CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

ndicho unacho ota wewe na Nape! Mwambie Nape atoe maagizo kwa Tendwa

....that is true hapa anayepashwa kushitakiwa ni babu slaa wala sio polisi kwani walikuwa wanatimiza kazi waliyosomea, kama walikatazwa kuandamana kwa nini waliandamana? hii ni hatari kwa nini tusiangalie kenya ilivyokuwa kipindi kile waliokuwa wanapigana na kuuana walikuwa ni vyama pinzani tu,tendwa futa hiki chama cha wauaji
 
Haya Wadau hayo ndio majibu mnayosubiria kutoka kwenye tume ziilizo undwa msitarajie majibu tofauti CDM chukueni option (B) tahariri squire tuu ndio suluhisho
 
Kumbe waliambiwa wasitishe mikutano yao mpaka sensa iishe?

Wanaleta fujo na machafuko halafu wanakuja humu JF kujidai wameonewa? hawa wana matatizo makubwa sana na wakiendelea kuachwa wataitumbukiza shimoni hii nchi, wadhibitiwe mapema sana, hatua nzuri ni kukifuta tu hiki chama.
CCM mlisitisha mikutano yenu?Unafikiri kufuta chama ni kama unavyofikiri?Uliza uelimishwe.
 
Waliosababisha wachukuliwe hatua kali kabisa, nakuunga mkono Nape
Wewe na Nape lenu moja lazima umuunge mkono boss wako!!!!Mliuwa Songea kimyaaa, mkauwa Usa, Arusha CCM kimyaa, mliuwa Igunga kimyaaa, Morogoro mmeuwa kimyaaa,sijui ni mara ngapi mtaendelea kuwauwa Watanzaia???? Ila kila jambo ukae ukijua lina mwisho wake, na nyinyi mtabaki historia kama KANU Kenya!!!!!

Nape Mnauye kawadanganye wale wazee wa vijijini mnaowapa rushwa ya khanga na tshirt wanawapa kura. Sasahv hata watoto wa chekechea wameshawagundua nyie magamba mnataka kuwafanyia nn watanzania walipa kodi. Ur perception on th killings is void ab initio
 
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

Wewe nape unaona matamko yako ya kijinga yanajenga amani,uliposema watu wajiandae na vurugu morogogo na kweli polisi wakaleta vurugu ulikuwa na maana gani, upeo wenu mdogo wa kuongoza ccm isiwe sababu ya kutunyima haki ya kupata sera mbadala.

Iko wapi copy and pastle ya vua gamba vua gwanda vaa uzalendo uliyoianzisha? Hivi unafikiri ccm yako itapona kwa mbinu chafu mnazowafanyia wapinzani?

Nawashauri tumieni sensa kujua wapiga kura wajao wanasifa zipi. Kwa taarifa yako ni wasomi ,yale malaki mliyo yazalisha shule za kata ndio wapiga kura hawadanganyiki na propaganda zenu.

Wengine TANU na CCM ni historia,tunajua mfumo wa vyama vingi tu hivyo ukisema amani wakati polisi ni wa ccm ndio wanaoua watu hatukuelewi na hatutakuelewa kamwe. Habari ndio hiyo
 
Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Huu ni unafiki mbona kule Zanzibar Buibui CCM ilikuwa na mkutano na tamasha la Fiesta liliendelea kule Mwanza wakati huo huo CDM ikiwa katika shughuli za kichama wala si mkutano wa M4C? HUU UNDUMILAKUWILI UFE haraka sana. Shame on you Kijana tarumbeta la magamba.

  • [h=2]CCM na DAUDI MWANGOSI[/h]

    CC:
    Nnauye Jr Ritz chama

    Hivi Nape Hakuiona Hii Picha wakati anaandika hiyo Taarifa yake

    "Kwa hiyo kwa mwaka 2010 Divisheni Four + Divisheni Zero Jumla yake ni 310,826 ====== 88.1%" Albedo Mwenyewe

    Ukiangalia tarehe kwenye hizo picha mikutano ya CCM inaendelea tena kipindi cha sensa ila mikutano ya CHADEMA NO!!!!! CDM walikuwa wanafungua matawi wanarushiwa mabomu na kuuwa waandisha wa habari, Tanzania tunaelekea wapi, serikali ya CCM inatupeleka wapi????

Huyu jamaa nilidhani ni mtu wa maana sana siku za nyuma kabla hawajamtuliza kwa kumpa cheo alichonacho. Kumbe ilikuwa ni uroho wa madaraka tu.Kayapata sasa hivi ndo tunamjua kwamba yupo tayari kuweka ubongo wake mfukoni na kuweka utumbo kichwani, halafu akafikiri kwa kutumia matumbo, kuwafurahisha tu waliomkirimu. Nyekundu ataiita bluu na nyeupe atasema nyeusi, hata kama nafsi yake haiamini kabisa anachokisema!
 
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
Wamevunja sheria gani?Na hii sheria ipo kwa ajili ya CDM tu?Kama ungekua timamu ungeongelea ndani ya chama chenu na kuwashauri kuacha kuwapa mashinikizo Jeshi la polisi wasiharibu kazi zao kwani mnaiongezea umaarufu CDM, then hii mision mlioipanga mjaribu kuibadirisha kwani ilishajulikana kabla kuwa mmepanga kufanya nini kenye hii mikutano ya M4C ili CDM ifutwe na hili limethibitishwa na msajili jana
 
Huyu jamaa nilidhani ni mtu wa maana sana siku za nyuma kabla hawajamtuliza kwa kumpa cheo alichonacho. Kumbe ilikuwa ni uroho wa madaraka tu.Kayapata sasa hivi ndo tunamjua kwamba yupo tayari kuweka ubongo wake mfukoni na kuweka utumbo kichwani, halafu akafikiri kwa kutumia matumbo, kuwafurahisha tu waliomkirimu. Nyekundu ataiita bluu na nyeupe atasema nyeusi, hata kama nafsi yake haiamini kabisa anachokisema!
 
Sena inafanywa usiku? hiyo Fiesta ya mwanza ilikuwa saa ngapi?

Bububu hujui kuwa watawala huko ni CUF na CCM, ulisikia kuna chadema huko? au mshapata japo sheha?
 
Mbona na nyie hamkusubiri sikuchache kuzinddua kampeni zenu huko bububuu? Au sensa haikihusu chama dusky??? Huu nk ujinga tafuteni wajinga wa kuwaeleza sio watanzania wa leo
 
Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.

CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.

Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.

Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Mnauye jijini Mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Chanel Ten Mkoani Iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa Chama cha CHADEMA mwezi September 2 mwaka huu 2012

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

SO WHAT? NYIE SI NDIO MNAWATUMA PILIccm KUUA WATU?....CHAMA CHAKO NA SERIKALI YAKO NDIYO INAYOTUMIA JESHI LA POLISI NA MAHAKAMA KUNYIMA UHURU WA WATZ?....SASA UNAJIPENDEKEZA KWA MTZ YUPI? HUYU WA SASA AU YULE WA MIAKA ILE ULIYEZOEA KUMPA PILAU NA POMBE ZA MKIENYEJI?
 
Siamini kwamba ni kauli ya Nape hii

Aah! Huamini nini mkuu, ulitegemea Nape ajibuje, maana hili dili walikuwa wamelisuka ili chadema ionekane imeua lakini Mungu siyo @Nape Nnauye wameumbuka! Hii hotuba ya Nape inathibitisha ushirika wa Jeshi la Polisi na CCM, ndio maana hata hawajalishutumu Jeshi la police kwa Mauji maana ni washirika wao kazini!
 
Sena inafanywa usiku? hiyo Fiesta ya mwanza ilikuwa saa ngapi?

Bububu hujui kuwa watawala huko ni CUF na CCM, ulisikia kuna chadema huko? au mshapata japo sheha?

Kwahiyo sheria ya kuzuia mikutano wakati wa sensa inaihusu chadema peke yake? Kuwa ccm siyo kibali cha kuacha kufikiri!
 
Back
Top Bottom