Moses Kyando
Member
- Mar 4, 2010
- 48
- 7
Inawezekana kabisa kwa sasa kila mtu akaona haya si mawazo sahihi kwa sababu ya kusikika kwa akina Magufuli, Lowasa na Mwandosya. Suala la Muungano wa nchi yetu ni tete sana kwa sasa na litaendelea kuwa tete kadiri tunavyousogelea mwaka 2015.
CCM kwa sababu ya kuwaondoa hawa wanaotajwa tajwa kama walivyomfanyia Sitta katika ngazi ya Uspika kwa kudai kwamba ilikuwa zamu ya wanawake licha ya kuwa si jambo la kikatiba, basi hata katika urais watatengeneza zamu ya Zanzibar bila kujali katiba bali vikao vya chama. Lengo la kufanya hivyo itakuwa kuwakata kilimilimi hawa wabara wanaoutamani urais lakini pia kujaribu kuuimarisha Muungano ambao miongoni mwa sababu za kuteteleka ni Wazanzibari kutopata Urais wa Muungano.
UVCCM yalifanyika kwa kumtoa Nape na kumpa Masauni na mifano mingine ipo. Bisheni leo lakini unabii huu utatimia