CCM yatikisa na kufanya 'kufuru' ya kisiasa Kibanda Maiti, Mjini Unguja Zanzibar

Msihadaike na CCM Hawana wingi WOWOTE ivo ni Vikosi vya polisi na magereza pamoja na wafanya kazi wa serekali ambao walilazimishwa kutokana na MADARAKA .... Hakuna mtu anapenda CCM kiukweli Isipokua Anachuki na Ubaguzi na SIASA ZA uchochezi.....SISI tunawajua CCM zanzibar kua hawana watu bali kulazimisha VIKOSI vya serekali vihudhurie Pamoja na kupeleka gari Mashamba kuchukua watu kwa ajili ya mkutano...NDIO kunasemwa ccm zanzibar Hawawezi kupata watu ILA kwa wasio muogopa MUNGU...Nakuhakikishia CCM hawana DINI sio UISLAM SIO UKRISTO...HAWAMUOGOPI MUNGU KWA UCHU WA MADARAKA .....WAKO TAYARI WATU WAFE ILA WAO WAONGOZE NCHI

Hama Tanzania sababu hakuna Dini katika Tanzania bali watanzania ndio wenye dini na UKAWA wamekubali hilo
 
Unajua mi nashindwa kuwaelewa hawa CCM mwalim nyerere aliacha nchi moja serikal moja...sasa hiv sasa nchi mbili serikali mbil sasa sijui tumeungana vip mi hata sielewi. Zanzibar wana rais wao.wimbo wao katiba yao. Bendera yao.sasa huo muungano uko wako jamani..kama ni rais ilitakiwa awe mmoja tu..katiba moja tuu..yaan hil swala ni bonge la changa la macho
 
Watu kidogo! Ata mpiga picha alijitahidi kufanya waonekane wengi kwa kuzoom makusudi ili ionekane hawaingii wote katika kioo cha camera. Walevi watupu Bora Afe (eeh BoraAfya) na Asha bakari, walevi watupu. Apa lazima Zanzibar iwe huru laa si ivo, Kusonge maskani Seng.e inateketea milele!

Amani Karume ni mlevi, Mbunge wetu jimbo la Chake Chake Pemba Mussa Haji mlevi pia
 
Ukiangalia kwa umakini watu si wengi kihivyo.Kuna maeneo yanaonyesha uhalisia wa waliohudhuria na kuna maenea mengine kunaonyesha kama picha imepikwa .Lakini bado sijaona sababu ya CCM kuanza kufanya yale wanayoona mabaya UKAWA kuyafanya,JK alisema kila kitu kipo kwenye BUNGE sasa mbona na wao wanafanya yale yale?

Au ndiyo ile methali Mkuki kwa nguruwe na kwa binadamu ni kwinini
 
Hakuna kitu hapo. Ujinga wa watanzania wengi! Ona wamepewa fulana na kupelekwa kwa mabasi mpaka mpiga picha amejisahau akapigaa na basi lililowapeka watu kwenye mkutano. Mnamdanganya nani?
 
I support CCM!
2 zatosha, 3 za nini???
CCM moto huo uendelee nchi nzima; kila Mkoa, kila Wilaya, kila kata, kila kijiji, kila Kaya!
Lazima wakae!
 
Ukiangalia kwa umakini watu si wengi kihivyo.Kuna maeneo yanaonyesha uhalisia wa waliohudhuria na kuna maenea mengine kunaonyesha kama picha imepikwa .Lakini bado sijaona sababu ya CCM kuanza kufanya yale wanayoona mabaya UKAWA kuyafanya,JK alisema kila kitu kipo kwenye BUNGE sasa mbona na wao wanafanya yale yale?

Au ndiyo ile methali Mkuki kwa nguruwe na kwa binadamu ni kwinini

Acha kujitoa ufahamu mkuu! Hivi mlidhani watu hawaipendi CCM kama mnavyodanganywa hapa jf? CCM bado inanguvu sana mkuu;
 
Huwa najiuliza kwa nini mikutano ya ccm wahudhuriaji wote wana sare.

NIKAPATA JIBU KUWA HUFUATILIWA MAJUMBANI
 
Acha kujitoa ufahamu mkuu! Hivi mlidhani watu hawaipendi CCM kama mnavyodanganywa hapa jf? CCM bado inanguvu sana mkuu;

Wewe wasema.Nimesemea juu ya picha sijasemea uhalali wa kuipenda au kutoipenda CCM.

CCM kama CCM kama sera na Katiba yake ingefuatwa kikamilifu na viongozi tuliwapa dhamana ya kuiongoza nchi yetu sidhani kama kungekuwa na sababu ya kuwa na vyama vingi vya siasa.Lakini sababu ya uchu wa madaraka.kujilimbikiza mali,kuhujumu uchumi wa taifa na mengineyo ndiyo maana leo tumekuja na vyama vingi.

Kama CCM itaweza kwa nguvu zote kupigania kile Mwalimu Nyerere alichokipigania nadhani mnaweza kurudisha watanzania wengi zaidi.

Vinginevyo mkiendelea na kujidanganya,mkawakumbatia wala rushwa,mafisadi,wauza madawa ya kulevya,mh!nadhani itafika mahali mtaisoma number ya gari ambalo mtapishana nalo hivi karibuni.

Hilo hilo mnalodhani linaendelea kuwabeba kuna mahali litawashusha na kuwachukua wengine!Hatuwezi kuwa wajinga daima itafika mahali elimu ndogo tuliyonayo itatuletea UHURU wa mawazo,fikra na uchumi.Na mind you hizo hizo CLIP za Mwalimu Nyerere mnazotumia kuwarubuni watanzania ndiyo hizo hizo zitakazowaacha nyuma.Sababu wengi wanaelimika na kuzifanyia kazi ya ziada kwa kuzipembua na kuzitafakari.
 
mimi nilidhani ulikuwa mkutano wa wananchi kumbe ilikuw ani mkutano wa ccm, kwa hiyo hakuna jipya, walihutbiana wenyewe kwa wenyewe
 
Kwani kwa mfano huo, gharama za serikali ya muungano kwasasa anazilipa nani na je kuna unafuu kwa anayezilipa?

Kuna malalamiko ya Tanganyika kuvaa koti la muungano, hayo nayo unasemaje? Utayaondoaje kwa serikali 2.

Mbona umekimbia kulee na sasa unaleta hoja zile zile ulizokimbia.

Haya mambo ya kudanganya watu tuwaachie akina Mwigulu na Nape. Hebu tuvae sura za uhalisia.


Mchambuzi Kobello Kichuguu Bongolander Tuko
Hivi kulee ni nani aliyekimbia?
Mimi bado nasubiri documents mnirushie angalau link ....
Pia nasubiri, UZI wa gharama za muungano wa S# kama mlivyoahidi, natumai nitauchangia vizuri.
 
Back
Top Bottom