CCM Zanzibar yasisitiza wazanzibari wasiokubali muungano uliopo warudishe kadi za chama!

Hana lolote yeye ni kibaraka tu kwa ajili ya kuimaliza z'bar na sio kweli kama ccm z'bar imetoa tamko hilo seif iddi hana uwezo huo kichama kutoa kauli hiyo labda kauli hiyo engeitoa kiserekali halafu afahamu ile katiba ya nchi sio ya ccm kila mmoja ana mawazo yake kupewa mke kitope isiwe sababu ya kutupandia vichwani wazanzibar
 
At least amesimamia kwenye sera ya chama chake.. Wanachama wote wa CCM ambao wako against serikali 2 watoke CCM.. Karibuni sana CDM ambayo sera zake ni Serikali 3..
 
(kwa mantiki hii CCM ni chama cha kidikteta. nijuavyo mimi chama ni cha watu wote bila kubagu makundi ya aina yoyote yale. Hivyo wanachama wanaweza kubadili sera, mtazamo, itikadi nk kulingana na mapenzi ya watu wote kwa wakati husika

walicho paswa kufanya ni kuwaita wanachama wao kisha wasikilize maoni yao. lakini si shangai ktk hili kwani mabadiliko mengi wanayafanya pasipo kuwahusisha wanachama wao

na hili wataonekana wapo sawa tu
)
Kwa hapo siwezi kukubaliana na wewe kwani ni wazi unapoingia kwenye chama ni kutokana na sera zilizopo tatizo watu wengi wanaingia kwenye vyama kumfata mtu binafsi na ndio maana tumeona migogoro mingi katika vyama au makundi ndani ya vyama kwa sababu za kibinafsi zaidi.Tunapozungumzia chama tunazungumzia sera na itikadi na hiyo hatuzungumzii ccm tu bali ni vyama vyote kama hukubaliani na sera na itikadi za vyama jiondoe usingoje ufukuzwe upate aibu.
Wanasiasa wengi wa sasa hivi sio wanasiasa bali ni wachumia tumbo ndio maana unaona kuna watu wanahama vyama kisa amekosa nafasi ya kugombea uongozi ingawa wakati mwingine wanaweza kuwa na sababu ya msingi lakini mwanasiasa mahiri huwezi kubaki kwenye chama wakati hukubaliani na sera na itikadi za muungano kama unabaki wewe ni mwanachama mamluki, kama vyama vyote vitatekeleza mapendekezo ya Balozi Seifu tutakuwa na vyama vyenye nguvu.Ndio maana pamoja na mfumo wa vyama vingi kufikisha zaidi ya miaka 15 bado tuna utitiri wa vyama na vyama vingi havina nguvu
 
Ma gt kazi kwelix2, hivi mnaelewa tofauti ya katiba na sera za chama na katiba ya nchi? mcahkato ni wa katiba ya nchi!
 
Huwa si busara kutumia vitisho wakati wa uchangiaji wa maoni ya katiba, huyu barozi kapotoka kabisaaa! Hajui afanyalo
 
Ni wakati wa kuchukua mawazo ya wananchi, sio ya viongozi wala ya chama! Mambo ya kizamani yko vichwani mwa viongoz wet
 
Hapa ndipo utawaona wazanzibar walivyo makafiri hakuna atakaye jitokeza , Wote kimya , rudisha kadi kama mna ubavu , tusubiri na kahuli nyingine itakayotoka kwa Mwenyekiti wa Chama , kama ambaye hataki muungano basi na afungashe virago arudi Zanzibar , wote watafyata mikia na ndio utakuwa mwisho wa malalamiko yasiyokwisha ya Wazanzibari
 
..G 55 waliokuwa wakidai serikali ya Tanganyika walitishiwa kufukuzwa CCM, matokeo yake hoja ile ikafa.

..sasa hawa wachague kati ya CCM, muungano, na Zanzibar. kipi kina umuhimu zaidi kwao??

.
 
Mbona hilo lina mantiki? Kama mwanaccm hakubali sera ya ccm anakivua yu uanachama.

Sio kwamba unaweza kupingana na sera za chama ulichopo kwa kupendekeza mabadiliko na kuleta sera-mbadala? Je ni lazima wote mkubaliane na sera zilizopo kwa chama chenu?
 
Sio kwamba unaweza kupingana na sera za chama ulichopo kwa kupendekeza mabadiliko na kuleta sera-mbadala? Je ni lazima wote mkubaliane na sera zilizopo kwa chama chenu?

Ibambasi,

..unatakiwa upendekeze sera mbadala ktk vikao vya chama, siyo mitaani, kwenye vyombo vya habari, au bungeni.
 
Msimamo wa CCM kuhusu muundo wa muungano uko wazi na umekuwa hivyo tangu chama kilipoasisiwa nao ni muungano wa serikali mbili yaani ya Zanzibar na ya Muungano. Hata huu mchakato wa sasa wa mabadiliko ya katiba sio zao la mawazo ya CCM ni mawazo ya wapinzani na wanaharakati wa kijamii. Na ndio maana mtazamo wa awali wa mswaada wa mabadiliko ya katiba uliweka kikomo kwenye mambo yanayojadilika na muundo wa muungano ulikuwa ni moja ya hayo mambo.

Hivyo hawa wanaojiita wana CCM kama kweli ni wakereketwa wa mabadiliko ya muundo wa muungano walitakiwa waanzishe mijadala ndani ya chama kuwashawishi wanachama wenzao na viongozi wao wa juu kuhusu ya mabadiliko ya sera ya CCM juu ya muundo wa muungano na siyo kwa kutumia hii style ya kuweka mitazamo yao kwenye vyombo vya habari. Huwezi kukata tawi la mti uliolikalia na ukategemea kuwa salama.

Vinginevyo busara ya kawaida inawataka hawa wakereketwa wa CCM wanaodai mabadiliko ya muundo wa muungano kujitoa ndani ya CCM ili wapambane wakiwa nje. Huu ndio mkakati uliotumika kuwazima kundi la wabunge wa CCM walijipambanua kama G55 wakidai kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika ndani ya muungano kwenye miaka ya tisini. Walishauriwa kujitoa lakini wote wlifyata mkia.
 
Na kama katika vikao vya chama inashindikana?


Ibambasi,

..huko kwenye vikao unatakiwa utumie hoja kukishawishi chama chako kifuate sera unayoipendekeza.

..ukishindwa kuwashawishi wajumbe na wanachama wenzako, basi unapaswa kufanya mambo mawili yafuatayo.

..mosi, unaweza kuchagua kuwa mtiifu kwa chama chako, na kuendelea kuunga mkono sera husika, pamoja na kwamba hukubaliani nayo.

..pili, unaweza kujitoa ktk chama, na kueleza kinagaubaga sababu za kufanya hivyo. baada ya hapo unaweza kwenda chama chochote ambacho kinafuata sera unayoipendekeza; au unaweza kuanzisha chama chako mwenyewe; au unaweza kuamua kutounga mkono chama chochote.
 
Ibambasi,

..huko kwenye vikao unatakiwa utumie hoja kukishawishi chama chako kifuate sera unayoipendekeza.

..ukishindwa kuwashawishi wajumbe na wanachama wenzako, basi unapaswa kufanya mambo mawili yafuatayo.

..mosi, unaweza kuchagua kuwa mtiifu kwa chama chako, na kuendelea kuunga mkono sera husika, pamoja na kwamba hukubaliani nayo.

..pili, unaweza kujitoa ktk chama, na kueleza kinagaubaga sababu za kufanya hivyo. baada ya hapo unaweza kwenda chama chochote ambacho kinafuata sera unayoipendekeza; au unaweza kuanzisha chama chako mwenyewe; au unaweza kuamua kutounga mkono chama chochote.

JK, nimelipenda jibu lako.
 
Back
Top Bottom