CCM: Dk. Slaa na wenzake wadandia kinguvu mazishi ya Mwangosi, Mbeya

Watanzania tumeishahamishwa kutoka kwenye focus.Hivi kila kitu ni siasa, hata uhai wa binadamu ni siasa? Ukiwa mwanachama wa CCM ukalaani waliomuua Daud Mwangosi utaonekana wa maana, otherwise utakuwa mnafiki wa kutupwa.
 
"Tulianza kukwaruzana tangu hatujaondoka mjini Iringa, kwani wakati tunatangaza taratibu za kusafiri, nilitumiwa ujumbe na viongozi wa CHADEMA, kuwa nitangaze msafara huo utaongozwa na Dk.Slaa, lakini niliwakatalia kuwa huo siyo msiba wa mwanasiasa bali ni mwanahabari hivyo hilo halitawezekana" alisema Godwin.

Godwin alisema aliwaeleza wazi viongozi wa CHADEMA, kuwa kama wanataka kwenda kushiriki mazishi hayo basi ni vyema watafute taratibu nyingine za kufika wilayani Rungwe, lakini siyo kung'ang'ania waongozane na mwili wa marehemu, kitu kilichowakera viongozi hao.

Aliongeza kuwa walishangazwa walipofika Tukuyu mjini, kundi la vijana wafuasi wa CHADEMA walilifuata gari walilokuwemo waandishi wa habari kutoka mkoa wa Iringa ambamo ndipo mwili wa marehemu Mwangosi ulikuwemo na kuamua kuingia kinguvu.
.......


Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati wa mazishi, Dk.Slaa alimfuata Godwin na kumueleza kuwa amemsamehe kwa yote aliyoyafanya....
Kuna issue hapo...
 
Ama kweli common sense is sometimes not common mwandishi amefariki mikononi mwa polisi akiwa kwenye tukio linalohusu CDM na bado mtu haoni logic ya Slaa kuwapo apo.
Ivi jamani kama upeo wetu finyu yaani ata utu hatuna?
Ndugu yangu Godwin ulitumwa na CCM kufanikisha ilo au walikuahidi ela ya sanda huwezi kuwa selective on nani wa kwenda kumzika mtu
 
Mbona kama ndugu wa rehemu walikuwa hawataki uwepo wa kiongozi yeyote wa cdm mbona kuhusu kusomesha mtoto hawajapinga?


Kweli ccm wanatapa tapa na Dr asinge kwenda wangesema wametelekeza msiba!

umeona eee!
 
Huu ni ujinga kusema eti msiba unadandiwa! Msiba hauna ukaribisho hapa kwetu labda kama mnataka kuanzisha utamaduni wa Ulaya!!!!!!! Magamba na polisi wenu ndio waliokuwa na silaha. La sivyo onyesheni silaha wazizokuwa nazo wana CDM kwenye hili tukio. Acheni ghilba na kuwahadaa wananchi leteni vielelezo halisia hadharani jinsi CDM walivyohusika mpakawazuiwe kujumuika kwenye huu msiba mkuuuu.
 
Pro-Chadema kila siku mnapiga kelele kuwa JK anapenda kwenda kujipendekeza kwenye misiba, vipi tena Dr Slaa anavamiia msiba wa watu au marehemu alikuwa kada wa Chadema...RIP Mwangosi.
Nilijua kuwa hutavumilia kuficha ujinga na upumbavu wako! tangu lini msiba ukamilikiwa? nani alikuwa anagawa kadi za mwaliko? Hivi wewe mjinga ni lini utajifunza kufikiri?
 
Wanataka wahudhurie ili waonekane watetezi wa wananchi kumbe ndio wanaosababisha vifo hivyo kwa kulazimisha mikutano. Leo channel 10 nimeona live habari ya slaa kwamba watahakikisha nchi haitawaliki. Ni dhahiri yanayojitokeza ni mwendelezo wa kutaka nchi isitawalike. Kaeni mkijua watanzania tunapenda amani, ni bora ulalie uji kwenye amani kuliko kula soseji kwenye. Ewe Mwenyezimungu tuepiushe na balaa la wana CDM.
Nina mashaka sana na uwezo wako wa akili. Nakushauri badala ya kumuomba huyo kwenye red kukupisha na balaa, ungemuomba akuongezee kaupeo japo kidogo ka kukaa na kuchambua mambo kwa busara! maana kwa hakika wewe ni mtupu kabisa huko kichwani!
 
Wanataka wahudhurie ili waonekane watetezi wa wananchi kumbe ndio wanaosababisha vifo hivyo kwa kulazimisha mikutano. Leo channel 10 nimeona live habari ya slaa kwamba watahakikisha nchi haitawaliki. Ni dhahiri yanayojitokeza ni mwendelezo wa kutaka nchi isitawalike. Kaeni mkijua watanzania tunapenda amani, ni bora ulalie uji kwenye amani kuliko kula soseji kwenye. Ewe Mwenyezimungu tuepiushe na balaa la wana CDM.

MKUNGA Usikubali kuona mambo kwa mtazamo mmoja tu. Jitahidi kupambanua mambo kuwa CDM si mbaya kama unavyodhani wala CCM si nzuri kama unavyodhani. Tanzania ni nchi yetu wote. Tujifunze kukubaliana kutofautiana kiitikadi lakini si sababu ya kujenga uadui na kuamini mia kwa mia kinachosemwa na upande mmoja.
 
Jamani, kwani kwenye mazishi ya Mwangosi kulikuwa na kadi za mwaliko wandugu?? Nashindwa kuelewa maana ya "kudandia kinguvu mazishi"
 
Pro-Chadema kila siku mnapiga kelele kuwa JK anapenda kwenda kujipendekeza kwenye misiba, vipi tena Dr Slaa anavamiia msiba wa watu au marehemu alikuwa kada wa Chadema...RIP Mwangosi.

wee akili yako hata mwenyewe una mashaka nayo, haikutoshi kabisa. Hivi huoni uhusiano kati ya msiba huo na CDM?
 
Na muomba mwenyezi mungu akupe uwezo wa kufikiri kwa kina.

Wanataka wahudhurie ili waonekane watetezi wa wananchi kumbe ndio wanaosababisha vifo hivyo kwa kulazimisha mikutano. Leo channel 10 nimeona live habari ya slaa kwamba watahakikisha nchi haitawaliki. Ni dhahiri yanayojitokeza ni mwendelezo wa kutaka nchi isitawalike. Kaeni mkijua watanzania tunapenda amani, ni bora ulalie uji kwenye amani kuliko kula soseji kwenye. Ewe Mwenyezimungu tuepiushe na balaa la wana CDM.
 
(nimeikuta huko lakini ina ukweli?) ukifika chini bofya
NEWZZ:DR.SLAA ALIVAMIA MSIBANI,AKAIDI AGIZO LA WENYE MSIBA




VIONGOZI wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa, wametuhumiwa kulazimisha kinguvu, kushiriki mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten, mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.

Marehemu Mwangosi aliyefariki katika vurugu, zilizobababishwa na CHADEMA eneo la Nyororo, alizikwa Jumanne ya wiki hii, katika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe huku kundi kubwa la wafuasi wa CHADEMA, likihudhuria mazishi hayo.

Inaelezwa licha ya kuambiwa msiba huo siyo wa kisiasa, hivyo hawatakiwi viongozi hao wala wanachama wa CHADEMA, lakini walilazimisha kushiriki kwa nguvu, na hata mwili wa marehemu ulipowasili Tukuyu mjini ukitokea mkoani Iringa, walilazimisha kuingia kinguvu kwenye gari hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, Francis Godwin, alisema kuwa tangu wakiwa mjini Iringa, aliwatangazia wazi CHADEMA kuwa msiba huo unawahusu waandishi wa habari na siyo wanasiasa.

“Tulianza kukwaruzana tangu hatujaondoka mjini Iringa, kwani wakati tunatangaza taratibu za kusafiri, nilitumiwa ujumbe na viongozi wa CHADEMA, kuwa nitangaze msafara huo utaongozwa na Dk.Slaa, lakini niliwakatalia kuwa huo siyo msiba wa mwanasiasa bali ni mwanahabari hivyo hilo halitawezekana” alisema Godwin.

Godwin alisema aliwaeleza wazi viongozi wa CHADEMA, kuwa kama wanataka kwenda kushiriki mazishi hayo basi ni vyema watafute taratibu nyingine za kufika wilayani Rungwe, lakini siyo kung’ang’ania waongozane na mwili wa marehemu, kitu kilichowakera viongozi hao.

Aliongeza kuwa walishangazwa walipofika Tukuyu mjini, kundi la vijana wafuasi wa CHADEMA walilifuata gari walilokuwemo waandishi wa habari kutoka mkoa wa Iringa ambamo ndipo mwili wa marehemu Mwangosi ulikuwemo na kuamua kuingia kinguvu.

Kwa mujibu wa Godwin, walipojaribu kuwakataza vijana hao wa CHADEMA, iwapo kuna mtu atawakatalia kuingia basi watambue wazi kuwa damu itamwagika hali iliyowafanya washindwe kuwazuia kwa kuogopa kuanzisha vurugu zisizo na msingi.

Aidha, katika kuonyesha kukerwa na hali hiyo iliyojitokeza, akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe, Godwin alisema hakuwahi kusikia marehemu Mwangosi akisema kuwa yeye ni mwanachama ama mfuasi wa chama chochote cha siasa.

Godwin alisema:”Ninachokifahamu mimi ni kuwa marehemu Mwangosi, alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, hivyo hatutegemei msiba huu kuanza kuingizwa itikadi za kisiasa”.

Aliongeza kwa kulitaka Jeshi la polisi kuwa hata kama marehemu Mwangosi, alifanya kosa lililopelekea akutwe na mauti hayo alipaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na siyo kufa aina ya kifo hicho cha kufa kwa bomu la machozi.

Katika kuonyesha kuwa kauli hizo ziliwachoma CHADEMA, Dk.Slaa aliposimama kuzungumza na wananchi, alisema anachofahamu yeye ni kuwa msiba hauna rangi, kabila wala dini.

Dk.Slaa aliongeza hivyo anapenda kutumia nafasi hiyo kukemea kauli za ubaguzi zilizotolewa, kwani CHADEMA wameenda kushiriki msiba huo kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na marehemu.

“Wakati tunaondoka mkoani Iringa kuja huku Rungwe-Mbeya, kuna kitu kilitokea ambacho kilitukwaza na sitapendi kukizungumza hapa…nimemjua marehemu Mwangosi alikuwa mtu wa haki na alikuwa akipinga vitendo vya kifisadi” alisema Dk.Slaa.

Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati wa mazishi, Dk.Slaa alimfuata Godwin na kumueleza kuwa amemsamehe kwa yote aliyoyafanya hali ambayo ilimlazimu naye (Godwin), kumjibu kuwa hajafanya kosa lolote linalostahili asamehewe.

chanzo:habari mpasuko blog


Blogu ya Wananchi: NEWZZ:DR.SLAA ALIVAMIA MSIBANI,AKAIDI AGIZO LA WENYE MSIBA


Nafikiri Chanzo cha habari kilipo ndo tatizo"http:// williammalecela.blogspot.com "
 
CDM wakiacha kushiriki wanasema wamewatelekeza, wakishiriki wanasema wamedandia. Sasa wewe Godwin umeshiriki kama nani? tangu lini msiba unapotokea kuna kualikana? Kama marehemu aliuawa wakati anafuatilia habari za CDM, utawaambiaje kuwa CDM wasishiriki?

mkuu, na wewe unaamini kwamba Godwin kasema hayo maneno?

CCM ipo mwaka 1978 na inafanya mambo ya mwaka huo wakati watu wapo 2012 with a vision ya 2035.

Kwao wao, kifo cha mwananchi ni nafasi ya kupata cha kuongea. Value ya raia kwao ni sawa na value ya mjusi kafiri.
 
Francis Godwin ulitakiwa kuungana na familia na wengine kuiombea familia inayopita ktk kipindi kigumu na siyo kuanzisha mijadala isiyo na tija yeyote. Tunza heshima ya rafiki yako na umuache apumzike kwa amani na kama kweli wewe ulikuwa rafiki wake wa kweli ilibidi uwe unaendelea kuifariji familia badala ya kuanza mijadala ya kijinga.
 
...Misiba ya Dar kamuachia DHAIFU akachangamkie UBWABWA.

Huwezi kuusafiria msiba ambao una uhusiano nao kama Dr Slaa anapenda kuzika mbona Dar kuna misiba mingi kaicha kaenda huko mbali.
 
Tayari Msiba wa Mwangosi umekuwa biashara hivi Godwin Francis ni mwanafamilia mpaka azuie watu fulani kumzika au kaambiwa atapewa ukuu wa wilaya akifuata maagizo ya polisi mjinga sana huyo kijana kama anadhani anaweza akachukua nafasi ya familia watoto na mke kupanga watu wa kuwahani
Huyo mdudu anayeiwa Godwin Francis si mwanafamilia na labda hafahamu kwamba Marehemu alikuwa mwanachama wa CHADEMA. Sasa kwa nini marehemu anyimwe haki ya kuzikwa na viongozi wa jumuia aliyoipenda (CHADEMA) na kuifia akipambana kama mpiganaji wa mstari wa mbele na manyang'au hawa? Mbona hakukataza azikwe kwa imani ya Kikristu?
Kwangu mimi ilikuwa sahihi kwake kuzikwa kwa imani na mapenzi ya enzi za uhai wake, kufanya kinyume cha vile ingekuwa kutomtendea haki. CCM ndiyo waliotaka kudandia maana hakuwa mfuasi wala mwanachama wao na wana damu yake mikononi mwao (Kwa vile aliuwawa kwa maelekezo yao) dami ile itawasakama hadi kusambaratika kwao. Wanajaribu kujikosha kwa kuupindisha ukweli.
 
Toka nizaliwe hii ni mara ya kwanza nasikia mfiwa akisema 'bwana huu ni msiba wetu, usije!'..ni dhahiri hata kama hili lingekuwa jambo la kawaida, Godwin hana mamlaka ya kuzuia yeyote kujihudhurisha kwenye msiba huu kwani yeye si ndugu wa marehemu.
 
Kwa amabye hamfahamu Francis Godwin atashangaa. Huyo ni mnafiki wa kisiasa namba moja. Kipindi cha uchaguzi 2010 akinogewa na bahasha za CCM alikuwa akiwashambulia CHADEMA pasipo sababu za msingi.

Wapi uliona watu wanaambiwa msiongozane na msafara wa msiba? Wanasiasa wataachaje kujumuika kwenye msiba uliotokea katika shughuli za kisiasa.

Hao ndiyo waandishi tulio nao. Waandishi wanaotokana na kufeli kidato cha nne msiwategemee kuwa na mantiki yoyote.

Njaa inawasumbua. Ndiyo maana hata makubaliano yao ya kutoripoti habari za polisi, wamegeukana.
 
Back
Top Bottom