CCM: Kiti cha Spika kimeinyima nafasi CCM!

Kishindo cha mikutano ya Wabunge sita wa CHADEMA waliosimamishwa na Naibu Spika,Job Ndugai, kwa uamuzi uliungwa mkono na Spika Anne Semamba Makinda,kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti kwa siku tano,kimeitikisa CCM. Inasemwa kwamba Kiti cha Spika kimewapa CHADEMA nafasi ya kufanya mikutano ya hadhara wasiyostahili na hivyo kuibana na kujibu mapigo ya mikutano ya Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abduralhman Kinana.

Inadaiwa kuwa Kiti cha Spika ni kama kilipanga kuendeleza mapambano ya kisiasa nje ya Bunge kwa kuwasimamisha Wabunge sita wa CHADEMA ambao wote ni wasemaji mahiri. Kimsingi,Kiti cha Spika sasa kinalaumiwa na CCM kwa kuwasimamisha Wabunge: Tundu Lissu,Joseph Mbilinyi,Mchungaji Peter Msigwa,Ezekiel Wenje,Highess Kiwia na Godbless Lema ambo sasa wanachanja mbuga mikoani kuwashtaki CCM na Serikali yao kwa wananchi.Tayari Wabunge hao,wakiongezewa nguvu na Mwenyekiti wao Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu Dr.Wilbrod Peter Slaa pamoja na viongozi wengine wa litaifa wa CHADEMA wameshafanya mikutano ya hadhara Mwanza,Dodoma na Iringa.

' Unamsimamisha Lissu,Lema na wenzao tena kwa siku tano unategemea nini?' aling'aka Waziri mmoja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. 'Muda huu wa Bunge la Bajeti ulikuwa muafaka kwetu(CCM) kufanya mikutano ya hadhara bila mawaa. Ndivyo ilivyopangwa na kukubaliwa na chama. Ndivyo afanyavyo Katibu Mkuu Kinana na Nape Nnauye. Sasa Kiti cha Spika kimeturudisha nyuma na kutuharibia mipango yetu' aliongeza.

Waziri mwingine ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa Kiti cha Spika kitashtakiwa kwenye vikao vya chama kwa kutoa nafasi kwa CHADEMA kujibu makombora ya CCM muda huu. ' Lazima tuwashtaki katika vikao. Laiti Wabunge hawa wangetingwa na vikao vya Bunge,wasingeweza kufanya kama wafanyavyo sasa. Hapa kuna harufu ya mpango maalum wa kuibeba CHADEMA. Bora hata Kiti cha Spika kiwaite haraka Wabunge hawa Bungeni ili kuwapunguza kasi' alisema Waziri huyo aliyeungwa mkono na Mawaziri wengine pamoja na Wabunge.

Ilikuwa ni katika Kikao kisicho rasmi cha kichama kilichofanyika hapa Dodoma baada ya kuwepo na uzushi kuwa eti CHADEMA imewachochea wananchi wa Liwale na wananchi hao wanajiandaa kuandamana na kufanya fujo.

Kizungumkuti kweli kweli!

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam ( sasa Dodoma)

Vuta Nkuvute:Bado unasimamia uamuzi wako wa kutoenda Arusha kwenye ule mnyukano wa kata nne za udiwani? (maana ile ya tano ya Kamanda mawazo Lumumba wamechakachua!) Unaweza kututonya nani atakuwa kiongozi wa kampeni huko? Waambie Lumumba huko watapigwa kipigo cha mbwa mwizi ni wazuri wakakubali matokeo, maana Kamanda Lema anahitaji wiki moja tu kuhamasisha watu wajitokeze kupiga kura(sio kupiga kampeni) ili kuiadhibu sawasawa CCM. Kama vipi unaweza kuja kucheck upepo A town unavumaje.
 
When they are totally defeated by poor minds, they discuss about CDM, you are poor heads, norrow thinking , you cant afford looking for your lost head any more.
 
Nape hawezi mlaumu spika manake wote nimpaka wapewe maelekezo thats why kampeni zake zakuwatoa mafisadi ndani ya cku 90 ziliyayuka cku zilipoanza.
 
Inawezekana kuna ka ukweli ndani yake. Hawa jamaa waliofikuzwa kwa sasa wamepewa uhuru wa kutangaza sera zao bila shinikizo la kuhudhuria vikao vya bunge na wana ujumbe ambao kila mwananchi angeoenda kusikia. Yaani inakuwaje mbunge ambaye amechaguliwa na maelfu ya wananchi anafukuzwa na spika kwa kisingizio cha busara za kiti na kanuni za kibabe. Kuna haja ya demokrasia ndani ya bunge kuangaliwa upya.
 
13.+Kinana+akikabidhi+Mbuzi+kwa+nahodha+wa+timu+ya+Libenenga,++Steven+Maundu.+Kulia+ni++bdallah+Mazengo+wa+Nkongo+FC+iliyofungwa+2-0+Kinana+Cup,+Ulanga.jpg

Hivi pembe za mbuzi nazo zinauzika? Nauliza tu!!!
Kwa nini huyo mbuzi focus yake iko kwa mtu mmoja tu hapo wakati wapo wengine chini ya jukwaa? No offense intended....just curious.
 
Kishindo cha mikutano ya Wabunge sita wa CHADEMA waliosimamishwa na Naibu Spika,Job Ndugai, kwa uamuzi uliungwa mkono na Spika Anne Semamba Makinda,kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti kwa siku tano,kimeitikisa CCM. Inasemwa kwamba Kiti cha Spika kimewapa CHADEMA nafasi ya kufanya mikutano ya hadhara wasiyostahili na hivyo kuibana na kujibu mapigo ya mikutano ya Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abduralhman Kinana.

Inadaiwa kuwa Kiti cha Spika ni kama kilipanga kuendeleza mapambano ya kisiasa nje ya Bunge kwa kuwasimamisha Wabunge sita wa CHADEMA ambao wote ni wasemaji mahiri. Kimsingi,Kiti cha Spika sasa kinalaumiwa na CCM kwa kuwasimamisha Wabunge: Tundu Lissu,Joseph Mbilinyi,Mchungaji Peter Msigwa,Ezekiel Wenje,Highess Kiwia na Godbless Lema ambo sasa wanachanja mbuga mikoani kuwashtaki CCM na Serikali yao kwa wananchi.Tayari Wabunge hao,wakiongezewa nguvu na Mwenyekiti wao Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu Dr.Wilbrod Peter Slaa pamoja na viongozi wengine wa litaifa wa CHADEMA wameshafanya mikutano ya hadhara Mwanza,Dodoma na Iringa.

' Unamsimamisha Lissu,Lema na wenzao tena kwa siku tano unategemea nini?' aling'aka Waziri mmoja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. 'Muda huu wa Bunge la Bajeti ulikuwa muafaka kwetu(CCM) kufanya mikutano ya hadhara bila mawaa. Ndivyo ilivyopangwa na kukubaliwa na chama. Ndivyo afanyavyo Katibu Mkuu Kinana na Nape Nnauye. Sasa Kiti cha Spika kimeturudisha nyuma na kutuharibia mipango yetu' aliongeza.

Waziri mwingine ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa Kiti cha Spika kitashtakiwa kwenye vikao vya chama kwa kutoa nafasi kwa CHADEMA kujibu makombora ya CCM muda huu. ' Lazima tuwashtaki katika vikao. Laiti Wabunge hawa wangetingwa na vikao vya Bunge,wasingeweza kufanya kama wafanyavyo sasa. Hapa kuna harufu ya mpango maalum wa kuibeba CHADEMA. Bora hata Kiti cha Spika kiwaite haraka Wabunge hawa Bungeni ili kuwapunguza kasi' alisema Waziri huyo aliyeungwa mkono na Mawaziri wengine pamoja na Wabunge.

Ilikuwa ni katika Kikao kisicho rasmi cha kichama kilichofanyika hapa Dodoma baada ya kuwepo na uzushi kuwa eti CHADEMA imewachochea wananchi wa Liwale na wananchi hao wanajiandaa kuandamana na kufanya fujo.

Kizungumkuti kweli kweli!

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam ( sasa Dodoma)

Waziri ambaye ni mbunge wa kuteiliwa ninayemjua ni Prof. Muhongo. Kweli CCM ni simu, Prof. Muhongo anaweza kulilia vikao vya chama kuficha UPUM.... wao. Kwa nini asisimame na kusema palepale bungeni kuwa kiti cha spika kimepwaya mpaka alilie vikao vya chama?
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.
Mie ni mmoja wa wachangiaji wa CHADEMA. Nafurahi sana kwa kazi nzuri inayofanywa na wabunge wa chama changu. Mwisho wa mwezi huu nitatuma tena donge kubwa kuliko yale yote niyoishatuma. Baada ya kufukuzwa, Wabunge wametetemesha magamba na kuzidi kuwanyima usingizi. Hakika wamefanya kazi nzuri na kubwa sana. Wanachadema na wapenzi na mashabiki wote wa CDM, Huu ndio wakati muafaka wa kukichangia zaidi chama!
 
Kwa Ndungai na mama Spika wameshaenda kuharibu pia?
inabidi wanapiga kura wao wajue uozo wa mama spika na mzee wa toka njeeeee
akidhani anamtimua paka,
hakujua makucha ya amfukuzae yangemdhuru mwenyewe
 
Back
Top Bottom