CCM wamtaka Amaan Karume na wenzake kurejesha kadi

wanatania tu hawa..nani arudishe kadi? karume ni powerful kuliko jk amd bu the way kati ya jk na karume nani anapaswa kurudisha kadi kwani?
 
Mengi yatajitokeza kipindi hiki tusubiri tu. Mungu ibariki Tanzania yetu na walaaniwe wabinafsi.
 
Mtu huwezi kulazimishwa kurudisha kadi au kununua kadi ya chama fulani,mbona wanaoenda kwenye vyama vingine vya upinzani huenda na kadi walizochukua upande mmoja na kuzipeleka upande mwingine?.
Wale wanaopewa kadi zile siyo zao ila zinatumika kama ushahidi/kieelezo kwa kampeni wanazofanya na jinsi walivyokubalika.
Ileweke kadi ya chama pia ni mali ya mwenye kadi iwe umenunua/nunuliwa.Acha uongo hizo ni janja za wanauamsho
Kweli kabisa... kama wana ubavu wawanyang'anye hizo kadi na si kuwataka warudishe
 
"kama ningekuwa na uwezo ningevididimiza visiwa vya Zanzibar katika bahari ya Hindi" (Nyerere). wazanzibari waligawanyika wakaingizwa katika jinamizi la muungano.Nyerere hakua na nia njema na muungano huu lakini karume alidanganywa akadanganyika matokeo yake ndio haya tunaendelea kuangamia wazanzibari. Tumejenga ya pamoja lakini sisi tumewekwa bomani, tena tumekomelewa tusifurukute, wenzetu wanatanua ndani na nje. Jeshi lao, mambo ya nje yao, uchumi (kodi, biashara, sarafu, benki kuu, fedha za kigeni nk) ni yao, hatufurukuti wazanzibari. Wazanzibari tuligawanywa tukawa tunahofiana wenyewe kwa wenyewe na upande wa pili ukapata mwanya mzuri. Sasa tumeungana kurudisha Zanzibar yetu. kama hawajui waliosikia tumefanya serikali ya umoja wa kitaifa lengo hasa lilikuwa kapuni kurejesha zanzibar yetu kwani tumeshaondoa hofu kati yetu. Na kama hofu hawaijui ni kwamba CCM zanzibar walidhani CUF hawayatambui mapinduzi ya 1964 na hivyo hwenda wakichukua madaraka watafuta historia na misingi ya mapinduzi ya 1964. Kumbe hawajui CUF ina wanamapinduzi kibao. wanathamini mapinduzi ya 1964 wanayaenzi. Sasa nchi yetu hakuna wa kuizuia. Tatizo bara hawafuatilii siasa za Zanzibar. Muungano wa MKATABA sasa ni msimamo wa SMZ Amani Karume (CCM), Mansour Yssuf Himid (Waziri CCM), Hamza (Mwakilishi CCM), Mshimba (mwakilishi CCM), Raza (mwakilishi CCM), Asha bakari (mwakilishi CCM), Mwanasheria mkuu na wengine wameanza tu wengine watafuatia na mwisho msimamo wa SMZ utakua wazi. Hatutaki tena muungano unawafanya watanganyika kuwa ndio wenye muungano wazanzibari ni watumwa wa muungano.

Mzanzibari usiseme 1, 2 wala 3 sema MKATABA tuuuu.
Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
 
Back
Top Bottom