CCM Yatapatapa Pemba: Yalishutumu Jeshi La Polisi Kwa Kutowaunga Mkono.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
JESHI la Polisi kisiwani Pemba limejibu tuhuma za CCM kuwa linafanya kazi kwa kukipendelea chama cha upinzani cha CUF, ikisema kuwa inafuata misingi ya sheria.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, Zainab Khamis Shomari aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita akisema kuwa chama chake hakina imani tena na polisi wa kisiwani Pemba kwa kuwa idadi kubwa ya askari wamejiingiza katika siasa kwa kuishabikia CUF.
Alisema kutokana na polisi wengi kujiingiza kwenye ushabiki wa vyama, inakuwa vigumu kwao kufanya kazi kwa haki na kwamba suala hilo si siri tena kwa kuwa liko wazi.
Jana kwa nyakati tofauti, makamanda wa polisi wa mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba walisema taarifa ya kada huyo wa CCM ni potofu na imelenga kuchafua jina zuri la Jeshi la Polisi kisiwani Pemba ambalo alisema hivi sasa linafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na jamii.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini, Said Salum Malekano alisema Shutuma zilizotolewa na mjumbe huyo wa CCM ambaye pia katibu wa chama hicho wilaya ya Chake Chake, hazina msingi.
“Kama tunaonekana sisi ni mashabiki wa CUF kwa kuwa hatukutumia nguvu, huo ni mtazamo wake lakini sisi kama Jeshi la polisi hatutatumia nguvu mahali ambako hapastahili na badala yake tutatumia misingi ya kisheria katika kutekeleza majukumu yetu,” alisema Malekano.
Naye kamanda wa polisi wa mkoa wa Kaskazini, Yahya Rashid Bugi alisema Kazi ya jeshi lake ni kusimamia amani na utulivu na kulinda usalama wa raia na mali zao.
Bugi, ambaye mwishoni mwa wiki alitahadharisha kuwa polisi watalazimika kutumia silaha za moto kulinda usalama, jana aliwataka wanasiasa kufanya kazi zao za kisiasa na kuviacha vyombo vya dola kufanya kazi zake zake ambazo ni za kitaaluma zaidi na ambazo zinahitaji kuendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria.
Katika tuhuma zake dhidi ya polisi, katibu huyo wa CCM alisema ni ajabu kuona askari polisi wakiwa wamejaa siasa na kuacha kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Alikwenda mbali zaidi na kumtaka Mkuu wa Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema kuichukulia hali hiyo kwa umakini wa hali ya juu.
“Wananchi wa pemba imani yao imebakia kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)… sio tena kwa polisi. Huwezi kuwategemea askari ambao ni manazi wa siasa katika hali kama ya Pemba,” alisema Zainab ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005.
Shomari alitoa mfano wa wakati wa zoezi la uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu katika mkoa wa Kaskazini Pemba ambako polisi waliokuwa kazini walishindwa kuwaondoa wafuasi wa CUF waliokuwa wakijikusanya katika baadhi ya vituo vya uandikishaji lisha ya sheria kueleza kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kukaa ndani ya mita 200 ikiwa hausiki na uandikishaji.
Hata hivyo, polisi kisiwani Pemba juzi walitumia silaha za moto na maji ya kuwasha kutawanya wananchi waliokataa kuondoka karibu na vituo vya kupigia kura kama taratibu zinavyotaka kuwa wakae umbali wa mita 200 kutoka vituoni.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa kisiwani Pemba wamezipokea shutuma hizo kwa mtazamo tofauti.
Mwenyekiti wa AFP, Sudi Said Sudi alisema polisi walifanikiwa kukwepa mtego wa CUF, ambayo alidai ilipeleka kisiwani Pemba vijana wengi kujiandikisha nguvu ya dola itumike kuwatanya na kuwapa wapinzani hao hoja za kulaumu Jeshi la Polisi.
Alisema kitendo cha kutotumia nguvu kuwatanya ni busara na kwamba imedhihirisha jinsi jeshi hilo lilivyoboreshwa.
Mwenyekiti wa UDP mkoa wa Kusini, Asha Mohamed alisema hizo ni sera za CCM kutumia vyombo vya habari kuzungumza mambo ambayo hayapo kwa lengo la kuanzisha fujo kwa vile wanaelewa kuwa wao wana vyombo vya dola.

SOURCE:ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Mzoweya kubebwa haya sasa wachocheeni wauwe kama kawaida yao, tatizo laki mama Zainab Shomari ni kuwaona wapemba wenzako wakidunguliwa kwa risasi kama askari wa vietnam ndo uwone jeshi lenu la polisi linafanya kazi, tusubiri tuone mtafika wapi naona mnatapatapa.
 
Back
Top Bottom