CCM ni 'nambari one' katika nini?

CCM is the land of opportunity. Wapi pengine mmeona kiongozi ovyo aka panda mpaka kuwa raisi au mtu asiye na ujuzi wowote akapewa kitengo maalumu? Wapi pengine mmeona mtu ana tajirika ndani ya mwaka mmoja? Wapi pengine mtu asiye na upeo wowote aka pata zali kupewa "Kiti maalumu"? Wapi pengine mtu anaiba mchana kweupe lakini bado anaendelea kuitwa muheshimiwa, kupewa security detail na kuendelea kutunzwa na pesa za watu aliyo waibia?
 
CCM is the land of opportunity.
Wapi pengine mmeona kiongozi ovyo aka panda mpaka kuwa raisi au mtu asiye na ujuzi wowote akapewa kitengo maalumu?
Wapi pengine mmeona mtu ana tajirika ndani ya mwaka mmoja?
Wapi pengine mtu asiye na upeo wowote aka pata zali kupewa "Kiti maalumu"?
Wapi pengine mtu anaiba mchana kweupe lakini bado anaendelea kuitwa muheshimiwa, kupewa security detail na kuendelea kutunzwa na pesa za watu aliyo waibia?

MWANAFALSAFA1,
Huu ndio huo unambari one au Ni FALSAFA ZAKO tu mkuu?
Mmmmhh/////////////////////???????????????
 
Ya kwanza kuinua elimu kama hivi

WANAFUNZI12.jpg

Jibaba Bonge big up,nimekubali hapo sina cha kuongeza
 
'Nambari eeeh, nambari one ni CCM, twende Kolimba twende tieni; tieni tieni kwa moyo mmoja eeh, nambari one eeeeh, nambari one ni CCM'

Duh hicho kipande kimenikumbusha long time enzi za giza, Kapteni Komba alivyokuwa anatuimbisha tumchague Mwinyi badala ya kivuli................tehe tehe..!
 
Kwanini wafanikiwe kila uchaguzi?
Inawezekana kuiba kila wakati?

Exaud, wizi nao ni tabia, na tabia yoyote ikishajengeka ni ngumu sana kuiacha na inawezekana walipoona mara ya kwanza wamefanikiwa,mwaka uliofuata wakasukumwa zaidi kutumia mbinu waliotumia miaka iliopita.
 
Exaud, wizi nao ni tabia, na tabia yoyote ikishajengeka ni ngumu sana kuiacha na inawezekana walipoona mara ya kwanza wamefanikiwa,mwaka uliofuata wakasukumwa zaidi kutumia mbinu waliotumia miaka iliopita.

Mkuu MSINDIMA.
Kama haya ni kweli,
Basi ipo kazi.
 
CCM is the land of opportunity. Wapi pengine mmeona kiongozi ovyo aka panda mpaka kuwa raisi au mtu asiye na ujuzi wowote akapewa kitengo maalumu? Wapi pengine mmeona mtu ana tajirika ndani ya mwaka mmoja? Wapi pengine mtu asiye na upeo wowote aka pata zali kupewa "Kiti maalumu"? Wapi pengine mtu anaiba mchana kweupe lakini bado anaendelea kuitwa muheshimiwa, kupewa security detail na kuendelea kutunzwa na pesa za watu aliyo waibia?

Utasema mchana,
Usiku utalala.

Amini usiamini, Hata mwaka kesho CCM itaingia ikulu mchana kweupe.
Mwenye hoja na aseme.
Nikitoka kisomoni , nitawapa vidonge vyenu.
 
Utasema mchana,
Usiku utalala.

Amini usiamini, Hata mwaka kesho CCM itaingia ikulu mchana kweupe.
Mwenye hoja na aseme.
Nikitoka kisomoni , nitawapa vidonge vyenu.

Kwani wewe unasema usiku na kulala mchana? Kama untaka kuiimbia CCM nyimbo za mapambio hauja katazwa. Ndiyo maana kuna kuangalia pande zote za shilingi. Wewe sema tu mazuri ya CCM na wengine wakisema mabaya ya CCM hiyo ndiyo demokrasia. Waiting for hivyo vidonge.
 
Wewe unaona CCM unambari one wke ni upi mkuu?


Kwakweli sina jibu mkuu.
Wala sijui lipi si jibu.

Kila nisikiapo SLOGAN hiyo huwa haimalizwi kuwa ni nambari one kwa kitu gani.

Ila majibu ninayopata hapa, yananipa kufikiri zaidi.
Labda tumpate KADA WA CCM atupenyezee siri ya fumbo hili.
CCM ni NAMBARI MOJA.
 
Kwa Muda mrefu nimekuwa nikisikia mbiu hii kwamba ''CCM NI NAMBARI ONE''.

Yaani CCM NI NAMBA MOJA.
Baada ya kufikiri sana, nimegundua kuwa sijui maana ya SLOGAN hii.

Naamini hapa jamvini huenda mwaweza kunijulisha kuwa ,
CCM NI NAMBARI ONE katika nini hasa?

Au ni msemo tu wana JF?
Kati ya walaji wote, nambari wani ni CCM

CCM inajiita nambari wani, hilo halina ubishi, lakini ni nambari wani katika mambo gani? CCM haisemi wazi yenyewe ni namba wani kwa kufanya nini na nani namba mbili na wa mwisho ni nani!

La kwanza ambalo wao CCM wanalionea haya kusema ni hili la rushwa. CCM ni mlaji rushwa mzuri sana. Kati ya Walaji wote katika nchi hii, nambari wani ni CCM. Mnamo mwaka 1978 mwezi Februari tarehe tano, kulikuwepo na sherehe kubwa sana pale Dodoma ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kuzaliwa kwa CCM tangu 1977 hapo TANU ilipounganishwa na ASP. Katika sherehe hizo mgeni rasmi (na mhutubiaji mkuu) alikuwa rais wa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere. Naikumbuka vyema hotuba yake, alilaani sana ulaji rushwa, akawafananisha walaji rushwa na malaya au kwa lugha ya siku hizi "changudoa". Katika moja ya kauli zake akasema kwa ukali, kuendelea kuwa na wala rushwa tunafuga malaya ndani ya ofisi." Hapo ndipo alipoamua kuiweka Anti-Corruption Squad chini ya ofisi yake na maelekezo yake mwenyewe. Mwaka huo 1978 ndio uliokuwa mwaka wangu wa kuajiriwa na ajira yangu ya kwanza ikawa hiyo ya "Investigator" Katika kikosi cha kuzuia rushwa. Kutokana na jinsi Nyerere alivyosema kwa ukali kuhusu rushwa, niliingia kwenye kikosi nikiwa na moto usio wa kawaida, nilidhani ya kwamba ni kweli serikali yake iko kinyume na rushwa, kumbe sivyo nilikuwa na mawazo ya kitoto, kwani haukupita muda kabla ya kugundua kwamba CCM ndiyo shina na chimbuko la rushwa yote iliyoko serikalini na kwenye vyombo vya dola, na kwenye mashirika ya umma.

Kuna wakati mmoja ambapo Nyerere alitutuma kuthamini mahekalu ya Mikocheni, Osterbay, Mbezi na Masaki, nakumbuka nyumba ya mtu mmoja kwa wakati huo hata kabla ya kumalizika kwa hatua za mwisho za ujenzi, tayari ilikuwa na thamani ya Tshs.800,000,000 (Milioni mia nane). Kwa wakati huo dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Shs.9.50 (tisa na senti hamsini) za Tanzania, kwahiyo kwa makadirio ya haraka nyumba ya mtu yule ilikuwa sawa na dola za Marekani milioni mia moja. Kulikuwa na nyumba nyingi tu za aina hiyo hadi mwisho wa zoezi hilo lililositishwa kwa amri ya wakubwa. Katika kufuatilia mwenendo wa rushwa nchini neno moja nililoliona kwa wakati huo ambalo lilinifanya nishawishike kumweleza kinaganaga Rais wa nchi ni nafasi ya mashirika ya umma katika kuuhujumu uchumi wa nchi.

Wakati huo kulikuwa na mashirika yapatayo 400. Mengi kati yao yalikuwa hayana hata mahesabu kamili ya kile kinachoingia na kile kinachotoka. Mashirika yalikuwa kama mtu wa kati wa kutoa fedha kwenda Hazina, ama kupokea fedha toka Hazina kama ruzuku. Humo ndimo wahujumu walipotajirikia maana walikuwa na uwezo wa kuchota kiasi chochote watakacho na kile wawezacho.

Lakini si mashirika ya umma tu bali CCM kwa wakati huo ilikuwa na uwezo wa kuamuru Hazina itoe kiasi fulani kwa ajili ya mkutano wake nayo Hazina ikatoa bila ubishi. Mashirika ya umma nayo hasa Benki, Bandari, Bima, NPF, Reli na mengineyo yaliyokuwa na uwezo wa kutengeneza fedha nyingi yaliweza kuamriwa kutoa bila ubishi. Lakini baada ya kuikatia CCM mgawo wake nao (wahusika) walichota kiasi chao. Kwa utaratibu huu ni wazi kwamba hakuna ambaye angeweza kumnyooshea kidole mwingine na kusema wewe "u-mbadhirifu". Kwa wakati huo kikao kimoja tu cha NEC ya CCM kilitumia kati ya Tshs.210,000,000 na Tsh.400,000,000. Mtu anaweza kukisia kitendo cha kutumia milioni mia mbili au mia nne kwa muda wa siku tatu au nne tu kwa wajumbe wasiozidi 1,000!

Ni dhahiri kwamba watu walikuwa wanakutana ili kugawana fedha na wala siyo kutumia fedha ama kufanya mikutano. Mara baada ya mkutano mjumbe tokaWilayani tu aliambulia 50,000/-, na yule wa mkoa alitokana 100,000/- ambazo zilikuwa zikiwekwa ndani ya "Handbag" ambazo kwa geresha bag hizo ziliandikwa Halmashauri Kuu ya Taifa. Ikumbukwe kwa wakati huo mshahara wa mtu mwenye digrii ulikuwa Shs.1,420/- (Elfu moja na mia nne ishirini) baada ya makato ya kodi zilisalia Tshs.1,180 (Elfu moja na mia moja themanini). Mtu yeyote mwenye kutazama mambo katika uhalisi wake anaweza kuona ni kwanini CCM ikawa kimbilio la wasiosoma na wasiokuwa na elimu ilimradi tuwa we na sifa kuu ya unafiki, kujikomba na kuwa tayari kutetea uwongo. Katika uhalisi wa mambo wakuu wa mashirika ya Umma nao waligundua kwamba viongozi wa CCM wanachota fedha za wananchi kwa kivuli cha mikutano na semina au warsha, kwahiyo, na wao wakaamua wasilaze damu, kila CCM ilipochotewa mgawo wake na wao walichota kiasi chao wakijua kwamba hakuna atakeyehoji wala kuwachukulia hatua za kisheria.

Katika muda wa miaka miwili ya uchunguzi wangu katika kikosi, pia niligundua kwamba hakuna mkubwa yoyote wa shirika la umma, au kiwanda, au kampuni ambaye alipewa nafasi hiyo pasipo kujulikana na chama ama pasipo mtu wa kumpigia debe huko CCM. Viongozi wa mashirika ya umma hawakupewa nyadhifa kwa sababu ya sifa ya kisomo peke yake bali pia walikuwa ni "Watoto wa Chama, na kwahiyo walikuwa na daraja lao maalum la "usiniguse". Mimi baada ya kuona kwenye kikosi tunafunga watu wa ngazi ya chini hasa mahakimu, mapolisi wa vyeo vya kati na chini, madaktari, na wadokozi tu wa mali ya umma badala ya wahujumu, ndipo nilipoamua kumwandikia Rais mada inayohusu rushwa kama ilivyo katika nchi, na katika mada hiyo wahujumu niliwaita "the Highly Corrupt". Nikaelezea jinsi CCM inavyochotewa fedha na jinsi watumishi wa ngazi za chini wanavyoiiga CCM na wao kuchota fedha kila mara CCM inapochotewa. Nikaelezea jinsi ubadhirifu wa chama unavyochochea "influence". Wafanyakazi wa kada ya chini kabisa nao kutumia nafasi zao kujinufaisha. Nilielezea jinsit abia ya Chama Cha Mapinduzi isivyokuwa ya kijamaa na jinsi kada ya juu wanavyoishi kama mamilionea ndani ya Taifa wanalodai ni masikini.

Niligusia baadhi ya vifungu vya Azimio la Arusha jinsi vinavyowabana watu na kusababisha waigeukie rushwa kama njia ya mkato ya ukidhi mahitaji yao. Nilieleza jinsi ambavyo muundo wa serikali bado ni wa Kikoloni na kwahiyo watumishi walioko kwenye nafasi za kati na za chini (ambazo enzi za mkoloni zilikuwa nafasi za weusi) ambavyo bado wanapuuzwa kimaslahi. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo nilipendekeza yafanyike mojawapo ni "ambush". Kutokana na ukweli kwamba niliutaja wazi ubadhirifu wa CCM, na kuisema wazi kwamba inachochea rushwa, na pia kugusia siasa ya ujamaa na kusema wazi kwamba serikalini bado kuna muundo wa kikoloni, Rais Nyerere hakupendezwa akaamua kunifukuza kazi.

