CCM yamwangukia Bashe!

Jumapili iliopita Husen bashe alifanya mkutano mkubwa NZega katika uwanja wa Park, mkutano huo kwa akili ya kawaida tu haiwezekani ukawa umeandaliwa na bashe mwenyewe je ni nani yupo nyuma ya bashe maana mkutano ulikuwa mkubwa muno

Huko Nzega ndio kwetu, Mama yangu mzazi ana asili ya huko. sasa ninaposikia habari za huko napenda kutaka kujua zaidi.

Sasa ndugu yangu hebu tuwekee sawia. Je mkutano huo ulikuwa wa nini?
 
Tujikumbushe vugu vugu la uongozi wa umoja wa vijana wa CCM kuwa Bashe na wengine walikuwa kundi gani ndani ya chama. Ukweli wa zile habari zilizoonekana kama uzushi na kupuuzwa sasa ndio unaonekana tunapokaribia uchaguzi. Leta habari zaidi za mkutano halafu tujadili bila hofu. WENGINE HATUFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE
 
Hivi lini Falsafa hii ya mtu akifanya kitu tunaanza kujiuliza KATUMWA NA NANI?why tusiulize kitu kilichomsukuma kufanya jambo hilo badala ya kuwaza huyu katumwa.

Aina hiyo ya mawazo mgando ni hatari sana ktk jamii,Bashe nzega i think ni kwao,na kwanini uulize mkutano wa JPILI tu usiulize mikutano ya maeneo mengine na siku zingine.

Pumba acha
 
Nianze kwa kupokea lugha isiyo ya kistaraabu kwa ndugu yangu aliyeniambia kuwa naanza na post moja kwa majungu, labda hatukuelewana. binafsi nilikuwepo eneo la mkutano ninachouliza kwa jinsi mkutano ulivyokuwa mkubwa na watu walivyokuwa wametulia wakimsikiliza kijana bashe akielezea maneno matamu kwa watu wa nzega,na tumezoea kuona watu wakiwa wanataka madaraka hutumia lugha ambali mbnali kama vile nimetumwa na Mzee wa ikulu kugombea , nimeitwa na wazee kugombea nk, swali kwa watu wa Nzega ni kuwa bashe katumwa na nani maana hata mi binafsi nilikuwepo eneo husika kama nilivyosema na nilivutiwa sana na ujasiri wa bashe wa kumiliki jukwaa npia kwa uchambuzi wa mambo mbali mbali kitu ambacho mbunge wetu wa jimbo amekuwa akikwepa mikutano ya hadhara na mara kadhaa amekuwa akidandia kazi zifanywazo na serikali na kusema kuwa amezifanya yeye. inawezekana nyuma ya bashe yupo mungu maana watu wa nzega tumetaabika vya kutosha , umeme wa Ndalla unasua sua kwa Mbunge wa jimbo kufanya kazi za kitaifa zaidi nyingine hazitusaidii sisi wa mwaka shahara. HONGERA SANA BASHE NYUMA YAKO YUPO MUNGU!
 
Zyansiku, pole na karibu sana jamvini! nimesoma post yako moja ya kwanza ni kawa sijakuelewa kabisa ! imenilazimu nichukuwe muda kidogo kufikiria nini cha kuandika lakini muda huu nikiingia JF nimekutana na ufafanuzi wako labda nikupongeze kwa hilo, namfahamu Bashe, naifahamu Nzega, namfahamu Selelii. sipo Tabora kikazi kwa muda mrefu kidogo kwa sasa nipo Dar ila naijua vizuri Tabora na viunga vyake vyote hapa niungane na wewe jambo moja kuwa wananchi wa mkoa wa tabora wamechoka kuburuzwa wa bunge ambao wamekuwa madarakani kwa miongo kadhaa bila kuleta tija, wabunge wamekaa madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili hadi vitatu, kwa kweli wamechoka hawana jipya. ni wabunge wawili tu kwa mkoa mzima ambao wamekuwa wakitembelea majimbo yao japo mara moja kila mwezi na wamefanya mabo mengi ya maendeleo si rahisi kuwaangusha watu hao hata kama kutakuwa na shinikizo lolote, wabunge hao ni Prof kapuya wa Urambo Magharibi na Mh Rostam Aziz wa Igunga hao ni wabunge ambao tulie tucheke watarudi bungeni kama watagombea na kujaliwa uhai waliobaki wote! wamechoka hawana jipya , japo mB wa tabora mjini Mh kaboyonga anaonekana kufaa sana kwa siasa za kitaifa ila jimboni hali ni mbaya sana
 
Katumwa na RA. Don la mafisadi.

Hakuna Mbunge wa maisha, miaka 5 ikiisha kila mtu anayetimiza masharti ana haki ya kugombea Ubunge. Hivyo ni kukosa hekima kuona kila anayetaka kugombea katumwa, kwani hao Wabunge nao walitumwa na nani?. Zaidi inatia shaka na aibu ukifikia sema eti katumwa na RA.
 
Hamna cha shaka au aibu. Katumwa na RA, the Don of Mafisadi.
 
hamna cha shaka au aibu. Katumwa na ra, the don of mafisadi.

bashe kashakuwa rais wa wanafunzi mzumbe chuo kikuu,jee alitumwa na rostam?

Toka sekondari nzega hadi a level dar-es-salaam amekuwa kiongozi wa wanafunzi all the way up to university.
Uongozi uko kwenye damu yake.ukimpa jukwaa ni sawa na obama.
 
Nianze kwa kupokea lugha isiyo ya kistaraabu kwa ndugu yangu aliyeniambia kuwa naanza na post moja kwa majungu, labda hatukuelewana. binafsi nilikuwepo eneo la mkutano ninachouliza kwa jinsi mkutano ulivyokuwa mkubwa na watu walivyokuwa wametulia wakimsikiliza kijana bashe akielezea maneno matamu kwa watu wa nzega,na tumezoea kuona watu wakiwa wanataka madaraka hutumia lugha ambali mbnali kama vile nimetumwa na Mzee wa ikulu kugombea , nimeitwa na wazee kugombea nk, swali kwa watu wa Nzega ni kuwa bashe katumwa na nani maana hata mi binafsi nilikuwepo eneo husika kama nilivyosema na nilivutiwa sana na ujasiri wa bashe wa kumiliki jukwaa npia kwa uchambuzi wa mambo mbali mbali kitu ambacho mbunge wetu wa jimbo amekuwa akikwepa mikutano ya hadhara na mara kadhaa amekuwa akidandia kazi zifanywazo na serikali na kusema kuwa amezifanya yeye. inawezekana nyuma ya bashe yupo mungu maana watu wa nzega tumetaabika vya kutosha , umeme wa Ndalla unasua sua kwa Mbunge wa jimbo kufanya kazi za kitaifa zaidi nyingine hazitusaidii sisi wa mwaka shahara. HONGERA SANA BASHE NYUMA YAKO YUPO MUNGU!

Ahali yangu,

Mi bado nina shauku sana kujua Bw Bashe aliongea mambo gani hayo matamu kwa ahali zangu wa Nzega?

naomba kwa ihsani yako tupe japo kiduchu.
 
Katika kile ambacho hadi sasa sijakipatia majibu ni pale nilipo mshuhudia Hussen Bashe muda kati ya saa 10-11 jioni akiwa katika ofisi za IPP na baadae alionekana aki ongea kwa muda mrefu sana na Mhariri wa Nipashe Je si hatari hiyo? mahusiano ya Bashe na IPP yameanza lini?
 
Hey ! Mbongo what the issue? kwani Husen hawezi kuwa na rafiki zake pale binafsi sioni kama kuna tatizo un less uje na hoja kamili
 
Ni sahihi, tusimuhukumu mtu kwavile ameonekana katika majengo ya IPP Media, either tulitegemea issue fulani au tusubiri kama kuna habari itakuja mbeleni.
 
what if his wife working there? unamfuatilia mpaka nyumbani kwake? majirani zake akina nani? vipi kuhusu schoolmate zake unawajua?

kuwakwepa mafisadi kazi sana ni majirani, wanaiba still wanakuja kuomba chumvi kwako!

ndio maana Yesu akasema yaache magugu yakue na ngano!
 
Ona sasa.....huyu mbongo kaleta hii mambo ya kimbea na udaku kabisa hapa.....no one anamwita Mmbea...but bro Yo Yo kuanzisha thread ya vyuo feki kawekewa na thread kabisa......! double standard au hatuoni?
 
Mh! Jamvi hili kweli ni kubwa linabeba kila aina ya viumbe.

Sasa mtu kuonekana IPP ni ajabu?, itafikia wakati sasa hata watu wasifanye biashara zao?. Nani hajui IPP ni chombo cha habari ambacho kipo open kwa watu wote?. Hebu kama hatuna thread za kuanzisha tuchangie thread zenye kujenga zipo nyingi tu humu, issue si kuwa na statitics ya threads bali kujadili mambo muhimu. Mtakimbiza vichwa muhimu sasa kama mnakuja na udaku humu.
 
Who is this person kwanza kabla ya yote???

Kwani kama ni fisadi - Naungana na mtoa hoja Mafisadi lazima tuwajue hata private issues zao. Lazima tufuatilie kila aina ya life yao kwa kuwa wameihujumu nchi yetu. So Mbongo akituambia who is that in this goble then tutaendelea kumfuatilia kwa karibu kama tunavyowafuatilia mafisadi wengine.

Vita ni vita Mura! Kama tumeamua vita ya ufisadi then tusiangalia tunapiganage cha msingi ni kumkabili adui.
 
Back
Top Bottom