Kweli iondolewe.invissible pls ondoa huu utoto
Kweli iondolewe.invissible pls ondoa huu utoto
Katika kile ambacho hadi sasa sijakipatia majibu ni pale nilipo mshuhudia Hussen Bashe muda kati ya saa 10-11 jioni akiwa katika ofisi za IPP na baadae alionekana aki ongea kwa muda mrefu sana na Mhariri wa Nipashe Je si hatari hiyo? mahusiano ya Bashe na IPP yameanza lini?
Katika kile ambacho hadi sasa sijakipatia majibu ni pale nilipo mshuhudia Hussen Bashe muda kati ya saa 10-11 jioni akiwa katika ofisi za IPP na baadae alionekana aki ongea kwa muda mrefu sana na Mhariri wa Nipashe Je si hatari hiyo? mahusiano ya Bashe na IPP yameanza lini?
Jamani haina maana sana kusema eti watu watoke CCM kwa kuwa wamepingana na maamuzi au na utaratibu wa jinsi mambo yanavyoenda humo. Watu wenye Busara waliwahi kusema kuwa "Endapo yai litapasuka kwa kuanzia ndani, basi kiumbe huwa kimepata uhai, lakini kwa nje matokeo huweza kuwa tofauti, kwamba kiumbe kimepoteza uhai"...yaani yai hilo limevunjwa na nguvu zilizopo nje"
Wengine, kama Nape (I presume) pengine wanapenda kuleta mabadiliko kutokea ndani ya mfumo, wakati wengine kama Zitto wanaamini katika kubadili mambo kutoka nje! Mfumo uliopo unaweza kuwa na matatizo kidogo ambayo wapiganaji wanaamini katika kuyarekebisha na kuufanya uwe bora zaidi!
Naomba kuwasilisha,
Dk. Hamisi Kigwangalla.
Naiheshimu sana forum hii kwani inasaidia kutoa mambo ambyo wakati mwingine hayasemwi na vyombo vingine.Nawashukuru kwa kunikaribisha, napokea kwa heshima kubwa karibu yenu wakubwa, naahidi ushirikiano mkubwa kwa kadri ya uwezo wangu wote.
SASA MAMBO MUHIMU TULIYOONGEA KATIKA KIPINDI CHA MLANGO WA DHARURA NI;
1). Niliunga mkono uteuzi wa wagombea kutoka Zanzibar kugombea Uenyekiti UVCCM. Baadhi ya sababu ni kuwa haya ni maamuzi ya kikao halali cha chama NEC, kwa kuzingatia kuwa hakuna uteuzi ambao usingekuwa na mapungufu, hata huu ninaouunga mkono una mapungufu yake mengi tu, lakini ukilinganisha na uteuzi mwingine kwa MTAZAMO WANGU huu ulikuwa nafuu kuliko mingine. Lakini nilikumbusha kuwa mwaka 2003 niligombea mimi uenyekiti uvccm na kulikuwa na wagombea toka znz ambao hawakurudishwa hivyo sioni sababu ya bara kulalamika leo.
2).Utendaji wa Makamba, nilichosema ni kuwa si dhambi kujadili utendaji wa Makamba kama katibu mkuu wa CCM, tena hata wanachama wa kawaida wana nwajibu wa kujadili hali ya chama chao, KWANI NAAMINI HICHI NI CHAMA CHA WANA CHAMA NA SI VIONGOZI. N a nikaongeza kuwa kikao chenye mamlaka ya kumwajibisha Katibu mkuu wa ccm ni NEC huu ndio utaratibu, hivyo hata baada ya kujadili mwisho lazima malalamiko yaletwe NEC ndo wanaweza kumwajibisha Katibu Mkuu.
3). Nikasema KUGOMBEA URAIS 2010 SI DHAMBI ni huru kwa mwana chama yeyote kwa mujibu wa katiba ya CCM ambayo ndio sheria mama, kwani hata ilani ya uchaguzi inatengenezwa mpya, hivyo sitashangaa kuona watu wanachukua fomu kuomba uteuzi, ndio demokrasia.
4). Nikasema pia si kweli kwamba wanaokosa wanakumbatiwa, inawezekana kwa upande mmoja lakini sio katioka kesi zote, nikatoa mfano wa waliowajibishwa kwa makosa ya Richmond, nikasema hawa walisaliti chama kwani tuliwatuma kutekeleza ilani ya chama wao wakaenda kutekeleza yao.
5.) Nikajibu swala la kufukuzwa uana chama uvccm, nikasema MWENYE AKILI NAJUA NANI MKWELI NANI MWONGO kwani UJENZI MPAKA SASA UNAENDELEA BILA MKATABA, MAPUNGUFU NILIYOYAELEZA NDIYO YALIYOUNDIWA TUME KUREKEBISHWA, SASA MWONGO NA MKWELI IKO WAZI, lakini najua mtu mzima kukiri kosa ni ngumu...maji marefu hapa kwa mzee wangu....
HAKIKA HATUKUMTAJA KABISA HUSSEIN BASHE KATIKA MAZUNGUMZO YOTE, SI MIMI, WALA OMARY KIMBAO AU JERRY SILAA NA HATA MTANGAZAJI KIBONDE, NIMESIKITISHWA NA TAARIFA HIZI KUZIKUTA HUKU, GAZETI LA TANZANIA DAIMA WALICHAPA PIA LAKINI KIMAKOSA, SIKUKANUSHA KULE COZ INGEATHIRI UCHAGUZI KWA UPANDE MMOJA NA HASA MGOMBEA MMOJA.
Namwomba ndugu yangu asituharibie heshima ya forum hii, naamini nimeeleza kwa kifupi yaliyotokea.
Nnauye Jr
Inasikitisha sana kuona CCM ya JK vyeo vyote sasa ni vya kujuana tu na wala sio uwezo wa mtu.
CCM ya Nyerere ilitafuta viongozi kutokana na uwezo wao hata kama hawakuwa na majina makubwa. Lakini leo hii ukiangalia mtu mzembe kama Rishard Bade ndio anayesukumwa (probably na EL, RA, Kinana) ili kukiongoza chama kikuu TZ.
Hii ni hatari. Tunakoelekea ni kubaya sana kama mabadiliko nchini au angalau ndani ya CCM hayatakuja mapema.
Nape Jr: Sipendi kuchangia sana kwenye hoja hizi mnazolumbana hapa, maana nyingi zinahusu chama chenu, lakini nilitaka kusema kwamba you are incredibly convincing in your argument na inaonekana kumbe hata huko kwenye UVCCM kuna watu wanafikiri!!!
Maana wakati mwingine huwa tukisoma mawazo ya viongozi wenu tunasikitika sana, lakini kupitia thread hii umenitia moyo. Wakati mwingine watu mnaowaweka mbele kuwasemea wanawaaibisha na kuonekana kama vile katika UVCCM wote hamnazo!! Nakumbuka niliangalia mdahalo mmoja kati ya kiongozi wenu wa UVCCM (naomba nisimtaje jina) na Mnyika wa BAVICHA, ilikuwa aibu-ni kama vile Mnyika alikuwa anapambana na mtoto aliyetoka kufanya mtihani wa darasa la nne!
Great man, you certainly have a great future in Tanzanian politics. My only worry is that you may be in a place where you're slowly but surely eroding your potential instead of realising it-good if you realised this sooner than later-I may be wrong though! Read my article: CCM ya Nape ni nadharia...http://www.chadema.net/makala/mkumbo/kitila_18.html