Baada ya muda kupita niliitwa Ikulu na kukabidhiwa barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Rais, na Katibu wa Baraza la Mawaziri Bw. Timothy Apio, barua ilikuwa na mistari miwili tu, "Rejea kichwa cha habari hapo juu. Rais amekufukuza kazi." Baada ya miaka mitatu zoezi la Moringe Sokoine lilitekeleza karibu nusu ya yale niliyopendekeza kwa Nyerere lakini neno wahujumu likachukua sura mpya na tofauti na tafsiri yangu, badala ya kuwashughulikia watu ambao ni "Highly Corrupt" kama nilivyokuwa nimeelezea, wakavamiwa "Wafanyibiashara" wakubwa huku "watoto wa chama" wakiachwa pasipo kuguswa wao wala mali zao walizozipata kwa njia ya rushwa. Mtu anaweza kushangaa Wahujumu wangewezaje kufanikiwa mambo yao bila ya kuwashirikisha mameneja. Ilipokuja awamu ya Mwinyi wengi wao wakaacha kazi naye Mwinyi kwa kutaka kuweka watu wake, akawa amewapa nafasi ya kuondoka bila kubughiwa na kwenda kutumia mali walizoziiba kwa amani. Labda Mwinyi hakujua kwamba anarithi Mashirika yaUmma amabyo ni mfu sawa na maiti zinazongoja kuzikwa, wakati wenyewe wauaji wanakwenda kuwa na kipindi kingine kipya cha kufanya karamu ya kusherehekea mali za dhuluma. Hata hivyo majereha au "damage' ambayo "watoto wa chama" wameuachia uchumi na nchi yetu si ya kutibika kwa muda mfupi, nadhani hata madeni ambayo mlalahoi sasa anayalipa kwa uchungu kwa kiasi kikubwa yanatokana na hujuma zao.

Mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kuona ni kwanini CCM kama taasisi pamoja na wateja wake hawataki kuachia madaraka mapema, wanaogopa kwamba ukurasa waliokwisha ufunika yaani ukurusa wa Mashirika ya Umma, ubadhirifu walioufanya enzi za mfumo wa chama kimoja na madhambi mengine mengi ya Azimio la Arusha, usije ukafunuliwa wakati watu wengi wangali na kumbukumbu za maovu hayo vichwani kwani kuna hatari watatiwa misukosuko ama wataaibika. Kwahiyo dawa pekee wanayoiona inawafaa ni kushikilia madaraka hadi yaje maovu mengine mapya ya kufunika dhambi yao walioifanya kati ya miaka ya sabini na themanini.

Lakini ni vigumu sana kufunika dhambi kwa njia ya ujanja na hila, kwa mfano dhambi ya CCM kudhulumu Walalahoi itabaki wazi sawa na doa la damu katika nguo nyeupe. Mpaka sasa CCM inashikilia majengo yanayodaiwa kuwa ni jJengo la CCM la Wilaya, au jengo la CCM la Mkoa, kama lilivyo sasa jengo la Umoja wa Vijana hapa Dar es Salaam, na Jengo la Chimwaga kule Dodoma. Hizi ni mali za wananchi, zimechumwa kwa jasho la watu wote na hivyo haifai CCM kuendelea kuyahodhi.

Vipo viwanja vya mipira kama Kirumba n.k., maeneo yaliyo wazi ambayo CCM inatumia kulaza magari na kuwatoza watu fedha. Je wana haki gani na mali hizo wakati ni mali za Taifa? Majengo haya yalistahili kunyang'anywa toka mikononi mwa CCM na kuwa mali ya serikaliili yatumike kwa huduma zingine za jamii kama vile Hospitali, Kliniki za kina mama wajawazito, mahakama, ama madarasa ya kusomea wanafunzi.

Si halali wananchi wapungukiwe majengo ya huduma za lazima katika maisha yao ya kijamii wakati CCM inahodhi majengo yao na kuifanya miradi yake ya kuiingizia fedha.

MOJA ya Sababu za TANU kutoa Azimio la Arusha mwaka 19967 ilikuwa ni kuondoa unyonyaji kati ya mtu na mtu, au kundi moja kunyonya kundi jingine. TANU kama chama cha ukombozi kilikuwa kimedhamiria kwa dhati kabisa kuondoa mfumo wa matabaka ambao uliachwa na mkoloni. Enzi za mkoloni Watanganyika waligawanywa katika matabaka matatu, kulikuwa na raia wa daraja la kwanza yaani Wazungu, na raia daraja la pili yaani Waasia na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, na raia waligawanywa katika makundi mawili wakulima wadogo au peasants kama walivyoitwa na wafanyakazi.


UWEZO wa kiuchumi, maisha bora au maisha duni, umasikini au utajiri, ulitegemea mtu anatoka tabaka gani. Kwasababu ya tofauti ya kipato kati ya Mwafrika (mweusi) na Mzungu au Mhindi (mweupe) ni dhahiri kwamba wenye uraia wa daraja la tatu ndio waliokuwa maskini kuliko matabaka mengine.

Baada ya kupatikana Uhuru 1961, yalitokea mabadiliko kidogo tu, kwani wale waliopigania uhuru hasa viongozi, na wasomi wachache wakachukua nafasi za Wazungu wakawa raia daraja la kwanza, Waasia na wafanyabiashara wakubwa wakabakia kwenye darajala kati, na Waafrika walio wengi yaani walalahoi wakabakia daraja la tatu, daraja la kufanya kazi nyingi, kazi kubwa lakini malipo kidogo, daraja la wazalishaji kwa manufaa ya watumiaji walioko daraja la kwanza na la pili. Ndiyo maana mara lilipotangazwa Azimio la Arusha, wananchi wengi katika ujumla wao walihamasika na kuunga mkono, tumaini lao lilikuwa kwamba "utabaka" utaondolewa na badala yake utajengwa mfumo wa kulinda haki kwa ajili ya wote na kwasababu ya haki watu katika ujumla wao wataishi maisha bora.

Tumaini la namna hiyo ndilo lililomfanya Mtanzania awe mtu wa amani na utulivu. CCM inajigamba na kujitapa kama bingwa wa amani na utulivu lakini hawajui siri ya amani na utulivu. Wao CCM wanajivunia amani kwasababu hakuna lolote la kujivunia la maana walilolifanya. Ukweli ni kwamba siku zote wanadamu tunaishi kwa matumaini, kwahiyo lile tumaini ambalo lilitolewa na Azimio la Arusha liliwafanya wawe wasikivu kwa viongozi wao na watulivu. Lakini sasa tumaini lile limepotea, matazamio ya watu kuishi maisha bora siku za usoni yanazidi kutoweka kila siku ipitayo. Tumaini la kwamba haki itatawala katika nchi hii nalo limefutika kabisa, badala yake mlalahoi ni mtu anayetazamia kudhulumiwa wakati wowote.

Kama si kudhulumiwa na dola, basi ni kudhulumiwa na mwenye nguvu (kiuchumi au kisheria) kuliko yeye. Njaaa na mashaka vimekuwa ni sehemu ya miasha ya kila siku ya mlalahoi. Hali kama ilivyo katika nchi inahitaji masihi au Mtume, mtu atakayekuwa tayari kufanya kazi kwa manufaa ya wengine pasipo kutazamia malipo ama mafao yoyote katika maisha haya.

Hali ni mbaya kuliko ilivyokuwa mbaya enzi za Mkoloni hadi kuwasukuma baadhi ya Wazalendo kudai uhuru. Umaskini umeongezeka, umekuwa na kukithiri hadi kufikia kiwango ambacho sasa hautibiki tena. Umaskini wa Tanzania hauna tofauti na ukimwi, hauna dawa, unaua, unauma na unatesa sana kabla ya kummaliza mtu kabisa. Lakini je ni nini chimbuko hasa la umaskini wetu kama taifa? Ni nini sababu halisi ya sisi kuendelea kuwa maskini? Rais Mkapa anadai kwamba Watanzania ni wavivu wanapenda kula pasipo kufanya kazi! Mkapa huyo huyo akiwa kama Mwenyekiti wa CCM anasema Ilani ya CCM haitekelezeki, na sera za chama chake hazitekelezeki.

Sasa hata watu wakifanya kazi kwa bidii kama wafanyavyo Wajapani watafanikiwa chini ya mpango gani? Maana ikumbukwe kwamba sera ni mpangilio au utaratibu wa kisayansi wa kutatua tatizo au kufanikisha jambo. Sasa chini ya sera za CCM ambazo hazitekelezeki, mkulima wa bongo hata angevuna tani milioni za mazao yake, bado atakuwa masikini kwasababu hakuna soko la uhakika linalompa "guarantee" kwamba atapata fedha. Vivyo hivyo mchimba madini wa bongo, hata angevuna madini yenye thamani ya matrioni ya dola bado atakuwa maskini tu kwasababu hakuna "guarantee" ya soko, baya zaidi serikali ya CCM inawapa nafasi wawekezaji ya kuvuna madini hapa nchini na kuyauza moja kwa moja kwenye masoko ya nje na mlalahoi hawezi kumudu ushindani wa namna hii kwa ajili hiyo mlalahoi hata aliyezaliwa ndani ya utajiri bado atakuwa maskini wa kutupwa mfano hai ni hao wakazi wa Tunduru (kwenye Alexandrite inayotajirisha wageni) Mererani (kwenye Tanzanite inayotajirisha wageni). Handeni (kwenye Garnet, Tomalini, Rhodrite n.k. isiyoguswa), Mahenge (kwenye Rubi inayotajirisha wageni), Geita, Ulyankulu, (kwenye dhahabu inayotajirisha wageni).

Wenyeji wa maeneo hayo ni maskini wa kutupwa, lakini makampuni ya kigeni yaliyopewa ruhusa na serikali ya CCM kuvuna rasilimali zilizo kwenye maeneo hayo wanatajirika kwa namna isiyoelezeka. Kulingana ndata za Profesa Lipumba, kampuni ya Shanti Gold Mines ya Ghana iliyopewa leseni ya kutafiti dhahabu maeneo ya Ulyamkulu iliamua kuuza baadhi ya hisa zake kwa dola za Kimarekani milioni mia nne, kwakuwa mauzo yamefanyika nje ya nchi serikali ya Bongo haikupata hata senti tano. Mambo hayo yamefanyika baada ya serikali kuwanyang'anya wachimbaji wadogo wadogo maeneo hayo. Serikali hiyo hiyo inayolia umaskini kila siku, imepitisha sera ya kwamba kila mwekezaji anayewekeza katika Tanzania alipe dola tatu kama kodi kwa kila dola mia anazopata kutokana na kuuza nje mali za nchi yetu. Hii tafsiri yake ni kwamba kwa kila mali inayotoka nje ya nchi yetu, Watanzania tunabaki na dola tatu na mgeni anakwenda na dola 97.

Aliye nacho anazidi kuongezewa, na yule ambaye hana ananyang'anywa hata hicho kidogo alicho nacho. Hii ni sera ya kuifilisi nchi na kumdidimiza mlalahoi, hata Mkoloni hakufanya unyonyaji kama huu. Wakati serikali ya CCM inawachia wageni kuja kuchota utajiri wa nchi yetu kana kwamba hauna mwenyewe, serikali hiyo hiyo ndio iliyomshikia bango mzalendo kuhakikisha analipa kodi hata kwenye biashara zisizompa faida, Serikali inatoza kodi ya mapato hata kabla mtu hajapata. Serikali inamlipisha mtu kodi hata kwa vitu ambavyo havizalishi kama vile baiskeli, mbwa, paka, mbuzi na kondoo. Baada ya serikali kumkamua mlalahoi namna hiyo ingetazamiwa kwamba walau ingeboresha huduma za jamii kama tiba na elimu, lakini wapi fedha zinazotengwa wakati wa Bajeti kwa ajili ya elimu na afya zinapungua mwaka baada ya mwaka.

Kuna siku sikuamini masikio yangu wakati mganga mkuu wa wilaya ya Mpwapwa aliponiambia fedha ilizitengewa hospitali ya wilaya ni Tshs.16,000 kwa mwezi, lakini juzi wakatki Profesa Lipumba alipokuwa akieleza jinsi bajeti ya Wizara ya Afya inavyofinywa na serikali ya Mkapa ndipo nilipoamini kwamba kumbe kweli wanaweza kutoa Ths.16,000 na kutarajia hospitali ya wilaya itumie kwa mwezi mzima. Hii ndiyo roho ya Chama Cha Mapinduzi, roho inayofanana na mumiani ambaye anafyonza damu ya mtu bila huruma alimradi yeye akapate faida.

Roho ya CCM haina tofauti na wachuna ngozi wa Mbeya kwani mlalahoi amechunwa hadi kuwa hoi zaidi wakati yenyewe CCM inakuwa juu zaidi uthibitisho wa hili ni jinsi ilivyoshughulikia malipo ya wastaafu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, wengine walilipwa hundi za Ths. 120/-, na serikali inajigamba kwamba imelipa.

Hii maana yake nini? Ni wazi kwamba haya ni mazoea ya unyonyaji na ukiukaji wa makusudi wa haki za msingi za binaadamu. Huko serikalini wanajua fika kwamba Shs.120/- za mwaka 1977 ni tofuati kabisa na 120/- za mwaka 2000 lakini bado wanafanya hivyo kutokana na kujua kwamba walipwaji hawawezi kufanya lolote kwani mara watakapodiriki tufanya lolote, basi rungu la dola litawainukia.

Serikali ya uhuru iko tayari kupiga, kuumiza na hata kuua raia wema wanaodai haki zao. Kwa mkulima asiyeweza kuandamana wala kukusanyika pamoja na wakulima wenzake ili kudai haki yake kiuchumi, amekuwa kama jalala la CCM.

Kwa muda mrefu amekopwa mazao yake na hakulipwa, si kwasababu hapendi kulipwa la hasha bali kwa kuwa tu hana njia au hajui atumie njia gani kudai haki yake.Matokeo yake mkulima amekuwa hoi bin taabani kwa umaskini, ufukara na uduni wa maisha. CCM kwa kuwa hawapati misukosuko yoyote kutoka kwa mkulima, wamemhesabu huyo kama mteja wao wa kudumu. Wanatamba kwamba CCM ina nguvu vijijini, wana uhakika wa kuzoa kura nyingi toka vijijini na baada ya hapo CCM hujihesabu wameshinda.

Kwa umaskini wa mwanakijiji, wao hauwahusu wala hawahesabu kwamba umaskini walio nao wakulima wa bongo ni ushahidi kwamba wameshindwa kutawala. Matokeo ya udhalimu na udanganyifu wa aina hii ni kizazi kipya kisichoafiki uwongo kukimbia toka vijijini na kuja mijini "kubangaiza".

Viongozi wa CCM kwa kuwa wana giza la ibilisi kwenye fahamu zao husimama bila haya na kutoa miito ya eti vijana kuacha kukimbilia mijini kana kwamba miito yao ndio dawa. Hawataki kukabiliana na ukweli kwamba tatizo la vijana kukimbilia mijini ni matokeo ya sera zao mbovu na zisizotekelezeka hasa zile zinazohusu vijana. Hata viongozi wa CCM wa vijana nao akili zao zimetiwa giza kama baba zao, huinuka kusema kwa niaba ya vijana lakini katika yote wanayoyasema hakuna hata moja linalohusu vijana wala linalogusa maisha ya vijana wala linalowakilisha matatizo halisi ya vijana wa nchi hii.

Wao viongozi wa vijana wa CCM wapo kama watumishi wa itikadi mfu ya chama hao. Mfano hai ni kauli za Emannuel Nchimbi kwa Askofu Kakobe, yote aliyosema Nchimbi hayana maana wala hayawakilishi maslahi ya vijana. Sidhani kama Nchimbi anayaelewa matatizo ya vijana wenzake kwa kuwa yeye ni mtu wa kubebwa na kuufurahia huo upendeleo anaoupata kutoka kwa watawala. Vijana wenzake kila mara wanafungwa mashati na kushitakiwa kama wazurulaji wakati hakuna ajira wala mazingira ya kujitegemea.

Vijana wenzake kila mara wanabambikiziwa kesi za kukutwa na misokoto ya bangi au ujambazi.

Vijana wa kike wanabughudhuiwa kila mara kwamba ni wakahaba, wazurulaji na wasio na kazi.

Vijana wenzake walioko shuleni wana lishe duni, na vifaa duni vya kusomea hali wengine wanapinda migongo kwa kukosa madawati ya kukalia wakati wa kuandika.

Kila siku vijana wananyanyaswa kwenye daladala kwa namna ya kutisha, je mbona hayo yasimuume Nchimbi hata akafumbua kinywa chake kusema kwa niaba ya vijana wenzake? Ama kwake hoja ya kuchanganya dini na siasa imekuwa kero kubwa kuliko kero zote wanzopata vijana wa nchi hii? Najua wazi huyu kijana anakabiliwa na maradhi ya "diversion of mind".

Hii ndiyo kazi ya Nambari wani, kuzifanya akili za watu kuacha kuuelekea ukweli na uhalisi wa mambo badala yake "kuchepuka", au kupinda mithili ya treni linaloacha reli na kwenda pembeni. CCM mbali ya kunyonya watu kiuchumi na kuwaacha hoi, pia imewanyonya kiroho na kuwafyonza kiakili hadi wamefikia kiwango kile ambacho Nabii Ezekieli anaelezea kwamba "watu wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii."

Ukombozi wa kweli wa mwananchi ni lazima uende sambamba na kuing'oa CCM madarakani
 
Ukombozi wa kweli wa mwananchi ni lazima uende sambamba na kuing'oa CCM madarakani

Kwa fikra kama hizi nitaendelea kuwepo CCM sana tu, iwapo hizi ni fikra mbadala nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM daima.
Hebu get serious kidogo gavana hiyo ndio njia sahihi? hivi wazo lenu kuu ni kuing'oa tu CCM madarakani na mtafanya hivyo kwa kuorodhesha mabaya ya CCM bila hata kuonesha mbadala wa sera au muono wenu?
 
Kwa fikra kama hizi nitaendelea kuwepo CCM sana tu, iwapo hizi ni fikra mbadala nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM daima.
Hebu get serious kidogo gavana hiyo ndio njia sahihi? hivi wazo lenu kuu ni kuing'oa tu CCM madarakani na mtafanya hivyo kwa kuorodhesha mabaya ya CCM bila hata kuonesha mbadala wa sera au muono wenu?
Msafara wa mamba na kenge mpo.
Hebu orodhesha mazuri ya sisi m kwanza!
 
Utasema mchana,
Usiku utalala.

Amini usiamini, Hata mwaka kesho CCM itaingia ikulu mchana kweupe.
Mwenye hoja na aseme.
Nikitoka kisomoni , nitawapa vidonge vyenu.
Emma wewe na wewe ni mmoja kati ya wale wanaotoa kura sisi m kwa sababu ya TOT? Naona umeweka tungo za TOT hapo juu.
Ni watanzania wajinga wa zamani wataendelea kuwapa kura kwa sababu Komba ameimba ngonjera. Watakaotoa kura zao ni wale ambao kwao kucheza ngoma wakati wa mavuno na kupata kilevi ni jadi. Na mwisho wa maisha yao. Thinking capacity yao inaishi kwenye ngoma basi.
Na wewe utakuwa kati yao?
 
Kati ya walaji wote, nambari wani ni CCM

CCM inajiita nambari wani, hilo halina ubishi, lakini ni nambari wani katika mambo gani? CCM haisemi wazi yenyewe ni namba wani kwa kufanya nini na nani namba mbili na wa mwisho ni nani!

;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; Najua wazi huyu kijana anakabiliwa na maradhi ya "diversion of mind".

Hii ndiyo kazi ya Nambari wani, kuzifanya akili za watu kuacha kuuelekea ukweli na uhalisi wa mambo badala yake "kuchepuka", au kupinda mithili ya treni linaloacha reli na kwenda pembeni. CCM mbali ya kunyonya watu kiuchumi na kuwaacha hoi, pia imewanyonya kiroho na kuwafyonza kiakili hadi wamefikia kiwango kile ambacho Nabii Ezekieli anaelezea kwamba "watu wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii."

Ukombozi wa kweli wa mwananchi ni lazima uende sambamba na kuing'oa CCM madarakani

Gavana,
Hizi hoja zako najua zitawasumbua wengi.
Zinahitaji kujibiwa na mtu mwenye roho ngumu.
 
'Nambari eeeh, nambari one ni CCM, twende Kolimba twende tieni; tieni tieni kwa moyo mmoja eeh, nambari one eeeeh, nambari one ni CCM'

Duh hicho kipande kimenikumbusha long time enzi za giza, Kapteni Komba alivyokuwa anatuimbisha tumchague Mwinyi badala ya kivuli................tehe tehe..!

Kweli MKUU ,
Hivi huo unambari one ni upi?
Na hiyo tieni, tieni nayo??????
 
Back
Top Bottom