CCM yatikisa na kufanya 'kufuru' ya kisiasa Kibanda Maiti, Mjini Unguja Zanzibar

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Sehemu ya hotuba ya Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara Kibanda Maiti, Mjini Unguja, Zanzibar.
[video=youtube_share;uGBa5ABntsY]http://youtu.be/uGBa5ABntsY[/video]

7.jpg

2.jpg

67.jpg

31.jpg

41.jpg

42.jpg

52.jpg

Sehemu ya Wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Unguja.
1.jpg

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini,Ndg. Boraafya Silima wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
63.jpg

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti, Mjini Unguja Zanzibar.
69.jpg

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwasalimia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi.
64.jpg

66.jpg

Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Aman Karume, Mama Fatma Karume akiongea kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka Wazanzibar kuacha kabisa kuuchezea Muungano kwa kuwafata watu wanaoupotosha na baada ya hotuba, alipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
4.jpg

Katibu wa NEC, Oganaizeshe CCM, Dkt. Mohamed Seif Khatibu akiwahutubia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti, Mjini Unguja Zanzibar.
59.jpg

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi wa Unguja kuhusu umoja ulioanzishwa wa baadhi ya vyama siasa na malengo ya umoja huo.
50.jpg

Mh. Stephen Wassira akiwasalimia wananchi na kusema maneno mawili kuhusu msimamo wa CCM katika ujenzi wa taifa endelevu.
60.jpg

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini,Ndg. Boraafya Silima akiwasabahi wananchi wa Unguja.
30.jpg

Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Mh. Said Mkumba nae hakubaki nyuma kuzungumza na wananchi wa Unguja.
8.jpg

Mbunge wa Jimbo la Mtera, Mh. Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akizungumza kwa kusisitiza kuhusu baadhi ya wanasiasa wanaowatukana waasisi wa Muungano wa Tanzania.
23.jpg

Makamu Mwenyekiti UWT, Bi. Asha Bakari Makame akiwahutubia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi.
45.jpg

44.jpg

Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubiwa wananchi wa Zanzibar na kuwauliza wanataka serikali ngapi huku akinyosha vidole kuonyesha serikali mbili ambapo pia amewataka Wazanzibari kutohadaishwa na UKAWA kuhusu swala la muundo wa Serikali katika mchakato wa Katiba.
47.jpg

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mh. Emmanuel Nchimbi akinukuu sehemu ya maandishi yaliopo kwenye kitabu cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
20.jpg

3.jpg

34.jpg

38.jpg

39.jpg

62.jpg

33.jpg

2.JPG
 
Mwl. Nyerere katika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania alipata nafasi ya kuelezea kwa ufasaha kwa nini Waasisi wa Muungano wetu walichagua Serikali Mbili badala ya Serikali tatu.

Mwl. Nyerere alisema,
Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000). Muungano wa Serikali Moja ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tutuhumiwe hata kwa makosa, kwamba tunaanzisha ubeberu mpya!. Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja.

Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali yake ya watu 12, 000, 000 na pia ndiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la watu 12,300,000.

Ni Watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo ingekuwa ndogo. Gharama ya Serikali ya Tanganyika isingekuwa ndogo, (waulizeni Wazanzibari), na wala ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo. Hata bila ya gharama za mambo yasiyo ya Shirikisho. Na gharama zote hizo kwa kweli zingebebwa na Tanganyika.

Kwa hivyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo; na hasa kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? Hivi tuna hofu ya kwamba Tanganyika, bila kuwa na SerikaIi yake, itaonekana kuwa imemezwa na Zanzibar?. Hofu yetu ni kwamba tukiwa na Serikali Moja Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafute mfumo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikalli mbili zenye uzito unaolingana.

Hivyo ndivyo tulivyofanya, na hiyo ndiyo asili ya muundo wa Muungano wa serikali mbili. Badala ya kutungua mfumo uliopo kama wapumbavu, tulitazamia hali halisi yetu ilivyokuwa, na tukabuni mfumo uliotufaa zaidi.
Kwa mazingira na hali halisi nchini, hakuna angalizo linalotuonesha kama mazingira ya sasa yanahitaji serikali tatu. Hata wananchi wengi hawakuona umuhimu wowote wa kuongelea Muungano katika tume ya Rasimu ya Katiba.

Hakuna Muungano usiokuwa na changamoto, lakini vile vile historia inatuonyesha tuko juu ya changamoto za Muungano kwa sababu miaka 50 ndani ya Muungano wa serikali mbili ni zaidi ya changamoto za Muungano.

