CCM tayarisheni mashine za kupumulia, mmelisikia tetemeko huko visiwani ?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,956
3,832
Wazee wenye elimu wametujuvya ya kuwa mara hii CCM inaanguka na sehemu ambayo itapigwa na chini ni Zanzibar ni baada ya kutokea tetemeko la ardhi baharini hivi majuzi, wazee hao walienda mbali zaidi na kusema hii sio dalili nzuri kwa CCM na kwa ishara hizi halina dawa wakubali tu bora nusu shari maana hata upande wa pili akikusudiya Tanganyika nako pia inagaragizwa.

Dalili ya mvua ni mawingu na upepo mkali tumeona Zanzibar na jana kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM chini ya mwevuli wa uzinduzi wa nyimbo za CCM, kijana polepole alisahau kuwakataza wasanii wasiseme CCM oyee au ,pigeni makofi na kwa kweli waliohudhuria kila ikitajwa CCM oyee, Mheshimiwa Magufuli hoyee kwa uwazi zaidi hakuna mtu alijibu salamu hizo ni wachache sana sana, mwishi wasanii wakiuliza mara moja tu, msio amini angalieni mtaliona hilo, inamaanisha watu hawakuendea kuisikia CCM, walichoendea wamekiona.

Wala hawakuwa wanafiki kuishangilia CCM waliikataa hapo hapo,na pole pole hakuonekana tena mpaka mwisho tena baada ya kutakiwa aende kutoa salamu za kufunga.

Tumeona namna shughuli ilivyofungwa au hamkuona? Je ndivyo shughuli zinavyofungwa haswa ikiwa zimetayarishwa na Chama kwa gharama kubwa na majilabu ya aina yake, mwisho walevi wanapigana.

Mwananchi mwanaccm kura ni siri yako endeleeni kupumbaa na CCM kadiri wanavyotaka, siku ya siku ikifika unaitupa mkono.
 
Chama cha mbogamboga kina hali mbaya sana. Si visiwani, si bara, yaani kule mtoto wa mzee Ruksa anakimbizwa na Maalim Seif, huku kwetu Magufuli amekabwa koo na mwanasheria nguli, Tundu Antipas Lissu.
 
Mapambano ya CCM na ACT huko Zanzibar yatakuwa yakusisimua

Maalim Seif akitumia uzoefu wa kushiriki kwenye knock out ya Urais Zanzibar na huku Mwinyi Junior akijinadi na Utawala wa Sayansi na Tekinologia

Lakini uzuri wa Zanzibar mmoja wao atakuwa Raisi na aliyeshindwa anakuwa makamu wa Raisi.
 
Mbona hamna picha ya tetemeko.

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone

[/url] Eti nabakia Africa. [/url]

Picha ilitokea mwisho Polepole alikuwa amekataa kwenda kutoa tangazo la kufunga,wenziwe walimsusia ,kama unakumbukumbu za hapa na pale ilichukuwa zaidi ya nusu saa ndipo alikubali kuja na hata hivyo hakusema sana kama ilivyo kawaida,someni alama za nyakati na hao nyumbu waliokusanyika kuimba walikuwa kama punda waliokata kamba,something wrong kwenye show.

Nyimbo zote hakuna jipya bora hata ile ye Jamani Membe huyoo Membe nasikia hapa mitaani mpaka watoto wadogo wanaiimba,
 
Huh

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone

[/url] Eti nabakia Africa. [/url]
 
Kama hakuna jumuiya ya kimataifa kuwalazimisha wamtangaze mshindi halali, sahau tetemeko lolote! Ingekuwa siyo ECOWAS, Yahya Jameh angelikuwa bado madarakani!
 
Kama hakuna jumuiya ya kimataifa kuwalazimisha wamtangaze mshindi halali, sahau tetemeko lolote! Ingekuwa siyo ECOWAS, Yahya Jameh angelikuwa bado madarakani!
Kwetu mashinikizo yote ya ndani ya bara la Afrika na kutoka nje ya Afrika, wakikomaza shingo
 
Niwaambie CCM ya zamani haipo, ipo ya kisasa iliyofanya maajabu kwa kipindi kifupi cha miaka 5 .
 
Endeleeni kujitekenya na kucheka..lakini kama mliweza kuangalia nyimbo za kuisifu ccm tena hadi saa sita usiku basi jibu mnalo tayari.
 
Endeleeni kujitekenya na kucheka..lakini kama mliweza kuangalia nyimbo za kuisifu ccm tena hadi saa sita usiku basi jibu mnalo tayari.
Tamasha limeangaliwa na dunia nzima, watanzania wamepata uelewa mkubwa sana kupitia nyimbo za wasanii na wamerahisishiwa kujua kazi aliyofanywa na ccm.Kazi kwao wapinzani kuubadili upepo wa jana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom