CCM ina shauku sana tu ya kuachia madaraka, ila hakuna upinzani unaojitambua!

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Heri ya J3. CCM ina shauku mno ya kukabidhi madaraka tena kwa amani kwa upinzani,ila swali linakuja, je, wapinzani wanajitambua ipasavyo? Kwa upande wangu kama Mtanzania huru najibu NO!

Nchi hii tuna vyama kadhaa vya upinzani tukianzia na CDM, NCCR Mageuzi, ACT Wazalendo, CUF, CHAUMA n.k, ni suala lisilowezekana miongoni mwa vyama hivyo vyote kisiwepo hata kimoja cha kupewa madaraka na CCM.

CCM imepima na kuona vyama vyote vya upinzani ni puppets tu kama puppets wengine. Ni njaa njaa tu! Na mwenye njaa hana akili timamu.

Tuanze kwa CDM chama ambacho ndicho kinaitwa ni chama kikuu cha upinzani TZ, kama Mtanzania huru nimebaini:

1. Kama mtanzania huru, naona viongozi wengi wa CDM hawana msimamo unaoeleweka kiasi cha kukabidhiwa nchi na CCM. Sasa kama watu wanayumba yumba wataweza kuwaweka wananchi kwenye mstari kweli? Tupa kule!!!

2. Hawajajipanga kwenye kuwekeza kwenye rasilimali za chama kama majengo bora ya kisasa kila mkoa, kuanzia makao makuu ya CDM n.k! Kwa kweli makao makuu ya CDM ni kituko na hayana hadhi ya kuwa makao makuu ya chama kikuu cha upinzani nchini. Ni aibu! Ni njaa njaa tu na kama yeyote haamini aka google.

3. Baadhi ya viongozi wao wa juu hawana elimu za kueleweka ukimtoa Lissu, hii inafanya upinzani kwa TZ hasa CDM, uonekane kama kituko na kichekesho. Ukiwa loose kichwani huwezi kukiongoza chama kwenye ukamilifu wake.

4. CDM ni kama inapokea ruzuku ila inaishia kwenye mambo mengine badala ya kwenye vitu vya msingi kama majengo ya kueleweka.

5. CDM ina wanachama wengi wahuni wahuni ambao hawapigi kura kwa wingi wao, zaidi ya kushangilia hovyo hovyo kwenye mikutano ya kisiasa. CDM haina wanachama hai wa kueleweka.

6. CDM ina kashfa nyingi za ukanda kutoka kwa baadhi ya wanachama wake, hii itawagawa waTZ na kwa hivyo CDM inakosa sifa ya msingi ya kukabidhiwa madaraka. Ijifunze kwa CCM!

7. Hawana agenda za kueleweka za kusimamia endapo wakipewa madaraka na CCM. Hawajaeleza kipi tofuti watafanya ambacho CCM haifanyi, na watafanyaje? Wanakosa jibu hapa, hali inayofanya wananchi waamini kuwa hawa ni waganga njaa(upinzani njaa).

8. Umasikini uliopo CDM kuanzia kwa baadhi ya wanaharakati wake na mpaka kwenye rasilimali zake mfano majengo yasiyo bora(mapagale) n.k!
Wanaharakati wengi wa CDM siyo smart, hasa kichwani, waropokaji na laymen.


Hivyo basi, kwa hayo yote CCM haiwezi kuachia madaraka kwa upinzani nchi hii kwa sababu mkuu wa upinzani yaani CDM hana bado msuli wa kuhimili kupokea madaraka, na ikiendelea hivi upinzani utakufa Tz, ni suala la muda tu.

Wananchi siyo wapumbavu na hawadanganyiki ng'ooo!

Masikini anapewaje nchi na kwa nini yaani? Never!

CDM rekebisheni hayo though itawachukua muda mrefu sana. CCM wenzenu ni wajanja na wameahajichimbia. Nyie mnapiga mihayo.

CDM igeni mbinu na tactics smart za CCM vinginevyo chama kitakufa kifo cha mende.

Nini hasa bora na chenye tija kwa taifa kwa ujumla, mtafanya ambacho CCM haifanyi endapo mtapata nchi?
 
....Bullsh***!, Aliyeshinda Uraisi Nigeria alikuwa ameiandaa kipi Cha zaidi Kuipokea Nchi, ambacho CHADEMA ama ACT hawajiandaa???
 
Back
Top Bottom