CCM yapora uwanja wa sheih Amri Abeid-Arusha

Nitashangaa kama sitasikia uongozi wa Halmashauri (Jiji) la Arusha kuchukua hatua za kisheria na kudai fidia kwa makusanyo yote yaliyochukuliwa kimabavu na chama tawala.
MAtukio kama haya ndiyo yaliyoturudisha nyuma miaka hamsini. Halafu hawa hawa wakiambiwa ukweli eti wanawaita wapinzani makanjanja, sasa kanjanja original hapa ni nani?
Jiji la Arusha liongoze majiji mengine kusafisha uchafu na ubabe huu ulioenea nchi nzima.
Nawasifu walioandaa hii ripoti Mungu awabariki.
Ameeeeeen Ameeeeeen
 
Nanyaro hii issue ni rais sana nyie waachieni ccm waendelee kumiliki huo uwanja then kusanyeni kodi halali ya ardhi na mali lazima watakuwa wanawalipa hela nzuri maana huo uwanja upo prime area. Na ccm walivyo najua hata julipa hiyo kodi itawashinda

Usiturudishe nyuma. Uwanja ni mali ya halmashauri na mapato ya kodi za pango na ada za michezo ni makubwa kuliko land rent na property tax. Mapato hayo yanahitajika kwa huduma za jamii na siyo kwa mikutano ya chama kimoja.
 
Hizi 'chokochoko' zitasababisha msuguano kijamii kwa muda mrefu. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba zipo nchi zinafuatilia, kuchunguza na ab kuchukua hatua hata udhalimu uliofanywa wakati wa WW II!
 
Alafu watu wanafananisha arusha na mikoa yao.Najua viwanja vingi na majengo yaliyotwaliwa kwa namna hii yakirudishwa kwenye umiliki wa halali yatakuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa halmashauri, manispaa, miji na majiji.
 
Ni aibu kwa mkuu wa mkoa kugawa uwanja wa umma kwa maslahi machache ya chama chake!
Kuna wanaokebehi,hao tunawasamehe na kuwapuuza.Tutasonga mbele kuhakikisha kuwa HAKI ya watu wa Arusha inapatikana
 
Ni aibu kwa mkuu wa mkoa kugawa uwanja wa umma kwa maslahi machache ya chama chake!
Kuna wanaokebehi,hao tunawasamehe na kuwapuuza.Tutasonga mbele kuhakikisha kuwa HAKI ya watu wa Arusha inapatikana
Mkuu tunawaombea dua
 
CCM wanang'ang'ania viwanja afu kuvihudumia hawawezi ila wanataka sifa ya kuonekana wanamiliki vitega uchumi kibao visivyo vya uhalali
 
Moja kati ya mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali ya 1992 kuhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa ilitaka mali zote za umma zilizokuwa chini ya uthibiti wa CCM (katika hadhi yake ya uchama-dola) zirejeshwe serikalini. Pia Jaji Nyalali alipendekeza kufutwa kwa sheria gandamizi 40 (ikiwemo Sheria ya Magazeti ya 1976). Lengo la mapendekezo haya ilikuwa ni kuweka mazingira ya usawa ya ushindani (level playing field) kwa vyama vyote vya siasa. Jambo la kusikitisha ni kuwa serikali iliyapuuza mapendekezo haya. Mwanzoni wakati wa bunge la kwanza la vyama vingi, wabunge wapinzani wakiongozwa na Mabere Marando walililipigia sana kelele suala hili bungeni. Kwa sasa unahitajika msukumo mpya wa kudai kurejeshwa kwa mali ya umma iliyoporwa na CCM ikiwa sambamba na kudai katiba ya wananchi.
 
mzee shabani nyanda namfahamu sasa hivi ni mstaafu wa TPRI tena alikuwa mchezaji wa timu ya JUMUIYA na huyo mzee aliyeitwa kwa jina la piga bao pia na yeye ni mstaafu wa TPRI wote wawili walikuwa wachezaji wa timu ya JUMUIYA mtu mwingine anaeweza kulifahamu suala hilo vizuri ni mzee walii maana yeye umri wake ni mkubwa kuliko hao waliotajwa yeye kwa nyakati zote hizo tangu uwanja kujengwa alikuwa ndio Dactary wa uwanja na meneja wa uwanja wa kwanza alikuwa Ali Mtumwa kabla ya Mwamwaja
 
Ephata Nanyaro!

Uko sahihi kwenye kujenga hoja ya viwanja. Ni ukweli mweupe kama theluji. Viwanja vingi na majengo yote ya CCM yalijengwa kwa nguvu za Watanzania wote kwa ujumla wakati wa Chama kimoja ukiondoa majengo yaliyojengwa baada ya 1992. Ilitakiwa mali zote za Ccm zichukuliwe na Serikali ili vyama vianzishwe on a clean slate na kungekuwepo na usawa. It was and still is shear madness kwa CCM kumiliki mali zote na mtandao uliojengwa na watu wote na kufanya mali yao ambao wanachama hai hawakuzidi milioni tatu. Kuweka rekodi sawa ni Bora Ccm ikarejesha Mali za Watanzania ilizopora on birth day in 1992. Sheria ya vyama vingi ilikuwa mbovu kwani iliipatia CCM exclusivity ya kuridhi jina la zamani pamoja na Mali zake. This is the fundamental problem ambayo wanaojiita wapinzani couldn't see the larger picture in 1992 na huo ndio msingi na mtaji wa CCM. Piga ua bila ya kusahihisha haya makosa ya kihistoria I can see CCM ikitawala mpaka wafanye makosa wenyewe au wajifunge goal wenyewe which I don't see that happening in my lifetime! Yes viwanja na majengo mengi ya CCM ni mtaji mkubwa plus katiba yao ya 1977. Narudia kuondoa huu udhalimu you need education , education and education. Vijana wa sasa ambao walikuwa watoto kipindi cha miaka ya themanini na tisini ukimwambia nakupeleka CCM walikuwa wanalia . Hao ndio sasa wanatakaka kuwa viongozi they are brain washed hawajui rangi nyingine zaidi ya kijani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom