Ukana Shilungo
JF-Expert Member
- Apr 17, 2012
- 3,041
- 2,422
Wanajamji heshima kwenu! Mpaka sasa hatima ya CCM iko kwa candidate Benard Membe,ipo sababu kubwa ya kusema hilii.
- Membe hajawahi kutangaza nia ya Urais ila vyombo vya habari vinamtaja mno kuwa huenda akatangaza nia.kwa hiyo vinahiriki kumjenga pasipo kukusudia.
- Kila linapotajwa jina la Membe kuhusishwa na Urais,watu wanaweweseka kwa woga kumuhofia.hiyo ni dalili kuwa ni material candidate.
- Membe ni mwanadiplomasia aliyetukuka,na mwenye weledi mbaye amefanya kazi nje ya nchi kwa mda mrefu,kama taifa linahitaji mtu wa namna hiyo,mintarafu suala la uhusiano wa kimataifa.
- Membe alishinda ujumbe wa kamati kuu ccm Nec kupitia kundi la kifo ,Membe alishinda alishinda pasipo kuzunguka mikoani,mbali ya kampeni chafu za akina Hussein Bashe kumchafua.
- Membe ni mtu mwenye rekodi safi kwa maisha yake kisiasa.Hiyo inamfanya pia awe bora ukilinganisha na wengine wanaotamani urais.
- Kura za 2015 zinaenda kupigwa kwa misingi ya candidate ni nani na sio anatoka chama gani,ukitaka kuona hili angalia issue ya kuchomwa makanisa,mauji ya wachungaji hasa Zanzibar padre Mushi, kutaja machache,hivyo watu wanaenda kupiga kura kwa misingi hiyo .............malizia.
- Membe ni mtu anayeonekana kuaminika mbele ya mkulu,kwani mamvi akiingia darakani hatatabilika aweza kuyafanya ya aliyofabnyiwa Chiluba Zambia.
- Amewahi kumwakilisha Mkuu wa Nchi na akahutubia UN badala ya mkulu.
- Sasa hivi ni mtu wenye cheo kikubwa ndandi Jumuiya ya Madola,hivyo Moto wa Membe haukamatiki ndani nje ya nchi,baadhi ya watu hudiriki kumwita mnafiki,lakini hakuna hata mmoja aliyefaulu kueleza unafiki wake upo katika lipi. KWA HIYO MEMBE ENDAPO ATASIMAMISHWA NA CHAMA CHAKE 2015 INAWEZA KUWA NAFUU,KULIKO KUMSIMAMISHA laigwani,AMBAPO Chadema itaingia kirahisi. Nawasilisha, Ukana Shilungo.