Bei Mbaya
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 2,262
- 843
Wameanza kujiandaa kwa kampeni za uchaguzi mdogo baada ya kupata taarifa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Mpendazoe(Chadema) dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ajira,Kazi na Vijana Dr.Makongoro Mahanga(CCM) kushindwa kesi hukumu itakayosomwa 02/05/2012.
Wajumbe wa Mitaa na Wenyeviti wamekuwa wakizunguka mitaani na kuulizia namba za Vitambulisho vya Mpigakura, na hasa wamekuwa wakiwalenga watu wa rika la kuanzia miaka 40 na kuendelea kwani ni wazi na rahisi kutoa ushirikiano ikilinganishwa na vijana.
Ushahidi wa polisi ndio uliomkaanga Dr.Mahanga kufuatia kukamatwa na maboksi 12 ya kura siku ya uchaguzi na kufikishwa nayo kituo cha polisi Tabata, pia ktk majumuisho ya vifaa yaliyokuwa yakifanyika kata ya Buguruni inadaiwa maboksi kadhaa kutoonekana na mengine kukutwa wazi bila 'seal' za kufungia baada ya zoezi la kuhesabu kura kurudiwa.
Pamoja na nguvu kubwa kutumika kwa Ikulu kumpigia simu na kumtaka Msimamizi wa Uchaguzi Bw.Fuime kumtangaza mgombea wa CCM mshindi usiku wa manane ktk ukumbi wa Arnatoglou-Mnazi Mmoja, Dr.Mahanga tarehe 02/05 anaenda kuenguliwa.
Ikumbukwe mwaka jana Mpendazoe alikamatwa na maafisa usalama eneo la Airport na kufunguliwa jalada la kumiliki gari la wizi na baada ya kutoa uthibitisho wa umiliki, polisi kituo cha Buguruni walitupilia mbali mashtaka yaliyokuwa yafunguliwe mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika, habari za kiintelijensia zinadai kulikuwa na lengo la kumuua kwa kushukiwa kupora gari maeneo ya Gongo la Mboto baada ya awali kabisa kesi kumuelemea Naibu Waziri mmiliki wa bar maarufu ya Nyantare iliyopo jimboni kwake.