CCM chama bora Afrika

“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,amlofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Si kweli kuwa CCM ni chama bora bali ni ni ktk contest ya vyama vilivyoko Afrika ambavyo vimejaa migogolo kama vyama vya Lyatonga,ukabila kama Chadema na udini kama CUF.sasa the best choice among altenatives parties is CCM.Wanachama wa ccm hawatoki nje ya watanzania ndio mana ata mienendo yao inaonyesha haswa tabia za watanzania,

CCM imejaa uongo, ulaghai, wizi, rushwa, uhuni, kutokumuogopa mungu, ukandamizaji, na kila aina ya wizi.
 
Mmmmh. kwa akili za kawaida huwezi kuandika haya. wezi wa ccm na watoto wao wanakazimwaka huu. endeleeni kumbana lubuva la sivyo. sijui itakuaje hatma yenu.maana ukawawatanza na kurudisha nyumba na mali za serekali. ila lubuva mnyika kamkalia kooni. safari hiimtatafutana. maana hapo naona mmepanic mbaya. post za kilamamna.
Poleni sana.
 
Kiliwanyama watu elimu ili kujiimarisha,na kendelea kuwatawala hao watu kwa kukosa kwao elimu
 
Sawa bwana mbona mdomo hulipii.Hivi kweli CCM ingekuwa bora si tungekuwa tumepata maendeleo na tungekuwa na mipango mizuri kama Ethiopia,Botswana au Somaliland(Sio Somalia).Sawa bwana,si Lumumba inakulipa kwa kueneza uzushi huu!?Ila kumbuka siku zote,kwamba utakuja kujutia uovu huu.
Sifa Kubwa 10 Kudhihirisha kuwa CCM ni Chama Bora Barani Afrika

1. CCM ni Chama chenye mtandao mpana mpaka ngazi zote za chini nchi nzima. Kiongozi wa chini kabisa katika jamii yetu ni mjumbe wa shina wa CCM. Kabla ya kumwona kiongozi yeyote katika ngazi ya chini, wa kwanza kumwona ni kiongozi wa CCM. Hakika ni mtandao pekee mpana barani Afrika!

2. CCM ni Chama kilichohimili na kustahimili mikikimikiki na misukosuko ya mabadiliko ya kisiasa pasipo kuyumba wala kutetereka. Vyama vingine vikongwe vimesambaratika vibaya. Mathalani UNIP cha Zambia, MCP cha Malawi, KANU na NARC vya Kenya, NDC cha Ghana, Socialist Party (PS) cha Senegal na SLPP cha Sierra Leone, na vinginevyo. Hakika huu ni uimara na umadhubuti wa pekee barani Afrika!

3. CCM ni Chama kilichoonesha uwezo na ukomavu mkubwa katika kusuluhisha migogoro na tofauti ndani ya Chama kwa njia za amani, maelewano, maridhiano na kusameheana kupitia vikao halali vya Chama. Hakika hii ni demokrasia ya pekee na ya kuigwa barani Afrika!

4. CCM ni Chama kilichoweza kubadilishana viongozi kwa mchakato ulio wazi, wenye ustaarabu mkubwa na wa demokrasia ya kweli ndani ya Chama na Serikali, pasipo uhasama wala vurugu zozote tokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere alipong’atuka 1985, na tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanza upya 1992. Hakika hii ni historia pekee na ya kuigwa barani Afrika.

5. CCM ni Chama kilichomudu kuimarisha na kuviwezesha vyama vingine kukomboa nchi zao kusini mwa jangwa la Sahara. Mathalani FRELIMO cha Msumbiji na MPLA cha Angola (1975), ZANU-PF cha Zimbabwe (1980), NRM cha Uganda (1986), SWAPO cha Namibia (1991) na ANC cha Afrika Kusini (1994), na vinginevyo. Hakika huu ni mchango mkubwa na wa kipekee katika historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

6. CCM ni Chama chenye kutetea, kulinda na kuimarisha amani, utengamano na umoja wa kitaifa nchini, na kuleta maelewano baina ya vyama, sambamba na viongozi wake kujihusisha bega kwa bega katika kuyapatanisha makundi yanayohasimiana katika nchi jirani na kwingineko barani Afrika. Hakika huu pia ni mchango wa pekee barani Afrika!

7. CCM ni Chama chenye uzoefu mkubwa wa kuwekeza na kuendesha miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa mali zao. Hii ni pamoja na kulinda na kuhifadhi magari ya thamani kubwa pasipo kujali itikadi za wamiliki. Hakika huu ni uzalendo na utaifa wa pekee na wa kuigwa barani Afrika!

8. CCM ni Chama kilichoweza kutoa viongozi mahiri na waliotukuka katika ngazi ya kitaifa na Kimataifa kwenye nyanja mbalimbali. Mathalani kwa uchache, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Salim Ahmed Salim, Balozi Ali Mchumo, Rais wa Bunge la Afrika Getrude Mongella na wengineo. Hakika hii ni sifa ya pekee na ya kujivunia barani Afrika!

9. CCM ni Chama kinachohamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kila siku pasipo kusubiri nyakati za uchaguzi. Tunawaona viongozi wa CCM wakituhimiza kila siku kufanya kazi kwa bidii. Hakika jambo hili ni nadra sana kuliona kwingineko barani Afrika!

10. CCM ni Chama kilichoonesha dhamira ya kweli kuhusisha na kuutambua mchango wa wanawake katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, ikiwa pamoja na uwepo wa wanawake wa kutosha katika Baraza la Mawaziri na kuwapa vyeo vya juu jeshini. Hakika huu ni mfano pekee na wa kuigwa barani Afrika katika usawa wa kijinsia.

Na: Gwandumi G.A. Mwakatobe (0714 - 511622)
(Mfuatiliaji na Mchambuzi wa Masuala ya Kitaifa na Kimataifa)
 
Nakubaliana na mtoa post kuwa CCM ni chama bora dhaifu na legelege kilicho hatarini kutoweka na kufutika kabisa!!..
 
Back
Top Bottom