Nnauye,
Ningependa nikurudishe nyuma kidogo,kwanza kabisa mimi sijui hizi kaiba za vyama ikiwemo ya ccm/umoja wa vijana.
Sasa nilitaka kujua hili la uchaguzi wa vijana,je kuna kalenda ambayo inaongoza hizi chaguzi au kuna utaratibu gani uliokuwepo ambao unaongoza hizi chaguzi.
Nina uliza hivi kwa sababu wewe binafsi swala la umri lilikuwa ajenda ktk kugombea moja ya nafasi ktk chama.
je kigezo cha umri kiaangaliwa siku ambayo uchaguzi utafanyika au siku ambayo fomu zinatolewa,hii ina maana hata kama uchaguzi utaahirishwa au kusogezwa mbele hauta hathiri umri wa mgombea.
Katibu Tarafa nashukuru kwa swali zuri.
CCM kama vyama vingine vya siasa kwa nchi yetu lazima viwe na katiba, hivyo CCM inatumia Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2007. Sasa ndani ya Katiba ya CCM kuna Jumuiya za Chama, ambazo ni VIJANA, UWT NA WAZAZI,sheria ya nchi hairuhusu Taasisi moja kuwa na Katiba mbili, hivyo hizi Jumuiya zinakuwa na KANUNI ukiacha UWT ambao wanakatiba...lakini kimakosa... jumuiya zingine zinaongozwa na KANUNI bila kuathiri Katiba ya Chama na nchi...
Swala la uchaguzi ni moja ya mambo yanayoelezwa kwenye kanuni za UVCCM. Sasa swala la umri limeanza siku nyingi kujadili umri wa kijana ni upi hasa, mpaka ilipoamuliwa kuwa sifa kubwa ya mwanachama wa UVCCM ni umri nao ni miaka13-35,kama ilivyo sifa ya mwanachama wa UWT ni jinsia yaani MWANAMKE.
Ni mimi nilyeanzisha mchakato huu mwaka 2003 wa kutaka tafsiri sahihi ya uanachama wa mwananchama wa UVCCM, HOJA ILIKUWA KAMA SIFA MOJA WAPO NI UMRI YAANI 13-35 UKIMRUHUSU MWANACHAMA WA MIAKA 32 KWA MFANO ACHAGULIWE KUWA KIONGOZI BAADA YA MIAKA 3 UANACHAMA WAKE UNAKOMA NA HIVYO ANAPOTEZA SIFA YA KUWA KIONGOZI KWANI SI MWANACHAMA.HIVYO LIKATOLEWA PENDEKEZO KUWA KILA ANAYEGOMBEA ASIWE AMEZIDI MIAKA 30 ILI ANAPOMALIZA AWE NDANI YA UMRI WA UANACHAMA WA UVCCM.
Mfano Nchimbi anatuongoza vijana akiwa si mwanachama wetu toka mwaka 2006, ni kinyume na sheria,mtu akienda mahakamani ni mgogoro mkubwa kwa taasisi.
-LILIPOKUJA SWALA LANGU-MIMI NIMEZALIWA TAREHE 07/11/1977,HIVYO MPAKA TAREHE 06/11/2008 MIMI NILIKUWA NA MIAKA 30 NA MIEZI KADHAA, NA KWAKUWA UCHAGUZI NI MCHAKATO/ PROCESS UNAANZA PALE UNAPOCHUKUA FOMU MPAKA SIKU UNAPOPIGIWA KURA NDIO MWISHO WA MCHAKATO. SASA NIMECHUKUA FOMU TAREHE 15/07/2008 NIKIWA NA MIAKA 30 NA MIEZI NA KWAKUWA UTARATIBU HUWA HATUHESABU MIEZI HIVYO KWA MUJIBU WA KANUNI UCHAGUZI UMEANZA MIE NIKIWA BADO NIMO NDANI YA KANUNI..
....na ndo maana baada ya kuona hoja ya umri haiuziki wakaja na hoja kunivua uanachama!! Kusema kweli ni kuigeuza siasa mchezo mchafu wakati haikupaswa kuwa hivyo...na wanajua nguvu waliyotumia kufika hapo walipo fikia.....
Nnauye Jr