CCM-Igunga

Salimia

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
665
103
Nani anafaa kuongoza kampeni za CCM Igunga kati ya January Makamba na Mwigulu Nchemba?
My take: January ni mtu makii na smart lakini ana damu ya kunguni ya kuchukiwa tu bila sababu za msingi hivyo si sahihi kwa chama kumpeleka Igunga. Mwigulu ni very smart na machachari na hana kashfa yoyote, anaweza kukisadia sana chama chake huko Igunga.
 
Mimi binafsi siamini kama JANUARY ni mwanasiasa makini. Hajawi kupata mihimili ya kisiasa. Namaanisha hakuwahi kusimama jukwaani kjiombea kura, Ubunge wake ni mlango wa nyuma (alipita bila kupingwa). hata kama angepita kwa kchaguliwa naamini hajaifahamu vizuri CCM, yuko hapo kwa mgogongo wa baba yake. Unapozungumzia anachma wa ccm wanaojua fitna za uchaguzi (ambazo tayari chadeam wanazifahamu) si mwiguru wa january wanaweza kuwemo kwenye lists. Ila nitafurahi wakipelekwa Igunga kwani ndio mwanzo wa sisi chedema kuanza kuongoza kura.
 
Nani anafaa kuongoza kampeni za CCM Igunga kati ya January Makamba na Mwigulu Nchemba?
My take: January ni mtu makii na smart lakini ana damu ya kunguni ya kuchukiwa tu bila sababu za msingi hivyo si sahihi kwa chama kumpeleka Igunga. Mwigulu ni very smart na machachari na hana kashfa yoyote, anaweza kukisadia sana chama chake huko Igunga.

sasa huyo si ndiyo yule mwizi wa pesa za BOT? Hapo hakuna wa kwenda kule zaidi ya yule jamaa anayecheka cheka, muda wote kukenua meno huku wananchi wake wamechanganyikiwa. yeye kucheka saa zote.
CCM watarajie kuwa chama cha upinzani Igunga
 
Hakuna hata anayefaa kuongoza kampeni. Wangeacha wenyewe watakuja,Peopleeeeeeeeeeeee Poweeerrrrrr!!!!
 
sasa huyo si ndiyo yule mwizi wa pesa za BOT? Hapo hakuna wa kwenda kule zaidi ya yule jamaa anayecheka cheka, muda wote kukenua meno huku wananchi wake wamechanganyikiwa. yeye kucheka saa zote.
CCM watarajie kuwa chama cha upinzani Igunga
acha fitna wewe! ukiambiwa uthibitishe hayo ya wizi utaweza? huyo kijana Mwigulu ndiye atabeba mikoba yote ya Igunga..........mtaniambia
 
Re : NEC-ROST KUVUA UBUNGE. Igunga wazawa wanahitaji muislam sasa ktk hao wawili muislam anatakiwa akawasikilize wazee wa pale Igunga ndio maana CUF imepamba moto na kinachoniogopesha hapa ni je ktk karne hii kuna element za udini kweli ?...ubaguzi ?...usisi na uwao ?
 
huyo swahiba wa Nape wamewapokonya tonge mdomo wazee wa igunga sidhani kama wanaweza kufanya upambavu huo, bado wana makovu anataka kuwa tonesha vidonda, wametembea nchi nzima wakihubiri siasa uchwara pamoja na Nape huyo Mwiguru.
 
hiyosafu sijaona wakuingia Igunga kwa kifupi Igunga inaenda upinzani haijalishim chama gani cha upiza kitasimika mgombea atapita tu
 
GAMBA KUU LA UFISADI CCM IGUNGA (GWIJI ROSTAM AZIZ) KIPEKEE LITABANDULIWA TU NA
MBUNGE WA PAMOJA TOKA KAMBI YA UPINZANI NCHINI!!

Mama yangu, mbona kwa CCM miti yote yateleza kiasi hiki kwa kila wakitendacho??

Ni vema ikaeleweka kwa kila mtu kwamba anguko la Gwinji wa Ufisadi nchini, Rostam Aziz, ni USHINDI kwa wanaharakati wooote ndani na nje ya nchi.

Hakika baada ya kuteseka sana na maisha magumu balaa ulisbabishwa na mafisadi wachache nchini, vijana hili ni FUNDISHO TOSHA kwetu kutokufanya ajizi Tabora.

Ni kweli kabisa kwamba WALAZWAHOI tunalo jukumu la kipekee kabisa la kutoweshwa kwake kabisa katika ramani ya siasa za nchi yetu ni jukumu la kila mmoja wetu ili kujihakikishia kwamba taifa letu Tanzania LINAZALIWA upya bila kuchukuliwa MATEKA tena wa huyu mtu, chama chake na au maslahi za nchi za nje anazoonekana kuziwakilisha katika nchi yetu.

Ndio, nasema kwamba ni jukumu la kila mpiga kura nchini, mpenda haki, mwanaharakati, mwandishi wa habari na akina kabwela tunaolazwa hoi na vituko vya huyu baba, kuhakikisha kwamba JUHUDI ZA KUNG'OA UFISADI NA MIZIZI YAKE YOTE ni sharti ianzie Igunga na kuenea kila kona ya taifa hili.

Kwa mshangao wa kila mmoja wetu jinsi ambavyo CCM kisivyokua na USO WA AIBU JUU YA UFISADI WA ROSTAM AZIZ bila kufikishwa katika mahakama yoyote nchini sasa tena waanza kupanga kupeleka MAKAPI na kulilazimisha kinywani mwao wananchi wa Igunga baada ya kuchukuliwa mateka kwa miaka mingi kwa nguvu za fedha za ufisadi.

Angalieni; mbali na Februari Makama kuwa ni miongoni mwa wabunge maarufu kwa DOSARI DONDA DUGU kuwahi kupitishwa kupitia MLANGO WA NYUMA na kisha KUJISHANGALIA MWENYEWE JINSI GANI ALIVYOWEZA KUTUA mjengoni Dodoma, hivi kweli WAADILIFU wote ndio hivo wameadimika ndani ya Chama hiki kiasi hicho kiasi cha CCM kuanza kuwazia kutuma JAMBAZi WA kule BoT, Mwigulu Nchemba, kwenda Igunga kuongoza safu ya kupatika MBUNGE WA WANANCHI atakayechukua nafasi ya aliyekua MBUNGE TX MWAKILISHI wa Maslahi ya Uajemi nchini ambaye pia anasadikiwa kuwa ni GAMBA KUU la Chama Cha Mapinduzi???????

Sasa ndugu zangu, kwa kuzingatia busara za usemi wa siku nyingi kati yetu kuwa 'Mtoto wa Nyoka ni Nyoka, je safu ya uchaguzi mdogo Igunga itakapongozwa ama na hili Jambazi letu la BoT ambaye bado kajinunulia fursa ya kuvinjari ovyo tu mitaani badala ya kule Keko au tusema kwamba itaongozwa na 'MBUNGE BLACK-MARKET' wa NEC kama ambavyo alivyo huyu dogo Februari Makamba; Watanzania TUTEGEMEE kuzaliwa kwa Mbunge wa aina gani Igunga??

Je, lengo letu kama taifa kulibandua Gamba Kuu la CCM, Rostam Aziz kwa kuweka Mbunge wa Wananchi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya kuchukuliwa MATEKA wa Uajemi utakua umekidhikika kweli hadi hapo???

