CCM inapo tapa tapa kusaka uungwaji mkono

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,881
Ni kweli kuwa vita vya panzi ni furaha ya kunguru.

Hata hivyo kwa mustakabala wetu wakiwamo watoto wa wajukuu zetu, tusiache mbachao kwa msala upitao.

Haina shaka kuwa nyongeza ya kwenye "boom" haina tofauti na punje ya mchele na punje ya almasi kwa jogoo.

Mengine haya ni yale yale:

Screenshot_20230212-205451.jpg

Tusiache kujiuliza kwani mpango mzuri kama huu uanzie wapi?

"Vijana watakapo hitimu au kwa wahitimu walioko mitaani tayari bila ajira?"

Inafahamika tutasikia mengi sana kwa kadri homa ya siasa itakavyoendelea kupanda.

Hata hivyo kama wenye akili zetu ni muhimu kuhoji.

Zaidi mno tutambue ndo ndo ndo si chururu.
 
Kuwa na mpango mzito kama huo, ingependeza Samia angeuzungumzia jana wakati akiongea na wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini jambo hilo kumuachia Msigwa ambaye tumeshamzoea kwa matamko yake ya kisanii ili kuitetea serikali sio wa kuaminika.

Tutasikia mengi bila shaka na kikokotoo ki njiani.
 
Huyu dogo alikuwa ana hustler pale songea JPM kamsaidia sana na sasa anajiona mjanja kasahau alikotoka. Ama kweli watanzania wakipata husahau shida zao bora tungekuwa hatumjui alikoanzia lkn maisha yake yote tunayajua kuanzia pale songea sekondari hadi redio maria mpaka aliposaidiwa na TIDO tunajua.
 
An Open Letter to President Dr. Samia Suluhu: Proposal for the Establishment of a High Education Graduates Bank (HEGB)

President Dr. Samia Suluhu,

I hope this letter finds you in good health and high spirits. I am writing to bring to your attention a critical issue that affects the future of our country, namely, the high rate of unemployment among high-education graduates. Despite their impressive qualifications, many of these individuals struggle to find employment due to the shortage of opportunities and access to capital.

In light of this challenge, I am proposing the establishment of a High Education Graduates Bank (HEGB). This bank will serve as a financial solution for high-education graduates who wish to start their own businesses but face difficulties in securing funding from conventional banks. The bank will provide loans to these entrepreneurs based on the feasibility and innovation of their business ideas, with funds generated from the contributions of all high-education students, who will contribute a small amount every semester.

By establishing this bank, we can encourage innovation and entrepreneurship among high-education graduates, and ultimately, reduce the unemployment rate in our country. The High Education Graduates Bank (HEGB) will not only provide financial support to high-education graduates but also foster a culture of self-employment and innovation, which are crucial to the continued growth and development of our nation.

I am confident that with your support, we can bring this proposal to life and make a significant impact on our country's future. I would be honored to discuss this proposal further and answer any questions you may have.

Thank you for your time and consideration.

Sincerely,
Bright and Genius Editors
Email: bandg.editors@gmail.com
Phone: 0747744895/0687746471/0612607426
 
Barua ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan; Pendekezo la Kuanzishwa kwa Benki ya Wahitimu wa Elimu ya Juu (HEGB).

Mpendwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan,

Ni imani yangu kuwa barua hii inakufikia ukiwa na afya njema na mwenye nguvu. Naandika barua hii kukujulisha juu ya jambo muhimu sana linaloweza kuleta athari chanya kwa taifa letu kuhusiana na wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana, hasa wale wanaohitimu elimu ya juu (vyuo). Pamoja na ufaulu mkubwa, bado vijana hao wamekuwa wakitaabika mno kupata ajira kutokana na uhaba wa fursa na ukosefu wa mitaji ya kuanzisha biashara mbalimbali.

Kutokana na changamoto hii, napendekeza kuundwa kwa Benki ya Wahitimu wa Elimu ya Juu (HEGB). Benki hii itakuwa suluhisho la kiuchumi kwa wahitimu wanaotamani kuanzisha biashara lakini wanapata wakati mgumu kupata mitaji kutoka katika benki mbalimbali hapa nchini. Benki hii itawawezesha wahitimu hao kuwa wajasiriamali kwa kuwanufaisha kwa mikopo inayolingana na ubunifu na ufanisi wa mawazo yao ya kibiashara. Benki hiyo itaendeshwa kutokana na michango watakayokuwa wakichangia wanafunzi wa elimu ya juu watakapokuwa masomoni kwa kila muhula.

Kutokana na kuundwa kwa benki hii, tunaweza kuchochea uvumbuzi na ujasiriamali miongoni mwa wahitimu wengi wanaomaliza elimu ya juu, na hivyo kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini. Sio tu kutoa mikopo, Benki hii pia italenga katika kueneza dhana ya kujiajiri na ubunifu, ambavyo ni muhimu katika ukuaji endelevu na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

Naamini sambamba na msaada wako tunaweza kulipa pendekezo hili uhai na kuleta mabadiliko makubwa katika taifa letu. Nitafurahia mjadala endelevu kuhusiana na swala hili na nitayajibu kwa furaha maswali yoyote unayoweza kuwa nayo kuhusiana na swala hili.

Nashukuru kwa muda wako.

Wako mtiifu,
Bright and Genius Editors
Barua pepe: bandg.editors@gmail.com
Namba za simu: 0747744895/0687746471/0612607426
 
Ni kweli kuwa vita vya panzi ni furaha ya kunguru.

Hata hivyo kwa mustakabala wetu wakiwamo watoto wa wajukuu zetu, tusiache mbachao kwa msala upitao.

Haina shaka kuwa nyongeza ya kwenye "boom" haina tofauti na punje ya mchele na punje ya almasi kwa jogoo.

Mengine haya ni yale yale:

View attachment 2515670

Tusiache kujiuliza kwani mpango mzuri kama huu uanzie wapi?

"Vijana watakapo hitimu au kwa wahitimu walioko mitaani tayari bila ajira?"

Inafahamika tutasikia mengi sana kwa kadri homa ya siasa itakavyoendelea kupanda.

Hata hivyo kama wenye akili zetu ni muhimu kuhoji.

Zaidi mno tutambue ndo ndo ndo si chururu.
WE ndio unatapatapa, serikali inapiga kazi kutimiza wajibu wake. Mmekosa cha kuwasema serikali mngetamani mpate cha kusema. Badilikeni badilini mbinu za kisiasa, CCM inajua sayansi ya siasa
 
WE ndio unatapatapa, serikali inapiga kazi kutimiza wajibu wake. Mmekosa cha kuwasema serikali mngetamani mpate cha kusema. Badilikeni badilini mbinu za kisiasa, CCM inajua sayansi ya siasa

Inataka sayansi hata kujua sababu za matukio. Kazi inayopigwa ni hii?

FoVixEVWAAAou0r.jpeg
 
Hapo pesa zitawafuata wenye pesa tu ila hakuna mlengwa hata mmoja atakayenufaika.
 
Ni kweli kuwa vita vya panzi ni furaha ya kunguru.

Hata hivyo kwa mustakabala wetu wakiwamo watoto wa wajukuu zetu, tusiache mbachao kwa msala upitao.

Haina shaka kuwa nyongeza ya kwenye "boom" haina tofauti na punje ya mchele na punje ya almasi kwa jogoo.

Mengine haya ni yale yale:

View attachment 2515670

Tusiache kujiuliza kwani mpango mzuri kama huu uanzie wapi?

"Vijana watakapo hitimu au kwa wahitimu walioko mitaani tayari bila ajira?"

Inafahamika tutasikia mengi sana kwa kadri homa ya siasa itakavyoendelea kupanda.

Hata hivyo kama wenye akili zetu ni muhimu kuhoji.

Zaidi mno tutambue ndo ndo ndo si chururu.
😅😅😅
 
Sasa ni wakati wa wasikilizaji kusikia kila sauti itokayo kila pembe. Kipindi kigumu saana kwa masikio yetu walahi. " MTAJI WA MASIKINI NGUVU ZAKE MWENYEWE, "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, ", VYOTE HIVI VIMEENDA WAPI?
Kilimo ni uti wa mgongo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom