sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 133
[h=2][/h] Jumatano, Agosti 22, 2012 06:03 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepuuza tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alimtaka Dk. Slaa kuacha siasa, kwani hivi sasa anazeeka vibaya.
Kauli hiyo ya CCM imekuja siku moja baada ya Dk Slaa kuibua madai mazito dhidi ya CCM, akikituhumu chama hicho kuwa kimeingiza silaha, zikiwamo bunduki bila vibali wala kuzikatia leseni, kwa lengo la kutaka kukihujumu.
Nape alivitaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi juu ya madai hayo, kwa kuanza kumhoji Dk. Slaa kama shahidi namba moja juu ya uingizwaji wa silaha hizo.
"Kwa alivyo Dk. Slaa hivi sasa, huenda mzee huyo nazeeka vibaya na huenda ana tatizo, hivyo tunaviomba vyombo vya usalama vifanye kazi ya kumhoji.
"Dk Slaa amekuwa akitoa tuhuma nzito eti CCM tunanunua silaha kwa ajili ya kuwapa vijana wetu waliopo kwenye makambi yetu, si kweli, hakuna kambi hata moja ya vijana ila tunaona sasa Dk. Slaa, ameamua kutunga uongo.
"Mwaka 2010, wakati wa kampeni Dk. Slaa, alizua uongo na kusema kuwa kuna kontena limebeba masanduku ya kura kinyemela, nasi CCM tulimsamehe kutokana alikuwa na kihoro cha kushindwa.
Nape alitumia nafasi hiyo kumshauri Dk. Slaa afanye kazi nyingine iwapo ameshindwa kufanya siasa na akishindwa kabisa basi anaweza hata kuchukua jukumu la kulea familia yake.
MTANZANI ilimtafuta msemaji wa Jeshi la Polisi ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo, huku msemaji wake, Advera Senso, akiahidi kulifuatilia jambo hilo kwa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro.