Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,520
- 86,081
nipo makaburini hapa mabibo_ makaburi kwenye mazishi ya mmoja wa makamanda wa ccm, ktk hali isiyo ya kawaida vijana hawa wanaonekana wavuta bangi wamemzuia Pastor asiendelee na ibada wakidai watamalizia wenyewe, Pastor nae amesusa ameondoka sasa hivi.
Picha ninazo kwene simu nitatuma baada ya kuweka kwenye computer, nitaleta na matukio mengine ila hawajafanikiwa kufanya vurugu hizo
Picha ninazo kwene simu nitatuma baada ya kuweka kwenye computer, nitaleta na matukio mengine ila hawajafanikiwa kufanya vurugu hizo
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/471062-magaidi-hawa-hapa.html
Haya jamani sasa, baadhi ya picha ambazo nilizipata kwa siri sana ni pamoja na hizi hapa chini, japo hazionekani vizuri lakini sitawasaidia wale akina Tomaso wenye mashaka, hilo ni gari alilojia huyo Padri, na hapo ndo wanaondoka, huyo kijana alievaa kofia na tshirt ya kijani ni mojawapo ya makamanda hao.
Mchezo ulianza hivi, tukiwa nyumbani ibada ilifanyika kwa amani kabisa huku makamanda hao wakiwa wamelizunguka jeneza la marehemu, baada ya ibada tukaanza safari ya kuelekea makaburini, na hawa jamaa wa CCM ndo waliobeba sanduku lenye mwili wa marehemu, tulipofika Padre akaendelea na ibada ile ya mwisho sasa na mwili ukashushwa kaburini, kaburi ambalo halikuchimbwa na makamanda hawa, baada ya hapo, Padre kama kawaida ya ibada za Kikristo, ni lazima waitwe ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya kuweka udongo kama ishara ya kumuaga marehemu then kinachofuatia ni udongo kuwekwa ili kuchimbia jeneza.
Wale vijana wa pale mtaani na ambao ndio waliochimba kaburi wakachukua machepe/sepeto ili kufukia mwili ule kumbe kwa kanuni za makamanda hawa mwili wa kamanda unafukiwa kwa mikono na sio kwa kitu kingine chochote, hapa ndipo vuta nikuvute ilipoanza.
hata hivyo, padri alikasirika na kuondoka sehemu ya tukio lakini baada ya muda kupita na busara za wazee kutumika, alikubali kurudi na kutoa hotuba fupi kama karipio kwa makamanda wale, huku akiuliza kuwa, KAMA KURA ZA MAONI WANAFANYA VURUGU VP WATAKAPOCHUKUA NCHI? swali ambalo lilizua tena utata na kumfanya padri aweke msalaba kwene kaburi na kusema AMEN kisha kuondoka.
Hawa ndio CCM makamanda