Mchakato wa Katiba kwa sasa utatupatia fursa ya kukabiliana na kuziondoa changamoto zilizopo kwa mshikamano zaidi ndani ya serikali mbili badala ya utengano zaidi kama inavyochombezwa kupitia serikali tatu.

CCM haiwezi kuwasaliti wananchi walioichagua kwa mamilioni ili iwajengee mazingira ya taifa lenye mshikamano na endelevu badala ya taifa lenye ubaguzi na utengano.

Wanaotaka kulimega na kuliangamiza taifa letu hawatafanikiwa kwa sababu wananchi kwa sasa wanawaona kwa jinsi wanavyobadilika kilaghai kama vinyonga.
 
CCM wanataka kuvunja muungano hawa. mbona wanaonyesha vidole viwili mikono tofauti? si waonyeshe vidole viwili mkono mmoja kama kweli wanataka muungano usivunjike?
 
CCM!.hapana,jonsia ya kiume iko wapo?.hizo picha zinaonyesha huo ni mkusanyiko wa kinamama.=Chama cha Mikusanyiko ya kinamama-CMK.
 
Dawa ya moto ni moto ukawa hawana hoja kabisa mbele ya ccm wanahangaika tu.
 
Mwl. Nyerere katika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania alipata nafasi ya kuelezea kwa ufasaha kwa nini Waasisi wa Muungano wetu walichagua Serikali Mbili badala ya Serikali tatu.

Mwl. Nyerere alisema,

Kwa mazingira na hali halisi nchini, hakuna angalizo linalotuonesha kama mazingira ya sasa yanahitaji serikali tatu. Hata wananchi wengi hawakuona umuhimu wowote wa kuongelea Muungano katika tume ya Rasimu ya Katiba.

Hakuna Muungano usiokuwa na changamoto, lakini vile vile historia inatuonyesha tuko juu ya changamoto za Muungano kwa sababu miaka 50 ndani ya Muungano wa serikali mbili ni zaidi ya changamoto za Muungano.

Mchakato wa Katiba kwa sasa utatupatia fursa ya kukabiliana na kuziondoa changamoto zilizopo kwa mshikamano zaidi ndani ya serikali mbili badala ya utengano zaidi kama inavyochombezwa kupitia serikali tatu.

CCM haiwezi kuwasaliti wananchi walioichagua kwa mamilioni ili iwajengee mazingira ya taifa lenye mshikamano na endelevu badala ya taifa lenye ubaguzi na utengano.

Wanaotaka kulimega na kuliangamiza taifa letu hawatafanikiwa kwa sababu wananchi kwa sasa wanawaona kwa jinsi wanavyobadilika kilaghai kama vinyonga.
Kwani kwa mfano huo, gharama za serikali ya muungano kwasasa anazilipa nani na je kuna unafuu kwa anayezilipa?

Kuna malalamiko ya Tanganyika kuvaa koti la muungano, hayo nayo unasemaje? Utayaondoaje kwa serikali 2.

Mbona umekimbia kulee na sasa unaleta hoja zile zile ulizokimbia.

Haya mambo ya kudanganya watu tuwaachie akina Mwigulu na Nape. Hebu tuvae sura za uhalisia.

Mchambuzi Kobello Kichuguu Bongolander Tuko
 
Tanganyika imevaa koti la rangi gani mbona mnaleta habari za vijiweni hapa tangu lini tanganyika ikavaa koti.
 
Amiri jeshi ni wangapi Tanzania? Mbona Rais wa Zanzibar anakagua gwalide na kupigiwa mizinga wakati kikwete anakuwa kama barozi wa nyumba kumi kumi?
 
wali maharagwe au jana mliongeza manjonjo kawapa nyama kutokana na unyeti wa jambo lenyewe
 
Hayo matapeli yakiongozwa na Kinana na mpiga debe Nape? Hayana hata akili!! Sasa yamejenga hoja gani hapo? Uchokoraa tu......

Amani Abeid Karume: Ni tatu!
 
CCM wanataka kuvunja muungano hawa. mbona wanaonyesha vidole viwili mikono tofauti? si waonyeshe vidole viwili mkono mmoja kama kweli wanataka muungano usivunjike?
Mtakuja na tafsiri za ajabu ajabu ili kufurahisha nafsi zenu lakini hamuwezi kuwatikisa wananchi mkitumia hoja za kijinga jinga ili muwalaghai katika kuifikia ahadi yenu ya kuwatenganisha wananchi ili mtawale mataifa mawili yenye utengano.

2 ZINATOSHA.
 
Back
Top Bottom