CCM na Siasa za maji taka kwa vyama na watu wanoonesha upinzani Mkubwa kwao tangia 1995- 2015 .

simaye

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
426
214
Mfumo wa Chama dola na harakari za vyama vingi katika kuimarisha Demokrasia Tanzanaia.

Mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini Tanzania ulianza rasmi mwaka 1992 na kuanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza mwaka 1995.
Katika kipindi hicho cha uchaguzi wa mwaka 1995, mwanasiasa aliyeonekana kuwa tishio kwa ccm ni Agustino Lyatonga Mrema. Mzee aliitikisa sana ccm na mgombea wake kiasi chakuonesha kuwa kama ccm wasingejipanga vema wandepoteza udhibiti wa dola katika uchanguzi ule. Shukrani kwa hayati baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere kuingilia kati na kushiriki katika uchaguzi ule kwa kusaidia kampeni za kumnadi mgombea wa ccm Ndugu, Benjamin Mkapa.
Ni ukweli usiopingika kwamba bila mwalimu katika kipindi hicho ccm walikuwa katika wakati mgumu sana dhidi ya Mrema. Zipo tetesi kuwa katika uchaguzi ule Mrema alishinda lakini kwa sababu ya kukosa wabunge ilikuwa vigumu kumtangaza kama mshindi kwa kuwa angekosa nguvu katika bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania.
Mkapa katika kipindi chake cha utawala kwa muda wa miaka kumi alididimiza sana upinzani kwa sababu kuu mbili;
Moja, katika utawala wake alifanya vema katika kuimarisha uchumi na maisha ya watu yalionekana kuwa bora zaidi. Hii ilitokana na Mkapa kuungwa mkono zaidi na Mataifa ya nje na benki ya duni kiasi cha Tanzania kusamehewa madeni na kupokea misaada mingi ya maendeleo. Kuthitisha kukubalika kwake, uchaguzi wa mwaka 2000, Mkapa alipata kura zaidi kwa kushinda kwa asilimia 80 dhidi ya 60 aliyopata mwaka 1995.
Mbili, Mkapa alitumia ubabe sana katika kupambana na wapinzani wake na hivyo kuwatia hofu na kuwafanya washindwe kufanya siasa katika mzingira huru. Wengi wa Wapinzani kwa kipindi hicho waliogopa kuendelea na siasa nje ya ccm. Mfano mzuri wa watu amabao walipata uwoga na kuamua kurudi ndani ya ccm kwa uchache ni pamoja na Stevin Wassira, Amani Kabrou na wengine wengi amabo wako ndani ya chama cha mapinduzi. Katika kuhakikisha kuwa wapinzani hawawi changamoto katika uongozi wa Mkapa zipo tuhuma kwamba aliagiza vyombo vya usalama kuwaua wanachama wa CUF huko visiwani Pemba na hivyo kujenga hofu kwa baadhi way a wanamageuzi na wale walioona kuwa ndani ya upinzani hakuna uhuru wa kuendesha siasa.
Uchaguzi wa mwaka 2005 ulikuwa na changamoto kubwa kwa wapinzani kwa sababu watu wengi walikuwa na imani zaidi na ccm chini ya uongozi wa serikali ya mkapa. Mtandao uliojengwa na Rais wa sasa Mh .Jakaya kikwete na wapambe wake chini ya usimamizi wa Mh, Edward Lawassa ulikuwa mlima mkubwa kwa wapinzani kupenya na hasa baada ya CCM kuaminiwa zaidi kutokana na kazi nzuri iliyofanywa wa Mh, Mkapa na Waziri mkuu wake Fredrick Sumaye.
Katika uchaguzi ule wa 2005 Mgombea wa ccm Mh. Jakaya Kikwete alipata asilimia 80 ya kura zote dhidi ya vyama vingine. Kwa vyovyote ushindi huu ulichagizwa na utendaji mzuri uliosimamiwa na serikali ya ccm chini ya uongozi wa Mkapa na Sumaye. Mwaka 2010, ushindi wa ccm ulishuka kwa asilimia takribani 20 kwa Rais Jakaya M. Kikwete kupata asilimia 61 kati ya zaidi ya asilimia 80 aliyopata mwaka 2005. Hili lilikuwa anguko kubwa kwa kiongoziwa nchi kama Rais amabaye yuko madarakani na anazo kila nyenzo za kumsaidia kushinda. Kuanguka kwa kura za ushindi wa Rais katika mwaka wa 2010 kulielezwa na wachambuzi kwa mitazamo tofauti. Baadhi ya wachambuzi walisema kumetokana na utendaji dhaifu wa serikali ya Jakaya Kikwete, ufisadi wa serikali yake, watu kukata tama kutokana na muhemuko wa kauli ya “ Maisha bora kwa kila Mtanzania” ambayo haikuwa halisia na utendaji wa serikali kwani wananchi walijikuta katika hali mbaya kutokana na mdororo wa uchumi ulioathiri kipato cha wananchi na hivyo kujikuta wanaingia katika hali ya kupanda kwa gharama za huduma kama chakula, matibabu, usafiri, malazi na huduma nyingine zinazoakisi maisha ya mtanzania wa hali ya chini kabisa.
Jambo lingine lililochangia ni watu wengi kukata tamaa ya kupiga kura kwa sababu wanachagua viongozi amabo kimsingi hawawasaidii wananchi. Kila tunapofanya uchaguzi wa viongozi lengo ni kuwa na watu wenye uwezo wa kutoa hamasa ya maendeleo kwa kuelewa kero zao na kusaidia katika kupanga mikakati ya kukabili changamoto zinazowakabili wananchi kila siku katika mfumo wa maisha yao. Tanzania uchaguzi unaonekana kama fursa ya kuwapatia watu ulaji. Hii inatokana na ukweli kwamba viongozi wanapochaguliwa hawashughuliki na matatizo ya wananchi kwa viwango vinavyohitajika. Wapo ambao wakishachaguliwa hawarudi tena kutafuta matatizo ya wananchi na kusaidia ikiwa ni pamoja na kuonesha jitihada kwa kusaidiana na wananchi katika kukabilana na matatizo yao. Hii huwakatisha wanananchi tamaa ya kuendelea kuchagua kwa sababu hakuna mabadilko ya kimfumo yanayotokea baada ya uchaguzi kwa muda wa misimu yote minne waliyoshiriki katika uchaguzi.
Sababu nyingine kubwa inayofanya watu washindwe kushiriki kwa usahihi katika harakati za uchaguzi nchini Tanzania ni wananchi wengi kukosa elimu ya uraia. Katika elimu hii watu wanaweza kuelimishwa juu ya umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi na kwa maana ya wajibu wa raia na kiongozi baada ya kuchaguliwa. Ni bahati mbaya kuwa wale wanaopata fursa ya kusimamia elimu ya uraia wanafanya kila jitihada ya kuminya elimu kutolewa ili wananchi waendelee kuwa mbumbumbu na wasielewe majukumu na nafasi zao kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Hii imefanywa makusudi kwa sababu wanajua kuwa wananchi wakijua watawaadhibu kila mwaka wa uchaguzi kwa sababu wameshindwa kukidhi mahitaji na matarajio yao kama yalivyokuwa pindi wanaomba kuchaguliwa. Ni bahati mbaya sana kuwa sasa kwa upofu uleule viongozi wengi kutokana na utamu wa madaraka wamekuwa wakitumia rushwa kubwa ili kuwapumbaza wananchi na kuwachagua tena.
Ni vizuri kwa wadau wa demokrasia wakasaidia kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili wawe na uelewa wa kutosha juu ya uchaguzi. Tanzania uchaguzi umefanywa kama jambo lisilo na umuhimu na ndiyo maana wananchi hawajitokezi kwa nguvu juu ya kufanya maamuzi yao katika kuwaweka viongozi wanaowataka madarakani.
Mahitaji ya wananchi yamekuwa yakikwepeshwa na viongozi wao kwa njia mbalimbali na hasa kupitia miamvuli ya vyama na demokrasia butu. Kupitia vyama wananchi wanachagua viongozi wanaowekwa na wanachama kwa maslahi ya wananchama wenyewe. Kiongozi wa chama hawezi kuwa na maamuzi nje ya sera na mipango ya chama chake.
Ikitokea kiongozi akafanya maamuzi nje ya maslahi ya chama na wateule wake anachukuliwa hatua kwa mwamvuli wa chama. Haya yanaweza kuthibitishwa na kile kilichompata komandoo Abudul Jumbe akiwa Rais wa Zanzibar.
CCM wamekuwa bingwa wa kuua demokrasia na hasa kwa kuwafania umafia viongozi wa vyama vya upinzani wanaoonekana kama tishio kwa maslahi yao. Kinachofanywa sasa na ccm na wanachama wake dhidi ya Edward Lowassa na wanachama wengine walioamua kutafuta fursa walizominywa ndani ya ccm ni mkakati uleule wa watawala kwa mgongo wa chama tawala kuminya demokrasia na kutaka kwa nguvu kujibakisha madarakani. Kama watanzania hawatajitambua na kupambana na mfumo dola wa serikali ya chama cha mapinduzi katika sanduku la kura mustakhabari wa Tanzania bado uko mbali sana.
Naomba nitoe wito kwa vijana, wazee, akina mama wanachama wa vyama vyote kushiriki katika uchaguzi wa octoba 25, 2015 ili kusaidia mabadiliko ya kiuongozi na kimfumo katika uendeshaji wan chi yetu ya Tanzania.
Tupuuze siasa za majitaka zinazofanywa na wapenzi wa ccm juu ya mgombea wa CHADEMA na umoja wa katiba ya wananchi{ UKAWA} kwa makusudi ili kufifisha mabadilko yanayoonekana dhahiri katika nchi yetu. Mabadiliko yanayoimbwa na wanachi ni yale yanayolenga kuleta mfumo mpya wa utawla na uendeshaji wan chi yetu nje ya chama cha mapinduzi. Ni bahati mbaya sana kuwa wasomi wengi wanajadili hili wanashindwa kueleza mabadiliko hasa yanayotakiwa na wananchi kwa makusudi au kwa hofu ya kuonekana wanegemwa upande wanapofanya uchambuzi. Wapo pia wananchi wengi ambao hawahitaji mabadiliko yeyote kwa sababu wanaridhishwa na mfumo wa uendeshaji wan chi chini ya chama cha mapinduzi. Hili nalo ni muhimu likaelezwa bila ya kuogopa kwa sababu ndiyo ukweli.
Wananchi wa Tanzania na hasa walio wengi wanahitaji kuambiwa ukweli na hasa wanasiasa wanapowambia mambo ya uongo il wachaguliwe katika nyadhifa mbalimbali. Utaratibu wa wanasiasa kuwadanganya wananchi kila mwaka wa uchaguzi na wasomi wakaungana nao kwa maslahi binafsi haliwezi kusaisia Taifa hili kutoka hapa lilipofikia.
Ni vema kila mtu kwa nafasi na wakati alionao kufanya kile anachofikiri ni sahihi Katika kuwasaidia watanzania kuelewa wajibu na haki zao wakati na baada ya uchaguzi.
Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Afrika.
Makala hii kama itawapendeza wahariri yaweza kuchapishwa katika gazeti la Mawio na Jamhuri tu.
Mwalimu wa walimu.

Sumbawanga-Rukwa
 
Mwaka huu watu wana uelewa mkubwa wa uraia, sababu ya danganya toto za ccm. Wanasubiri kwa hamu kuchinja mfumo mbovu mapema asubuhi oct 25.
 
Mwaka huu watu wana uelewa mkubwa wa uraia, sababu ya danganya toto za ccm. Wanasubiri kwa hamu kuchinja mfumo mbovu mapema asubuhi oct 25.


Ni kweli watu wanelewa lakini bahati mbaya ni kwamba ccm inatumia kila hila iuli wakate tamaa na wasipige kura. Ndiyo maana kila kukicha wanapambana na wapinzani wao kwa kiala rasilimali zilizo chini ya usimamizi wake aghalabu kuhakikisha kwamba wanawavunja moyo baadhi wa wananchi.

Jambo lingine wananchi wa Tanzania bado hawana uelewa wa thamani ya kura yao na ndiyo maana wengine wanasombelewa kwenye malori kwa ajili eti kujaza uwanja wa mgombea na wamesahau kabisa matatizo yanayowakumba sasa hivi kutokana na serikali ya ccm kutoweka mifumo mizuri ya wananchi kuishi maisha mazuri kwa kuzingatia shughuli za kila mwananchi.
 
Back
Top Bottom