CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

Kauli kama hii ni dhahili ombwe la uongozi linatumaliza, Nape haya uliyosema ni kutoka moyoni mwako kabsa na wala hujatumia kilevi? Kiongozi makini anajua kuchagua na kupangilia maneno husika ya kuongea kwa wakati na mazingira husika, kauli za kilevi zinazotoka zinakuja kwetu wananchi wa kawaida kutaka kutughiriba wananchi,

Lakini kaeni mkijua chuki mnayoipandikiza kwa wananchi kwa sababu mnazozijua wenyewe inaua taratibu kama kansa msiposhtuka leo,kesho mtakua mmechelewa
 
itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) mkoani iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu ndg. Daudi mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo. Chama cha mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.

Ccm inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu daudi mwangosi.

vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa taifa letu.

Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi ccm nape mnauye jijini mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya mwandishi daudi mwangosi wa chanel ten mkoani iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa chama cha chadema mwezi september 2 mwaka huu 2012


imetolewa na;
nape moses nnauye chama cha mapinduzi katibu wa nec-itikadi na uenezi taifa.

nonsense!!!!!!!
 
Sualla la sensa lisichukuliwe kisingizio cha kuidumaza CHADEMA. Kwani sensa imekamilika nchi nzima isipokuwa mkoa wa Iringa?

Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na huu UONGO mweupe wa CCM!
Tangu sensa inaanza tarehe 26/08/2012 Watawala hawahawa walisema kuwa zoezi la sensa HALIWEZI KUZUIA SHUGHULI ZA KILA SIKU ZISIMAME! Kwa maana kwamba watu wataendelea kuhesabiwa na shughuli za kimaisha zitaendelea kama kawaida.

CCM wanazidi kujichanganya wenyewe maana kama sensa haizuii shughuli za kila siku kwanini wakomae na kutaka kuzuia mikutano ya nje na ndani ya CDM???Huu ni unafiki uliopitiliza! Maana CCM hawahawa mikutano yao ya Kampeni za Chaguzi za Jumuia zake pamoja na Uchaguzi mdogo kule Bububu imeendelea bila ya kuingiliwa na Polisi! CCM wanamdanganya nani kwa faida ya nani????

Tanzanians of this day are no longer Tanzanians of those Black and Dark continent! They're just watching every move,action and words from CCM and its henchmen(Police,TISS,Magistrate,PCCB etc). Nobody is gonna cheat us!

Hatudanganyikiiii!!!!
 
Ningependa kumshauri ndugu NAPE kwamaba silazima kila siku azungumze kwenye vyombo vya habari , hata kama matukio anayojaribu kuyatolea maelezo yako wazi kwamba muhusika ni serikali na ccm chini ya kivuli cha polisi! Haihitajiki kuwa na Phd kujua utoto ulioko ndani ya siasa za ccm hivi sasa na propaganda za kitoto wanazojaribu kuzitumia kujibu hoja za msingi. Haiingi akilini walioua ni polisi na ISSUE hapa ni mauaji ya kutumia bomu, hivi in this kind of situation mtu anazungumzia kuhusu chadema. Is that the main issue? swali ni kwamaba kwanini polisi waue watanzania for very cheap reasons?Haihitaji akili nyingi kujua ni nani anawatuma polisi, jaribu kuangalia watanzania wote wanalaani polisi EXCEPT ccm , wao wanalaani chadema! Tatizo ninaloliona ccm ni coordination ya mambo yao! Hata kama MPANGO ni kuifuta chadema , basi mjaribu ku organize kama watu ambao mnatumia common sense! Every propaganda ya ccm nowadays hata mtoto wa standard 1 anajua whats going on! Hii ni moja ya hasara za kupeana madaraka kindugu bila kuangalia qualifications, ndani ya ccm there is alot of capable people ambao wangeweza kufanya vyema than what we see and hear nowadays frm the so called ccm speakers! Hivi ndugu yangu Nape unapozungumzia utawala wa sheria, do u exactly know what you are saying? Kuua raia kwa bomu ni utawala wa sheria? au kwako utawala wa sheria is only for chadema to obey what ccm want them to do? Hivi kweli ccm ndio inatuhubiria habari za utawala wa sheria wakati wao ni wavunja sheria namba moja? Mkitaka watu waheshimu sheria inabidi na nyinyi muonyeshe mfano wa kuziheshimu hizo sheria! Sio sheria kwa chadema but ikija kwa ccm it is not applicable! Kujaribu kuzuia haki za watu kwa matendo yasiyohaki hakuwezi kufanikisha lengo lenu la kutotaka kukosolewa! DARKNESS has never won any war against LIGHT, believe me it is just a matter of time when you ccm will realize that!


well said and presented! Utaalamu wa chini kabisa wa propaganda au ni dalili za wazi za kuzidiwa na chadema.
 
Huyo ndio Nape. Kwa umri wake ni kijana ila sura yake na akili yake ni kizee; ndio maana yuko kwa magamba. Shame upon him.
 
Kwa kauli ya tendwa...............mtego wa kwanza wa kuimaliza ccm umeshindikana....naamimi ilipagwa mauaji kutokea, kuna taarifa askari mmoja alikuwa anakataa wasifanye walilokusudia kwa kuwa anamfahamu...lakini haukuweza kuzuia, maana wauaji walitoka mbali.............inteljensia kidogo tu ....ni kwamba malehemu aliwekewa bomu mfukoni, kisha akamatwe nalo au kuwawa kabisa...... Na ccm waifute cdm.......mungu kwaumbua kweupeeeeeee
 
Nashindwa kumwelewa kabisa Nape. Dr. Slaa awajibike kwani ni yeye aliyeua? Kitu cha kujiuliza hapa kwanini CCM na serikali yake inatumia nguvu nyingi kuzuia mikutano ya CHADEMA? inaogopa nini?

Ikiwa polisi wanatumiwa kulinda mikutano ya CCM kwanini hao hao polisi wasitumiwe kulinda mikutano ya CDM. Hapo haki/usawa uko wapi? Je polisi ni kwa ajili ya CCM tu?? polisi inatumia nguvu nyingi kuzuia hiyo mikutano ingetumia nguvu hiyo hiyo wanayoitumia kuhakikisha usalama. Anayetakiwa kuwajibika ni IGP na timu yake wanaonekana kushindwa kazi. Aidha napenda kujua vyombo ya usalama ni kwa faida ya nani hasa? Chama, Serikali au wananchi??
 
Hiyo press release ni ya kisiasa haielezei uhalisia. It is very biased. haina jipya kwa sababu ni kelele zilezile kutoka upande mmoja.
 
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

Hivi wewe Nape na Mawaziri vihiyo mtaacha lini ujinga ulio wazi?mmeunda tume,lakini ni kama vile tume haina tena kazi ya kufanya kwa sababu tayari kwa sababu mnazozijua tayari mmewahukumu CHADEMA.Judge Ihema kama una akili ya kutosha ebu kataa uenyekiti wa Tume hii.Tume si huru tena,tayari umepewa findings hata kabla uachunguzi haujaanza.
 
Nape, hivi ni uchunguzi gani unaotaka ufanywe? Zile picha hukuziona? Wanahabari waliokuwa kwenye tukio waloptoa ushuuda jinsi mwenzao alivyo uliwa na polis hukusikia? Ala hivi yule mwanahabari aliyesema alimfuata rpc na kumueleza kuwa anayepigwa ni mwanahabari rpc akafunga vioo vya gari lake na kupiga honi mara tatu na kuondoka kisha mwangosi akaripuliwa hukusikia? Nani atabisha kuwa honi zile zilikuwa ni ishara ya rpc kwa vijana wake kuwa wammalize mwangosi? Husitoe matamko kwa kutimiza wajibu. Mimi sina kadi ya chama ila ninayo kadi ya mpiga kura ni suala la muda tu ccm mtaifuata kanu iliko
 
Wale wabakaji wa demokrasia wa kijani na njano wao katazo halikuwahusu, mbona walijazana bububu wanazindua kampeni, hamuwezi kukwepa lawama, nyinyi ni wafamaji, mtalipa damu za watu mnaowaua.

Bububu wapo chadema? Bububu kuna CUF na CCM na vyote hivyo vyama vinatawala Zanzibar, au hujui hilo?
 
Nape ni mweupe kichwani. Na sitegemei press release ya maana toka kwake!!! Siku zote alikuwa wapi hajatoa press? Alikuwa anajipanga au ni baada ya kuona kila mtanzania amekemea jambo hilo? Viongozi wa dini nao wamesimama kidete!!! Subirini!!!

Jamani nitafutieni Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Mukama, we miss him !!!!:spy:
 
well said and presented! Utaalamu wa chini kabisa wa propaganda au ni dalili za wazi za kuzidiwa na chadema.

Nape alipaswa kueleza ni kwanini mwandilshi auawe wakati yeye hakufanya vurugu na mazingira waliyomuulia hayakuwa tishio kwa polisi. Ni dalili ya uwezo mdogo wa kufikiri kukimbilia kukilaumu chama kingine. hasira za wanachi wakati huu haziko kwa Chadema bali kwa polisi. pia mfululizo wa mauaji sehemu mbalimbali nchini haukuanza na harakati za chadema pekee. ziko za wamachinga, maeneo ya madini, wafugaji n.k. yeye kwa ufinyu wa kuwaza na kuelemea upande mmoja akajitia kutoa maelezo mabovu. ni bora angekaa kimya.
 
Ccm kuvuruga maandamano ya vyama vya upinzani ndiyo kazi yenu na sasa kipaumbele chenu ni kuua kupitia hao ndugu zenu sijui mnawaita walinzi wa watu na mali zao.

Mbinu yenu hii ni chafu, wala msifikiri watanzania ni wajinga kiasi hicho ambacho nyie mnafikiria. Wananchi siku hizi tunajua kuchambua mbivu na mbichi, endeleeni lakini mwisho wenu uko mlangoni. Nawakumbusha msemo mmoja usemao,
"colonialism planted the seeds of its own destruction"
 
ubatili mtupu, ss sio wajinga, picha na video viko wazi, macho yanaona wala hatuhitaji darubini
 
Back
Top Bottom