Baada ya yote, kutokana na majumuisho ya hapo juu na mengine mengi watakayoandika wenzangu humu, sasa nadiriki kusema chonde waheshimiwa Dr Slaa, Mwana Anga wa ukweli Mhe Freeman Mbowe, Vijana wa ukweli Zitto Kabwe, Julius Mtatiro na John Mnyika, James Mbatia, Kamanda Gobless Lema (Katapila), Simba wa Vita Tundu Lissu, Mwenyekiti wetu BAVICHA, nawaombeni sana tena sana KUONYESHA MSHIKAMANO WA KI-UPIGANAJI kwa Maslahi yetu sisi Walazwa Hoi kwa kumpitisha Prof Ibrahim Haruna Lipumba kuchukua kiti hiki cha uwakilishi bungeni.

Kwa kusema ukweli ninayo imani kubwa sana kwamba hili linawezekana sana tu kwenu kama ambavyo na sisi Machalii Wapiga kura nchini tunavyoiombea dua hivi sasa.

sasa huyo si ndiyo yule mwizi wa pesa za BOT? Hapo hakuna wa kwenda kule zaidi ya yule jamaa anayecheka cheka, muda wote kukenua meno huku wananchi wake wamechanganyikiwa. yeye kucheka saa zote.
CCM watarajie kuwa chama cha upinzani Igunga
 
natoa shauri vyama vyote vya upinzani viungane na kupitisha mgombea mmoja tu na kisha nguvu yote itumike kuiadabisha CCM.Iwapo mpinzani atapita itawasumbua sana CCM kisaikolojia na hvyo upinzani kuendelea kupata ujasiri.come on wapinzani,onesheni kuwa umoja ni nguvu angalau mara hii tu.tofauti zenu mtazisort out baadae.nataman uchaguzi uwe kesho na ccm ibwagwe chini.aarrh!
 
Natumai kuna mtu katika kambi ya upinzani hapa jukwani hivi sasa na kwamba salam zetu hizi zinawafikia vema na wao kuwa n utayari wa kuyazingatia vilivyo!!!!!!!!

natoa shauri vyama vyote vya upinzani viungane na kupitisha mgombea mmoja tu na kisha nguvu yote itumike kuiadabisha CCM.Iwapo mpinzani atapita itawasumbua sana CCM kisaikolojia na hvyo upinzani kuendelea kupata ujasiri.come on wapinzani,onesheni kuwa umoja ni nguvu angalau mara hii tu.tofauti zenu mtazisort out baadae.nataman uchaguzi uwe kesho na ccm ibwagwe chini.aarrh!
 
Lipumba hagombei igunga, mgombea ni yule yule aliyepambana na Rostam, mh Leopard Mahana mbunge mtarajiwa wa igunga. tunavyo ongea hivi sasa yupo igunga na timu nzima ya cuf.
 
Nani anafaa kuongoza kampeni za CCM Igunga kati ya January Makamba na Mwigulu Nchemba?<br />
My take: January ni mtu makii na smart lakini ana damu ya kunguni ya kuchukiwa tu bila sababu za msingi hivyo si sahihi kwa chama kumpeleka Igunga. Mwigulu ni very smart na machachari na hana kashfa yoyote, anaweza kukisadia sana chama chake huko Igunga.
<br />
<br />
Unaleta mada then unijibu mwenyewe so una maana gani kama unajua huyo anafaa?
 
Hebu tupe kidogo dondoo za huyo mwenzetu Leopard Mahana hasa ndie nani na amewahi kuifanyia NINI Tanzania huko nyuma??

Lipumba hagombei igunga, mgombea ni yule yule aliyepambana na Rostam, mh Leopard Mahana mbunge mtarajiwa wa igunga. tunavyo ongea hivi sasa yupo igunga na timu nzima ya cuf.
 
mpelekeni Nape na wasanii wa bongo fleva

ni kweli mkuu, wakitaka kujaza watu kwenye mikutano wafanye hivyo - pia wasisahau kuwapa ulaji pia ze comedy kina Joti. Pia bado napata kigugumizi kujua ni nani msafi ndani ya CCM atakayeongoza mapambano ya kulikomboa jimbo? CCM ina kazi kubwa sana kwa sasa kwenye ukweli lazima tuseme.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom