaza shingo
Unajua huku arusha wapinzani wengi hawakujiandikisha. wengi waliojiandikisha ni ccm. Huu ndio ukweli. kipindi wanaandikisha chedema ilikuwa kimya ikawa inafurahia watu kwenda kutojiandikisha kumbe ndio inajichimbia shimoni. ukweli ndio huo lets wait muone watu watakaoende kupiga kura. sasa sielewi hata hizo kampeni watampigia nani?
 
Siku ya matokeo uje hapa maana nyie misukule ya ufipa kwa kukimbia jukwaa hamjambo
 
Back
Top Bottom