Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,066
- 4,085
Anakaribishwa sana kwenye chama cha kizalendo na chenye dhamira ya dhati kuboresha maisha hali ya maisha ya mtanzania wa chini, kuondoa rushwa na kuwafikisha mahakamani wabadhirifu
Mbunge mteule wa A.Mashariki Makongoro Nyerere amesema kura za wabunge wa CDM ndizo zilimfanya kushinda ubunge huo.Makongoro amesema wagombea wenzake kupitia CCM walitishia ushindi wake kutokana na jinsi walivyokuwa wanatembeza rushwa.
Makongoro amesema alikuwa hana hata nauli ya kwenda Dodoma lakini alimtegemea Mungu.Amesema CDM walipotaka kususia uchaguzi ule aliamini mwisho wake ulikuwa umefika kwani kura zote za wabunge wa CDM zilikwenda kwake.Amesema ni ngumu sana kugombea nafasi yoyote kupitia CCM kama huna hela za kugawa.Makongoro ameendelea kusema kwamba chuki ya rushwa waliyo nayo wabunge wa CDM ndiyo iliyomuokoa kwani anaamini ni vigumu wabunge wa CDM kuchagua mtoa rushwa.Amemalizia kwa kusema shukrani yake kwa CDM ni kwa yeye kuwatumikia wananchi wote bila ubaguzi wowote.
SOURCE:TANZANIA DAIMA