CCM wamtaka Amaan Karume na wenzake kurejesha kadi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
ccm%2Bkampeni%2Buzini%2B3.JPG

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Vuai Ali Vuai.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemtaka makamo mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Amani Abeid Karume na baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kurejesha kadi za chama hicho kutokana na kwenda kinyume na maadili ya chamana kutangaza sera zisizo za chama hicho.


Kauli hiyo imekuja kufuatia azimio la wajumbe wa chama hicho wa mkoa wa mjini magharibi waliokutana juzi mjini hapa na kuwashirikisha wanachama wapatao 400 ikiwemo wajumbe wa Halmadhauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Azimio hilo ambalo limesomwa mbele ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo limesema kwamba Mansoor akiwa na majukumu makubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na chama cha Mapinduzi CCM kama mjumbe wa NEC amekuwa akitamka kutaka Muungano wa mkataba hali ya kuwa akijua hiyo sio sera ya CCM.

Azimio hilo pia limesema kwamba Himid amekuwa akisema waziwazi kukataa muungano uliopo pamoja na kuwashawishi wananchi na wanachama wa CCM kuunga mkono suala hilo.

Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walifurahia baada ya kutolewa uamuzi huo kuonesha wanaunga mkono uamuzi huo wa kumtaka waziri Himid kurudisha kadi ya chama cha Mapinduzi.

"Tunaunga mkono maamuzi yalitolewa na viongozi wetu wa chama kwa sababu huyu muweka hazina wetu hivi sasa amebadilika sana" alisema mwanachama kiongozi mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini na kuongeza kwamba.

"Siku hizi wawakilishi wetu wamekuwa wakicharukwa sana kule barazani kwa hivyo azimio la leo litawafanya wengine warudi nyuma katika misimamo yao kwa sababu wote wanaokwenda kinyume na sera za chama tutawataka warejeshe kadi zetu" alisisitiza.
Katika vikao vya Baraza la Wawakilishi vinavyoendelea katika michango ya bajeti ya Wizara ya nchi ofisi ya rais Fedha mipango na Uchumi pamoja na wizara ya Katiba na Sheria, Himid alitamka bayana kuwepo kwa Muungano wa mkataba ambao utaiwezesha Zanzibar kuwa na dola kamili inayojitegemea na kuwa na kiti katika umoja wa mataifa.
Kikao hicho kilichowajumuisha mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Yussuf Mohammed na mwenyekiti wa wilaya Borafya Silima wakiwemo na wajumbe wengine wakiwemo wenye viti wajumbe wa halmashauri kuu aliwemo Waziri Machano Othman Said, Burhani Saadat na wengineo.

Himid alisema Zanzibar inahitaji kuwa na aina ya Muungano utakayoifanya kuwa dola kamili inayojitegemea,hatua ambayo itasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Aidha kumekuwepo vipeperushi vinayoshabihishwa na CCM, ambapo Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Vuai Ali Vuai alisema kusema vipeperushi vinavyosambazwa katika kisiwa cha Unguja na Pemba havina uhusiano na chama cha Mapinduzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kuu Kisiwandui,Vuai alifafanua na kusema inasikitisha sana kwamba baadhi ya watu wasiojulikana wamechapisha vipeperushi mbali mbali ambavyo vinasambazwa katika mitaa mbali mbali vikiwa na sura ya chama cha Mapinduzi pamoja na kumuhusisha rais wa Zanzibar dk.Ali Mohd Sheni.

'Napenda kuwajulisha wanachama na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi kwamba vipeperushi vinavyosambazwa mitaani havina uhusiano na chama cha Mapinduzi Zanzibar licha ya kuwahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama na Serikali'alisema Vuai.

Vuai alisikitishwa sana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukaa kimya huku jina la rais wa Zanzibar dk.Ali Mohd Sheni likitumiwa vibaya na kumuhusisha katika vipeperusdhi vinavyokwenda kinyume na sera ambayo yeye ndiyo iliyomuweka madarakani.

'Nasikitishwa sana na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekaa kimya wakati jina na picha ya rais wa Zanzibar ikitumiwa vibaya katika vipeperushi vinavyomuhusisha muundo wa Serikali ya Muungano wa mkataba'alisema Vuai.

Watu wasiojulikana wamekuwa wakisambaza vipeperushi vya aina mbali mbali vikiwataka wananchi wa Zanzibar kuchaguwa muundo wa Serikali ya umoja wa kitaifa huku vipeperushi hivyo vikiwa na picha za viongozi wakuu wa Serikali akiwemo rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohd Sheni.

Baadhi ya vipeperushi hivyo vimewataka wananchi wa Zanzibar kuachiwa kupumuwa,vikimaanisha kuachiwa kuwa huru katika Muungano,huku vyengine vikiwashawishi wananchi wa Zanzibar kuchaguwa muundo wa Muungano wa mkataba ambao ndiyo utakaoleta maslahi ya wananchi wa Zanzibar.

Vipeperushi hivyo vimekuwa vikisambazwa katika maeneo yote ya Unguja na Pemba pamoja na vijijini huku vikiwa vimechapishwa kwa teknolojia ya rangi vikiwa na picha za viongozi wakuu wa serikali.

Vuai alisisitiza na kusema chama cha mapinduzi sera yake ni muungano wa serikali mbili ambao unakidhi mahitaji isipokuwa unakubaliana na kuwepo kwa marekebisho ikiwemo Zanzibar kupata fursa zaidi za kiuchumi zitakazoleta tija na maendeleo kwa wananchi wake.

 
Amani Abeid Karume yupo kwenye heading, lakini habari yenyewe haimtaji na wala haisemi tuhuma zake ni zipi.
From which source anyway?
 
Mkuu nashangaa wewe kutoa hizo habari wakati tunajua we ni uamsho damu damu.
Sasa unafurahia au unasikitika?
Kila mtu anajua kwa hivi sasa Karume is a political liability as far as muungano is concerned.
 
Mtu huwezi kulazimishwa kurudisha kadi au kununua kadi ya chama fulani,mbona wanaoenda kwenye vyama vingine vya upinzani huenda na kadi walizochukua upande mmoja na kuzipeleka upande mwingine?.
Wale wanaopewa kadi zile siyo zao ila zinatumika kama ushahidi/kieelezo kwa kampeni wanazofanya na jinsi walivyokubalika.
Ileweke kadi ya chama pia ni mali ya mwenye kadi iwe umenunua/nunuliwa.Acha uongo hizo ni janja za wanauamsho
 
The tide of history cannot be resisted. Like Karume, Mansoor will you stand on right side of history or like Vuai on the wrong side of history? Nafurahia umoja na undugu wetu!
 
Kwani Amani Abeid Karume bado ni makamu mwenyekiti wa CCM? Si huwa urais ukikoma huwa wanang'atuka kwenye vyeo vya uenyekiti na umakamu uenyeketi, au Karume aliamua kutofuata utamaduni wao?
 
Jamani hata Karume!? anyway; wahenga walisema panapofuka moshi panaficha moto! only time will tell kuhusu mwelekeo wa Tanzania in the foreseable future.​
 
Mbwa kala mbwa hiyo......wapi M4C.............Meli hiyooooooo:flypig:
 
Jamani hata Karume!? anyway; wahenga walisema panapofuka moshi panaficha moto! only time will tell kuhusu mwelekeo wa Tanzania in the foreseable future.

Hata mama wa taifa wa pili ameutilia shaka muungano.
 
nadhani kilichowazi miongoni mwa wengi bara na zanzibar ni kuwa kwa aina ya serikali tuliyonayo, kamwe hatuwezi pata maendeleo. hivyo kila mtu anaona kuwa akiondokana na serikali hii, bila shaka maendeleo yatapatikana. hivyo basi hata wanaotaka muundo wa sasa wa muungano kubadilishwa ni pamoja na kuachana na mfumo wa sasa wa utawala ili tuwe na mfumo ulio wazi zaidi na wenye kuleta uwajibikaji ili tuweze kupiga maendeleo, au kama hatuendelei, basi wawepo watu wa kuwajibishwa kwa hilo.
 
nadhani kilichowazi miongoni mwa wengi bara na zanzibar ni kuwa kwa aina ya serikali tuliyonayo, kamwe hatuwezi pata maendeleo. hivyo kila mtu anaona kuwa akiondokana na serikali hii, bila shaka maendeleo yatapatikana. hivyo basi hata wanaotaka muundo wa sasa wa muungano kubadilishwa ni pamoja na kuachana na mfumo wa sasa wa utawala ili tuwe na mfumo ulio wazi zaidi na wenye kuleta uwajibikaji ili tuweze kupiga maendeleo, au kama hatuendelei, basi wawepo watu wa kuwajibishwa kwa hilo.

Kuna ukweli ndani ya hoja yako. Mfumo tulionao umekwama,na hakuna dalili za kujikwamua,ndiyo maana Wazanzibari wanaona heri wawe na sauti/mamlaka kamili ya nchi yao waachane na mfumo uliojaa uzembe,wizi na rushwa!
 
Back
Top Bottom