Elections 2010 CCM wachapana makofi Kawe; wachana daftari la majina; Londa ahusishwa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Wale walio karibu na Kawe

Jamani au kama mna waandishi wa habri kuna picha ya bure hapa wanakaya wa kata ya Kawe wanachapaa makofi live karibu na shell ya KOBIL.

Ni moto, sakata halisi lilikuwa kama ifuatavyo...ilibidi nisimame nikaangalie nini tena ...

Mmoja wa wanachama mwanamama akiwa anang'aka kama amenyimwa unyumba mwezi anasema haiwezekani kabisa huyu Londa anatufanyia mambo ya kihuni akuna anaemtaka hata afanye uhuni gani.....

Wakiongea kwa hasira wanasema wamekuja kupiga kura gafla wakati wanasubiri majina yao ndipo waliokuwa wameshikilia daftari wakadai majina yameisha weee...wakaanza kuuliza mbona mjumbe wetu huyu hapa iweeje atupo na tumeandika majina yetu moto ukaanza hapo yule mwenye daftari akaanza kujibu ovyo kabla ya mmoja wa mpiga kura ambae nilionyeshwa alikuwaakiwasha moto wa ngumi kama rashid matumla enzi zake kwa wanaume si wanawake..akachukua daftari akafungua akakuta katikati kuna karatasi mbili za majina zimechanwa alipotoka nje na kuwaambia wenzake ilikuwa balaa

....nimeacha saga linaendeleawenye vyombo vya habari mnakaribishwa mkaone picha za bure ;;;naona ccm wamemshindwa huyu londa kabisa kabisa walipomhoji mmoja wa waliokuwa na daftari wanasema wamepigiwa simu na mwenyekiti na wachane ukurasa wa kadhaa na kadhaa...wakaulizwa kwa mamlaka yapi wakadai Londa kawaamuru....haya nimeadnika jana ssiemu mkipanda bangi mtavuna bangi tusileeteane lawama tu ....
 
Wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya kawe karibu na kobil wanaomba itv;tbc na waandishi wa habari popote walipo muelekee kawe pale kata ya kawe ccm wilaya ya kinondoni...very urgent.wameomba niwasaidie ..waliokaribu mtawasaidia kuwajulisha wahusika
 
uchaguzi huu ni kiboko, nadhani kama hatujakuwa makini hautakuwa na mwisho mzuri

dawa ni kufata ushauri wa Dkt Slaa, hii mishahara na marupurupu ya wabunge ipunguzwe kabisa ili tupate watu wa kweli na wala sio hawa wa kutafuta kipato
 
mkuu ungerekodi kwa simu yako au ungepiga picha kwa kutumia simu yako ku-support habari yako manake jamaa wanaweza kukataa hivi hivi na kusema wao ni wasafai kama hamna ushaidi wa picha.

si umeona kwa "shyrose" kule wameweka picha.
 
mambo si ndo hayo, naimani siyo kawe tu, kila kitongoji haya mambo yanafanyika tena kwa mwenyekiti wa mtaa kuna uchafu wa hali ya juu sana Tanzania bila kuamka, tutaishia kula mara moja kwa siku, wengine wanakula mara sita au mara nane kwa siku.

Watu wamegeuza uongozi kuwa ni dili wala siyo Heshima kuwatumikia watanzania. Inatia kinyaa, inatisha, na inanipa nguvu ya kupinga kwa nguvu zote ccm na matawi yake.
 
siasa siyo skramenti hivyo basi tu-expect the unexpected
 
Kwetu ni Somalia. Tumezoea mapigano ya aina hii. sasa Wa-Tz munaojidai kukomaa kisiasa...

Lakini tuulizane, Mwenyekiti wao na yule katibu (Makamba) mwenye majibu ya ajabu wako wapi. nani mwenye amri na nani mwenye madaraka.

Baadaye sasa jiulizeni jinsi mpaganji wa Ikulu atakavyookota wabunge wa kuunda serikali! Kwa tabia yao, kutoambilika, atachukuwa hao hao. Bara tunahitaji serikali ya Kitaifa, tuachane na hawa WAHUNI.
 
:A S shade: Yaani we acha tu kipindi hichi inabidi Ze comedy, Futuhi waende likizo kwa muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom