Ccm yapata mwenyekiti mpya mkoa wa Kilimanjaro

Asango

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
234
24
hatimaye jana mwenyekiti mpya wa ccm mkoa wa kilimanjaro alipatikana.mwenyekiti huyo mpya anaitwa IDDI JUMA aliyekuwa akichuana vikali na mbunge wa zamani wa TLP na baadaye kutimkia ccm na kuwa mwenyekiti wa wazazi mkoa, MH. NGAWAIYA ameshindwa katika uchaguzi huo.Ngawiya alianza kuukimbia ukumbi hata kabla ya kutangazwa kwa matokeo.hongera sana IDDI JUMA kwa ushindi huo karibu kwenye majukumu.ushauri wangu kwa ngawiya aache kutangatanga kwenye siasa
 
Hongera sana mh idd.umeaminiwa na tunategemea utawaunganisha wana kilimanjaro na utahakikisha wananchi wote hapo wanarudisha imani yao kwa ccm
 
Hongera sana mh idd.umeaminiwa na tunategemea utawaunganisha wana kilimanjaro na utahakikisha wananchi wote hapo wanarudisha imani yao kwa ccm
kilimanjaro wameungana toka enz za mababu na iman yao kwa sisiem aijawai kuwepo .jipange baab
 
Nafurahia kushindwa kwako ngawaiya, siasa za kinazi zina mwishooooooo, njaaaaaaa mbaya
 
Kweli CCM wamekata tamaa na Kilimanjaro. Katika wote hao hakuna ambae angeweza kufanya siasa za Kili. Kama Mama Nsilo kamasi lilimtoka. IDDI nadhani ataachia.... .

Naona wana CCM waliukimbia mkoa kuogopa aibu za kushindwa kwa aibu... 2015.
 
hatimaye jana mwenyekiti mpya wa ccm mkoa wa kilimanjaro alipatikana.mwenyekiti huyo mpya anaitwa IDDI JUMA aliyekuwa akichuana vikali na mbunge wa zamani wa TLP na baadaye kutimkia ccm na kuwa mwenyekiti wa wazazi mkoa, MH. NGAWAIYA ameshindwa katika uchaguzi huo.Ngawiya alianza kuukimbia ukumbi hata kabla ya kutangazwa kwa matokeo.hongera sana IDDI JUMA kwa ushindi huo karibu kwenye majukumu.ushauri wangu kwa ngawiya aache kutangatanga kwenye siasa

Ngawaia ananuka unafiki. Hawezi kufanikiwa hata afanyeje.
 
ila idd akipewa ushirikiano atafanya jambo imani ninayo juu yake kuliko angepata ngawaiya chama kinge malizikia hata sisi wachache tuliobaki.hakika sasa chama kitaimarika
 
Kurudisha imani kwa CCM Kilimanjaro ni ndoto ya mchana. Nafurahi kwa kumshikisha adabu huyo mchumia tumbo, Ngawaiya. Kwa taarifa yenu wote wanaorudi kwa magamba ni wachumia tumbo.
 
Tom Ngawaiya amepata alichokitafuta huko,sasa anakataa kusaini wakati matokeo yameshatangazwa,rufaa ataipeleka wapi?Rudi nyumbani matimila toka huko.
 
Mshindi ni IDDI JUMA! Angalia, Kilimanjaro ina Wakristo wengi, lakini wamemchagua Muislamu. Hii ndiyo Tanzania ya Nyerere bwana! Hakuna udini wala nini. Si sasa ambako Kikwete anataka Waislamu wamchague mwenzao, na Wakristo wamchague paroko mwenzao. Hongereni Kilimanjaro kwa kuthibitisha misingi imara aliyoiacha Baba wa Taifa.
 
mshindi ni iddi juma! Angalia, kilimanjaro ina wakristo wengi, lakini wamemchagua muislamu. Hii ndiyo tanzania ya nyerere bwana! Hakuna udini wala nini. Si sasa ambako kikwete anataka waislamu wamchague mwenzao, na wakristo wamchague paroko mwenzao. Hongereni kilimanjaro kwa kuthibitisha misingi imara aliyoiacha baba wa taifa.

hakuna watu wapenda maendeleo na wanaokerwa na wanafiki kama watu wa kilimanjaro.hawa watu ninawaaminia sana.deal kwao ni kupiga kazi ili kuwashawishi wakuamini..ukiwa mnafiki,mchumia tumbo,propaganda kwa sana,ni vigumu sana SANA ,kupewa kura na mtu wa mo town.ngawaia aisahau siasa ,aliteleza kitambo sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
ngawaiya amekwisha arudi kwenye jengo lake pale mazense akasimamie kodi ya pango,kilimanjaro sasa hawadanganyiki na siasa za maji taka,anasambaza taarifa chafu kwamba katibu wa ccm mkoa,steven kazidi amehongwa mil.3 ili aziwagawe kwa wajumbe,ama kweli mfa maji haachi kutapata,ngawaiya kushinei
 
Mzee kazidi hanaga hizo mambo za mlungula,anatapatapa kama sumaye tu hamna lolote
 
Back
Top Bottom