Wa Ndima
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 1,526
- 323
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa kuiagiza Chadema kuisoma na kuielewa vizuri Sheria ya Gharama za Uchaguzi na sheria nyingine za uchaguzi ili kuepuka usumbufu.
Ombi hilo ni miongoni mwa maombi matatu yaliyotolewa na CCM wakati wa kujibu malalamiko yaliyotolewa na Chadema, dhidi ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,
Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa vyombo vya habari, Chadema haijaelewa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kama
inaelewa, imeamua kufanya usumbufu usiokuwa wa lazima kumwekea pingamizi Kikwete.
Taarifa hiyo imenukuu kifungu 21 (1), wakati wa uteuzi, kampeni
za uchaguzi au uchaguzi, kitendo kinachokatazwa ni Kwa tafsiri ya asili kwa mujibu
wa taarifa hiyo, maneno ya kifungu hicho hayahusu ahadi zitakazotekelezwa
baada ya uchaguzi kwa kutumia fedha za Serikali, bali kinahusu ahadi zinazotekelezwa wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea, kampeni au wakati wa uchaguzi.
Pia kinakataza wagombea kutumia fedha binafsi kutekeleza ahadi zake. Kama sheria hiyo ingekataza kutoa ahadi zitakazotekelezwa baada ya uchaguzi, ingeua dhana nzima
ya kampeni inayovitaka vyama vya siasa na wagombea kuelezea mambo gani wanayoahidi iwapo watachaguliwa, alisema Makamba.
Makamba amesisitiza kuwa malalamiko ya Chadema hayahusu sheria hiyo kwa sababu haipingani na dhana nzima ya kampeni kama ilivyoainishwa ndani ya Sheria ya
Uchaguzi, pamoja na maadili ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.
CCM inasema inashangazwa na hatua iliyochukuliwa na Chadema kwa kuwa jambo lililofanywa na mgombea wa CCM, linafanywa pia na wagombea wa vyama vingine
akiwamo Dk. Willibrod Slaa. CCM inamshangaa Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika anayejiita raia mwema kwa kutomuwekea Dk. Slaa pingamizi kwa kutoa ahadi kemkem katika kampeni zake kama kweli anaamini kuwa kutoa ni ukiukwaji wa sheria.