sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,134
- 4,251
Usipoangalia vizuri unaweza ukachanganya udhaifu wa uongozi na kutojiamini.
Ninachokiona mimi ni tofauti tu ya sirka na uwezo wa watendaji wakuu wa CCM wa sasa ukilinganisha na wale wa waliokuwepo kwenye chaguzi zilizopita, ila kimsingi ile hofu na panic ya CCM kama chama ya mwaka 1995 sijaiona kwenye uchaguzi huu.
Uchaguzi wa mwaka 1995 hofu ilikuwepo kwa CCM sababu ya mazoea wa chama kimmoja bila hata mpinzani kutoka chama hicho,kura ya ndio au hapana. Kumbuka ilikuwa ni shindikizo kutoka kwa wafadhili wa nchi za magharibu na wala haikuwa mapenzi ya watawala.Pili njia zilizotumika kumpata mgombea uraisi ziliwakera baadhi ya vigogo waliokuwa wameenguliwa nafasi hiyo,hawakumuunga mkono mgombea uraisi,lakini hawakuwa na wasiwasi na viti vya ubunge Tanzania Bara.Tatu Wasiwasi ya kunyanganywa uongozi wa Zanzibar kwa nyanja zote na chama cha CUF ilikuwa kubwa. Mwaka 2010 mchezo umebadirika, huko Zanzibar watakuwa na serikali ya mseto,wasiwasi umepungua,Huku bara mwanzoni CCM haikuwa na wasiwasi sababu ushindi mkubwa iliokuwa imeupata chaguzi 3 mfululizo kwa muda wa miaka 15. Lakini Bara ya leo imegeuka kuwa Zanzibar ya 1995.Na upeo wa kuelewa mambo wa wapiga kura umeongezeka.