Muungano kama Muungano

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, je, ni namna gani tunasherehekea Muungano huu?

Tunasikia kauli za wanasiasa wakipongeza na kusifia Muungano, namsikia Waziri Jafo akilielezea hatua kubwa iliyopigwa katika kutatua "kero za Muungano"! Lakini siwasikii wananchi wa kawaida wakitoa pongezi kama hizo, kwa nini?

Nawaona wazanzibar wanaotamani muungano uvunjike kwa sababu wanaamini Tanganyika wanautumia kuwanyonya na kuwa huu Muungano ni sababu ya kuwachelewesha kupata maendeleo wanayostahili.

Watanganyika hawajali uwepo wa muungano, wanaona hawaihitaji Zanzibar ili kuendelea na maisha yao.

Hisia za wananchi wa kawaida husikika hasa pakitokea jambo la kero, watu wanatema nyongo zao. Mfano, kuna binti Mtanganyika alirusha ujumbe wa sauti kumsema hayati Maalim Seif wakati tukielekea Uchaguzi ule wa mwisho, matokeo yake zilitumwa jumbe nyingi sana kutoka kwa wazanzibari zikijibu, lakini zilibeba maneno mazito hasa kuwasema Watanganyika, mfano, sauti ya Mama mmoja ilisikia ikisema Watanganyika hawana desturi, na ndio inaaminika kule Zanzibar kuwa tabia mbaya zinapelekwa kule na watanganyika.

Swali, je, hadi sasa bado tunahitaji huu muungano ikiwa lengo kuu la kuanzishwa kwake ni ulinzi, hasa kipindi kile cha vuguvugu la mapinduzi na mapigano ya kugombea uhuru? Sasa hakuna nchi itataka kuivamia Tanganyika, je, bado tunaihitaji Zanzibar?

Kama bado tunauhitaji na sasa ni miaka 59, kwa nini tusifanye kuwa nchi moja kikamilifu na kuwa na serekali moja, na watu wote kuwa na haki sawa kote, badala ya sasa ilivyo kuwa Mzanzibari anaweza kununua ardhi Tanganyika ila kupata ardhi Zanzibar ni hadi kuwa na kitambulisho cha mkaazi, ambacho kinatolewa kwa wazawa tu?

Kuna eneo la Tanganyika, kule Bagamoyo limepewa kwa SMZ na pamewekwa kibao chao!!!! Je, ikitokea muungano umevunjika, nini mustakabali wa eneo hili?

Kwa nini serekali zinakuwa na muhali kukusanya maoni ya wananchi juu ya uhitaji wa muungano?

Kwa watanganyika kukaa kimya juu ya kuutaka au kutokuutaka Muungano, je, ni dalili kuwa hawathamini utanganyika wao kama wenzao wanavyothamini Uzanzibari kuliko utanzania? Maana ni nadra kukuta Mzanzibari anajitambulisha kama Mtanzania kwanza.

Binafsi napenda muungano lakini si kwa namna ulivyo sasa.
 
Leo ni maadhimisho ya miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TA from Tanganyika; NZA kutoka Zanzibar na NIA ni NIA YA MUUNGANO). Katika miaka 59 hiyo kulikuwa na hoja 25 na hoja 17 zimeshashughulikiwa lakini Tanganyika haipo tena eti Tanzania bara huku Zanzibar ikibaki na jina lake. Viva Muungano viva!!
 
ipo siku tanganyika itapinduliwa na zanzibar
Tanganyika imevaa koti la Muungano!. Tangu lini Muungano wa nchi 2 zilizokuwa huru ziliungana halafu zikaendelea kuwa nchi mbili zenye wakuu wa nchi wa wawili?. Tanganyika ipo na itaendelea kuwepo ikiwa imevaa koti la Muungano.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteua ............. kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar.
 
Huu ulikuwa muungano wa Nyerere na Karume na sio watanganyika na wazanzibar

Huu ni muungano wa kisiasa zaidi Kati ya TANU na ASP =CCM

Ni muda wa kudai Tanganyika yetu
Muungano wa marekani na uingereza waliomshinikiza mtu wao Nyerere kuungana na Zanzibar,karume hakuutaka muungano,baada ya mapinduzi Tanganyika ilikua na Askari 300 zenji kumlinda karume,alipoletewa wazo la muungano aligoma,akaambiwa tutaondoa Askari wetu zenji,kishingo upande akakubali
 
Nyerere alikua na akili sana,sema kwenye huu muungano karata hakucheza vzr,
 
Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, je, ni namna gani tunasherehekea Muungano huu?

Tunasikia kauli za wanasiasa wakipongeza na kusifia Muungano, namsikia Waziri Jafo akilielezea hatua kubwa iliyopigwa katika kutatua "kero za Muungano"! Lakini siwasikii wananchi wa kawaida wakitoa pongezi kama hizo, kwa nini?

Nawaona wazanzibar wanaotamani muungano uvunjike kwa sababu wanaamini Tanganyika wanautumia kuwanyonya na kuwa huu Muungano ni sababu ya kuwachelewesha kupata maendeleo wanayostahili.

Watanganyika hawajali uwepo wa muungano, wanaona hawaihitaji Zanzibar ili kuendelea na maisha yao.

Hisia za wananchi wa kawaida husikika hasa pakitokea jambo la kero, watu wanatema nyongo zao. Mfano, kuna binti Mtanganyika alirusha ujumbe wa sauti kumsema hayati Maalim Seif wakati tukielekea Uchaguzi ule wa mwisho, matokeo yake zilitumwa jumbe nyingi sana kutoka kwa wazanzibari zikijibu, lakini zilibeba maneno mazito hasa kuwasema Watanganyika, mfano, sauti ya Mama mmoja ilisikia ikisema Watanganyika hawana desturi, na ndio inaaminika kule Zanzibar kuwa tabia mbaya zinapelekwa kule na watanganyika.

Swali, je, hadi sasa bado tunahitaji huu muungano ikiwa lengo kuu la kuanzishwa kwake ni ulinzi, hasa kipindi kile cha vuguvugu la mapinduzi na mapigano ya kugombea uhuru? Sasa hakuna nchi itataka kuivamia Tanganyika, je, bado tunaihitaji Zanzibar?

Kama bado tunauhitaji na sasa ni miaka 59, kwa nini tusifanye kuwa nchi moja kikamilifu na kuwa na serekali moja, na watu wote kuwa na haki sawa kote, badala ya sasa ilivyo kuwa Mzanzibari anaweza kununua ardhi Tanganyika ila kupata ardhi Zanzibar ni hadi kuwa na kitambulisho cha mkaazi, ambacho kinatolewa kwa wazawa tu?

Kuna eneo la Tanganyika, kule Bagamoyo limepewa kwa SMZ na pamewekwa kibao chao!!!! Je, ikitokea muungano umevunjika, nini mustakabali wa eneo hili?

Kwa nini serekali zinakuwa na muhali kukusanya maoni ya wananchi juu ya uhitaji wa muungano?

Kwa watanganyika kukaa kimya juu ya kuutaka au kutokuutaka Muungano, je, ni dalili kuwa hawathamini utanganyika wao kama wenzao wanavyothamini Uzanzibari kuliko utanzania? Maana ni nadra kukuta Mzanzibari anajitambulisha kama Mtanzania kwanza.

Binafsi napenda muungano lakini si kwa namna ulivyo sasa.
Muungano hauna faida kwa watanganyika bora ufe tuu
 
Tanganyika imevaa koti la Muungano!. Tangu lini Muungano wa nchi 2 zilizokuwa huru ziliungana halafu zikaendelea kuwa nchi mbili zenye wakuu wa nchi wa wawili?. Tanganyika ipo na itaendelea kuwepo ikiwa imevaa koti la Muungano.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteua ............. kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar.
Lakini Tanganyika haina Katiba yake,Haina Bendera ya Taifa lake na Jina Tanganyika halitambulikani na mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom