CCM: Dk. Slaa na wenzake wadandia kinguvu mazishi ya Mwangosi, Mbeya

Kweli mkuu, hata mimi sijawahi kuona kadi za mwaliko wa msiba. Huyu Godwin naye anajivunjia heshima, kama anayo lakini.

Heshima yenyewe si mpaka awe nayo!!!hiyo adabu tu hana, ndiyo maana anabanagua watu wa kuhudhuria
msiba.
 
Ni huyu Huyu G aliyetuletea taarifa eti alitaka kuuwawa heri yeye ndiye angekufa mnafiki mkubwa huyu(samahani kwa kuongea haya)
 
[h=3](nimeikuta huko lakini ina ukweli?) ukifika chini bofya
NEWZZ:DR.SLAA ALIVAMIA MSIBANI,AKAIDI AGIZO LA WENYE MSIBA[/h]

VIONGOZI wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa, wametuhumiwa kulazimisha kinguvu, kushiriki mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten, mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.

Marehemu Mwangosi aliyefariki katika vurugu, zilizobababishwa na CHADEMA eneo la Nyororo, alizikwa Jumanne ya wiki hii, katika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe huku kundi kubwa la wafuasi wa CHADEMA, likihudhuria mazishi hayo.

Inaelezwa licha ya kuambiwa msiba huo siyo wa kisiasa, hivyo hawatakiwi viongozi hao wala wanachama wa CHADEMA, lakini walilazimisha kushiriki kwa nguvu, na hata mwili wa marehemu ulipowasili Tukuyu mjini ukitokea mkoani Iringa, walilazimisha kuingia kinguvu kwenye gari hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, Francis Godwin, alisema kuwa tangu wakiwa mjini Iringa, aliwatangazia wazi CHADEMA kuwa msiba huo unawahusu waandishi wa habari na siyo wanasiasa.

“Tulianza kukwaruzana tangu hatujaondoka mjini Iringa, kwani wakati tunatangaza taratibu za kusafiri, nilitumiwa ujumbe na viongozi wa CHADEMA, kuwa nitangaze msafara huo utaongozwa na Dk.Slaa, lakini niliwakatalia kuwa huo siyo msiba wa mwanasiasa bali ni mwanahabari hivyo hilo halitawezekana” alisema Godwin.

Godwin alisema aliwaeleza wazi viongozi wa CHADEMA, kuwa kama wanataka kwenda kushiriki mazishi hayo basi ni vyema watafute taratibu nyingine za kufika wilayani Rungwe, lakini siyo kung’ang’ania waongozane na mwili wa marehemu, kitu kilichowakera viongozi hao.

Aliongeza kuwa walishangazwa walipofika Tukuyu mjini, kundi la vijana wafuasi wa CHADEMA walilifuata gari walilokuwemo waandishi wa habari kutoka mkoa wa Iringa ambamo ndipo mwili wa marehemu Mwangosi ulikuwemo na kuamua kuingia kinguvu.

Kwa mujibu wa Godwin, walipojaribu kuwakataza vijana hao wa CHADEMA, iwapo kuna mtu atawakatalia kuingia basi watambue wazi kuwa damu itamwagika hali iliyowafanya washindwe kuwazuia kwa kuogopa kuanzisha vurugu zisizo na msingi.

Aidha, katika kuonyesha kukerwa na hali hiyo iliyojitokeza, akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe, Godwin alisema hakuwahi kusikia marehemu Mwangosi akisema kuwa yeye ni mwanachama ama mfuasi wa chama chochote cha siasa.

Godwin alisema:”Ninachokifahamu mimi ni kuwa marehemu Mwangosi, alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, hivyo hatutegemei msiba huu kuanza kuingizwa itikadi za kisiasa”.

Aliongeza kwa kulitaka Jeshi la polisi kuwa hata kama marehemu Mwangosi, alifanya kosa lililopelekea akutwe na mauti hayo alipaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na siyo kufa aina ya kifo hicho cha kufa kwa bomu la machozi.

Katika kuonyesha kuwa kauli hizo ziliwachoma CHADEMA, Dk.Slaa aliposimama kuzungumza na wananchi, alisema anachofahamu yeye ni kuwa msiba hauna rangi, kabila wala dini.

Dk.Slaa aliongeza hivyo anapenda kutumia nafasi hiyo kukemea kauli za ubaguzi zilizotolewa, kwani CHADEMA wameenda kushiriki msiba huo kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na marehemu.

“Wakati tunaondoka mkoani Iringa kuja huku Rungwe-Mbeya, kuna kitu kilitokea ambacho kilitukwaza na sitapendi kukizungumza hapa…nimemjua marehemu Mwangosi alikuwa mtu wa haki na alikuwa akipinga vitendo vya kifisadi” alisema Dk.Slaa.

Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati wa mazishi, Dk.Slaa alimfuata Godwin na kumueleza kuwa amemsamehe kwa yote aliyoyafanya hali ambayo ilimlazimu naye (Godwin), kumjibu kuwa hajafanya kosa lolote linalostahili asamehewe.

chanzo:habari mpasuko blog

Blogu ya Wananchi: NEWZZ:DR.SLAA ALIVAMIA MSIBANI,AKAIDI AGIZO LA WENYE MSIBA

Hoja dhaifu
 
Huwezi kuusafiria msiba ambao una uhusiano nao kama Dr Slaa anapenda kuzika mbona Dar kuna misiba mingi kaicha kaenda huko mbali.

Ningetegemea huyu Godwin kuwakataza CHADEMA kuuchukua mwili wa Mwangosi eneo la tukio baada ya kutelekezwa na Polisi. Yeye Godwin ndo anadandia mambo. Kama mtu amefia nyumbani au ofisini kwako kuna tatizo gani ukabeba mojawapo ya majukumu makubwa katika kufanikisha mazishi? Dr. Slaa hajavamia bali amewajibika na ndivyo alivyotakiwa afanye.
 
Tayari Msiba wa Mwangosi umekuwa biashara hivi Godwin Francis ni mwanafamilia mpaka azuie watu fulani kumzika au kaambiwa atapewa ukuu wa wilaya akifuata maagizo ya polisi mjinga sana huyo kijana kama anadhani anaweza akachukua nafasi ya familia watoto na mke kupanga watu wa kuwahani

Hili jamaa jinga sana na ni lilamba viatu na liosha kinywa la magambaz!
 
Msiba siyo wa chadema ni wawanahabari.mwanahabari kauawa kwenye mkutano wa cdm ambao siyo wawana habari.wana habari walikwenda kufanya nini kwenye mkutano usiyo kuwa wao?.kile kilicho wafanya wanahabari wakaenda kwenye mkutano usiyo wahusu ndiyo kilicho wafanya chadema kwenda kwenye msiba tena hata zaidi ya wanahabari wenyenyewe.kwa sababu msibaumetokea kwenye himaya yao ni kama wao.
 
Hapa tena siasa, jamani! nafikiri mhusika aliogopa kuwa kama chadema wangeshiriki basi utawala na ccm wangeowahusisha waandishi na cdm. hii ni hofu ya kawaida. lakini kutoshiriki kwa cdm kungetafsiriwa negatively na kuipunguzia cdm credibilty. Watanzania ni watu wanaojali sana misiba na katika hili hata huko mitaani hakuna ubaguzi. sasa unadhani cdm wangeendele na mikutano au wakalele wakati tukio lilitokea ndani ya nyumba yao? ACHA HIZO!
 
watupe taarifa ya utekelezaji wa sera ya kujivua gamba, waache kupotosha ukweli ulio wazi katika picha na video
 
Ningetegemea huyu Godwin kuwakataza CHADEMA kuuchukua mwili wa Mwangosi eneo la tukio baada ya kutelekezwa na Polisi. Yeye Godwin ndo anadandia mambo. Kama mtu amefia nyumbani au ofisini kwako kuna tatizo gani ukabeba mojawapo ya majukumu makubwa katika kufanikisha mazishi? Dr. Slaa hajavamia bali amewajibika na ndivyo alivyotakiwa afanye.

Mkuu wala usiumize kichwa ukisoma vizuri hii habari utagundua ina walakini mfano:
1. Wanasiasa wanaosemekana walizuiwa ni wa CDM pekee? Mbona Mwandosya na wapambe wake walikuwepo? Au ndo nyani hao k**dule?

2. Wanasema gari lililokuwa na mwili wa marehemu pamoja na waandishi lilisimamishwa na kundi la watu na kuingia kinguvu. Huo mwili waliubebea kwenye Fuso au Hood from Iringa? Maana kama ni gari ndogo (hata coaster) sidhani kama ingetosha kubeba waandishi, jeneza, ndugu, kundi la vijana.
 
Hivi Kanumba alikuwa na cheo gani ktk siasa vile?

watu wengi walihudhuria wakiwepo wanasiasa ambao pia walitoa ubani, lilikuwa tukionmaalum. tukio la Mwangosi ni unique na mtu yeyeto aliyesikia angeweza kushiriki.
 
Tayari Msiba wa Mwangosi umekuwa biashara hivi Godwin Francis ni mwanafamilia mpaka azuie watu fulani kumzika au kaambiwa atapewa ukuu wa wilaya akifuata maagizo ya polisi mjinga sana huyo kijana kama anadhani anaweza akachukua nafasi ya familia watoto na mke kupanga watu wa kuwahani

Huyu Godwin Francis ni mwandishi wa habari wa media gani,Ch10,Uhuru/Mzalando,Habari Leo,Daily News au????
Kinachooneka hapa ni kwamba huyu jamaa anataka kutumiwa tu na CCM ili kupotosha maana halisi ya ushiriki wa CDM kwenye msiba huu!

Kwa jadi za kiafrika mtu yeyote na mahali popote anaweza kushiriki kwenye msiba/mazishi ya marehemu bila kujadili itikadi za chama wala dini. CCM waache kulaghai watu kwa kujaribu kukipaka matope CDM! Pambaf zao.
 
CCM Blog: DK. SLAA NA WENZAKE WADANDIA KINGUVU MAZISHI YA MWANGOSI, MBEYA

VIONGOZI wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa, wametuhumiwa kulazimisha kinguvu, kushiriki mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten, mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.

Marehemu Mwangosi aliyefariki katika vurugu, zilizobababishwa na CHADEMA eneo la Nyororo, alizikwa Jumanne ya wiki hii, katika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe huku kundi kubwa la wafuasi wa CHADEMA, likihudhuria mazishi hayo.

Inaelezwa licha ya kuambiwa msiba huo siyo wa kisiasa, hivyo hawatakiwi viongozi hao wala wanachama wa CHADEMA, lakini walilazimisha kushiriki kwa nguvu, na hata mwili wa marehemu ulipowasili Tukuyu mjini ukitokea mkoani Iringa, walilazimisha kuingia kinguvu kwenye gari hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, Francis Godwin, alisema kuwa tangu wakiwa mjini Iringa, aliwatangazia wazi CHADEMA kuwa msiba huo unawahusu waandishi wa habari na siyo wanasiasa.

“Tulianza kukwaruzana tangu hatujaondoka mjini Iringa, kwani wakati tunatangaza taratibu za kusafiri, nilitumiwa ujumbe na viongozi wa CHADEMA, kuwa nitangaze msafara huo utaongozwa na Dk.Slaa, lakini niliwakatalia kuwa huo siyo msiba wa mwanasiasa bali ni mwanahabari hivyo hilo halitawezekana” alisema Godwin.

Godwin alisema aliwaeleza wazi viongozi wa CHADEMA, kuwa kama wanataka kwenda kushiriki mazishi hayo basi ni vyema watafute taratibu nyingine za kufika wilayani Rungwe, lakini siyo kung’ang’ania waongozane na mwili wa marehemu, kitu kilichowakera viongozi hao.

Aliongeza kuwa walishangazwa walipofika Tukuyu mjini, kundi la vijana wafuasi wa CHADEMA walilifuata gari walilokuwemo waandishi wa habari kutoka mkoa wa Iringa ambamo ndipo mwili wa marehemu Mwangosi ulikuwemo na kuamua kuingia kinguvu.

Kwa mujibu wa Godwin, walipojaribu kuwakataza vijana hao wa CHADEMA, iwapo kuna mtu atawakatalia kuingia basi watambue wazi kuwa damu itamwagika hali iliyowafanya washindwe kuwazuia kwa kuogopa kuanzisha vurugu zisizo na msingi.

Aidha, katika kuonyesha kukerwa na hali hiyo iliyojitokeza, akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe, Godwin alisema hakuwahi kusikia marehemu Mwangosi akisema kuwa yeye ni mwanachama ama mfuasi wa chama chochote cha siasa.

Godwin alisema:”Ninachokifahamu mimi ni kuwa marehemu Mwangosi, alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, hivyo hatutegemei msiba huu kuanza kuingizwa itikadi za kisiasa”.

Aliongeza kwa kulitaka Jeshi la polisi kuwa hata kama marehemu Mwangosi, alifanya kosa lililopelekea akutwe na mauti hayo alipaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na siyo kufa aina ya kifo hicho cha kufa kwa bomu la machozi.

Katika kuonyesha kuwa kauli hizo ziliwachoma CHADEMA, Dk.Slaa aliposimama kuzungumza na wananchi, alisema anachofahamu yeye ni kuwa msiba hauna rangi, kabila wala dini.

Dk.Slaa aliongeza hivyo anapenda kutumia nafasi hiyo kukemea kauli za ubaguzi zilizotolewa, kwani CHADEMA wameenda kushiriki msiba huo kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na marehemu.

“Wakati tunaondoka mkoani Iringa kuja huku Rungwe-Mbeya, kuna kitu kilitokea ambacho kilitukwaza na sitapendi kukizungumza hapa…nimemjua marehemu Mwangosi alikuwa mtu wa haki na alikuwa akipinga vitendo vya kifisadi” alisema Dk.Slaa.

Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati wa mazishi, Dk.Slaa alimfuata Godwin na kumueleza kuwa amemsamehe kwa yote aliyoyafanya hali ambayo ilimlazimu naye (Godwin), kumjibu kuwa hajafanya kosa lolote linalostahili asamehewe.

Achani mambo ya ki pu uzi na ki umagamba magamba. Tangu lini tukabaguana nani wa kufika kwenye msiba???? Watanzania hatujafika hapo jamani. Mnataka kutupeleka wapi???? Eti mtu kadandia msiba. Are you insane????
 
Nachukia sana hii mambo ya kushadadia siasa kwa kila jambo na kuacha kushughulikia mambo ya msingi ya maendeleo. CCM wanatakiwa wawaeleze wananchi kodi zao zimezaa matunda gani na si kuja na kauli nyiiingiii za kisiasa katika kifo cha mwenzetu Mwangosi ambacho kimesababishwa na serikali yao, na sasa wanafikri WaTz watawaonea huruma kwa ku-capitalize kuwa M4C ndo chanzo. CCM, eleweni kuwa sisi siyo akina ZOMBA!
 
Hivi Dr. Slaa alipigwa ban asiwe anaenda kwenye misiba ya aina hii? Propaganda nyingine ni ujinga mtupu.
 
Mi nashindwa kuelewa mkuu. Halafu mbona Mwandosya naye alikuwepo! Au si mwanasiasa yule siku hizi? Au kwa vile ni wa CCM?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom