CCM:DOWANS ni suala dogo saaaaanaaaaaa!!!

VUVUZELA

JF-Expert Member
Jun 19, 2010
3,103
786
Saturday, 29 January 2011 08:33
0diggsdigg
Elias Msuya na Fredy Azzah
KIKIWA kinatimiza miaka 34 tangu kuzaliwa kwake Februari 5, 1977, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelezewa kuwa, ingawa kimeendelea kushinda nafasi ya urais nchini, kinakabiliwa na wakati mgumu.

Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, wabunge wa CCM walisema chama hicho hakiwezi kufa kwa sasa, lakini kinapitia tu wakati mgumu kama ilivyo kwa vyama vingine duniani.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, alisema kwa kipindi cha miaka 34 ambacho CCM imekuwa madarakani, kimefanikiwa kufikia malengo yake hasa kwa kushinda chaguzi zote.


“Chama chochote kile duniani, malengo yake ni kushika dola. Kwa kipindi chote CCM tumefanikiwa kushika dola. Hata kwenye michezo, kama timu inashuka daraja mwenye timu huivunja,” alisema Lukuvi.

“Chama cha siasa ni taasisi endelevu, sio kwamba tumeongoza kwa maziwa na asali. Tunapitia kwenye milima, misitu na vichaka.

Ni jukumu letu kujitambua ili tuendelee kushika dola,” alisema. Kuhusu suala la Dowans ambalo limeonekana kukigawa chama hicho kabla ya wabunge wake kukutana na kuweka msimamo wa pamoja, Lukuvi alisema hilo haliwezi kukigawa chama.“Chama hakiwezi kugawanyika kwa ‘petty issues’ (mambo madogo madogo).

Chama kupitia mwenyekiti wetu alishasema jambo hilo sio kubwa. Ni uhuru wa maoni tu, kama ni mawaziri kupingana watakuwa wamevunja kanuni zao, sio chama,” alisema.

Naye Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib, alisema sio kwamba CCM imepoteza mwelekeo, bali kinakwenda kulingana wakati ulivyo.

“Sioni kama chama kimepoteza mwelekeo, kinakwenda kulingana na wakati, dunia imebadilika, mahitaji yameongezeka, vionjo vimeongezeka kwa hiyo chama kinakumbana na mazingira ya wakati huu,” alisema. Alikitetea chama hicho kuwa, hakiwezi kuleta pepo duniani na kwamba, matatizo yapo duniani kote sio Tanzania pekee.

Kuhusu suala la Dowans, Khatibu alisema kilichotokea ni uhuru wa maoni sio kugawanyika kwa chama. Naye Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Stella Manyanya, alisema kwa kipindi cha miaka 34, chama hicho kimefanya mambo mengi mazuri ambayo yameifikisha nchi hapa ilipo, na bado kina uwezo wa kuongoza miaka mingi ijayo.

Hata hivyo, Manyanya alisema changamoto anayaoiona ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi, ni suala la mawasiliano.

Source:Mwananchi 01/29/2011
 
Billioni 94 kwao ni ndogo kwa sababu wamezoea kumega pakubwa
Ivi hajui kuwa izo ela zinaweza jenga rami na shule za maana jimbo lake lote uko pawaga,isimani
 
mr lukuvi na wanaccm waelewe kuwa hata Mubaraka alikuwa na imani hiyo kama yao kuwa wamefanya mambo mengi mazuri na huu ni wakati ama mapito tu,
mtambue kuwa wananchi wanakiangalia chama na serikali yake kwa sura tofauti sana,najuwa mmesema hivyo kwa kuwa mpo madarakani na hamtawezasema ukweli juu ya mambo magumu yanayosumbuwa nchi hiii

pale wanacnhi watakapoitowa serikali kwa kutumia nguvu ya umma kama sehemu nyingine ndipo mtakapotambuwa kuwa sasa mmechokwa
tunawaomba msome alama za nyakati la sivyo mtadhani kuwa MMEJIFICHA KTK SHAMBA LA KARANGA HAMUONEKANI TUNAWAONA SANAAA na mwisho wenu waja

HIVI HAMUONI? NA HATA MSIKIIII? HII NI HATARI SANAAAA


MAPINDUZIIII DAIMAAAA:A S 20::coffee:
 
CCM bwana wanafurahisha wakati mwingine,sijui matatizo wanamficha nani kwani haihitaji shahada kutambua wanawakati mgumu na wanaelekea ukingoni.Tusubiri tuone hii tabia ya kuficha ficha matatizo itafika wapi.
 
Unapo kuwa kufani hutangulia ubongo kufa, mdomo hubwabwaja' masikio huziba pia huweza kufa kinywa wazi na kukodoa macho than hutaona hata maandalizi ya msiba!
 
Unapo kuwa kufani hutangulia ubongo kufa, mdomo hubwabwaja' masikio huziba pia huweza kufa kinywa wazi na kukodoa macho than hutaona hata maandalizi ya msiba!

sikio la kufa
 
CCM hawako serious. Kama ni kitu kidogo waendelee kuilipa mpaka mwisho ndio watajua
 
Back
Top Bottom