CCM chama bora Afrika

Ahsanteni kwa dataz wakuu, maana never before kuon something like this, lakini mkuu Mpoki uko wapi hebu tuwekee vitu hapa huyu wakwenu huyu ni Malafyale huyu au?
 
Gembe,

SAmahani ndugu zangu. CCM haijaoza ni baadhi ya wanachama wa CCM ndio wameoza. Chama bado kipo imara. Ndo maana nasisitiza kuwa kweli aliyoandika jamaa sio sahihi kwasababu kwa sasa chama kimeharibika!

Ila bado hatujakata tamaa.
 
....kwa kweli na hasara na njaa zote wanazotutia bado kuna watu wanasifia hawa mafisadi,kazi ipo kweli kweli!
KOBA mkuu wangu!
Kuna kitu kinaitwa LIMBWATA unakijua hicho? basi mkuu hicho mtu akishalishwa hata umwambieje hatakuelewa. Ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.Watu wa namna hiyo wamepewa limbwata na CCM.
 
Huyu mhurumieni, anatafuta namna ya kufika walipofika wenzake akina Tambwe na Akwilombe ili naye aanze kutembea na Makamba kwenye misafara.
um
Maumivu yako nayajua Mr Opportunity,kwanza unakumbuka zile pesa zako ambazo ulitugawia wakati wa kampeni ya uvccm na bado tukakupiga chini,usingekata tamaa japo najua ulizoea siasa za shule na pia wakati ulikuwa ndio kwanza unatoka shule ni bora ungemtumia Mzee Mkumbwa ile pesa kuliko kuwapa wale bustard.Lazima uiogope historia yako kwa kuwa ndio inayotupa dira wewe ni mtu wa namna gani au umetubu?
 
Kama sasa anaongea haya kwa kifua mbele means amebadilika na katoka CCM kwa kuwa aligundua mapema kwamba si mahala pake .So historia pia inaweza kuandikwa na kesha andika sasa kwamba nyie mafisadi kuanzia Baba zenu na nyie endeleeni kubakia CCM yeye kesha ondoka .
 
Huyu mhurumieni, anatafuta namna ya kufika walipofika wenzake akina Tambwe na Akwilombe ili naye aanze kutembea na Makamba kwenye misafara.

Unakumbuka hii hoja yako?

Jee? Bado maoni yako ni hayo hayo toka ulivyopigwa chini chadema au yamebadilika?
 
:d:d:d
 
Attachments

  • 1443608524877.jpg
    1443608524877.jpg
    16 KB · Views: 160
8. CCM ni Chama kilichoweza kutoa viongozi mahiri na waliotukuka katika ngazi ya kitaifa na Kimataifa kwenye nyanja mbalimbali. Mathalani kwa uchache, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Salim Ahmed Salim, Balozi Ali Mchumo, Rais wa Bunge la Afrika Getrude Mongella na wengineo. Hakika hii ni sifa ya pekee na ya kujivunia barani Afrika!

Hapo kwenye rangi ya bluu ni kweli kabisa, maana kiongozi mahiri anawaambia wazungu kuwa hajui kwanini nchi yake ni maskini.

Viongozi mahiri kabisa, wanaotuhumiwa kuua tembo na kusafirisha wanyama(twiga) nje ya nchi.

Viongozi mahiri kabisa wanakwapua pesa za umma kama sakata la escrow lilivyotoa majibu chini ya kamati PAC.

Viongozi mahiri ambao licha ya kuwa nchi ina rasilimali za kutosha lakini kila siku wako ulaya na marekani kuomba misaada/ufadhiri.

Viongozi mahiri kabisa wenye kuongoza nchi yenye ardhi kubwa yenye rutuba na maji ya kutosha kwenye mito na mabwawa lakini wananchi wanakufa na njaa na chakula kinauzwa kwa bei ghali sana ilhali kinalimwa nchini mwao.
 
Sifa Kubwa 10 Kudhihirisha kuwa CCM ni Chama Bora Barani Afrika

1. CCM ni Chama chenye mtandao mpana mpaka ngazi zote za chini nchi nzima. Kiongozi wa chini kabisa katika jamii yetu ni mjumbe wa shina wa CCM. Kabla ya kumwona kiongozi yeyote katika ngazi ya chini, wa kwanza kumwona ni kiongozi wa CCM. Hakika ni mtandao pekee mpana barani Afrika!

2. CCM ni Chama kilichohimili na kustahimili mikikimikiki na misukosuko ya mabadiliko ya kisiasa pasipo kuyumba wala kutetereka. Vyama vingine vikongwe vimesambaratika vibaya. Mathalani UNIP cha Zambia, MCP cha Malawi, KANU na NARC vya Kenya, NDC cha Ghana, Socialist Party (PS) cha Senegal na SLPP cha Sierra Leone, na vinginevyo. Hakika huu ni uimara na umadhubuti wa pekee barani Afrika!

3. CCM ni Chama kilichoonesha uwezo na ukomavu mkubwa katika kusuluhisha migogoro na tofauti ndani ya Chama kwa njia za amani, maelewano, maridhiano na kusameheana kupitia vikao halali vya Chama. Hakika hii ni demokrasia ya pekee na ya kuigwa barani Afrika!

4. CCM ni Chama kilichoweza kubadilishana viongozi kwa mchakato ulio wazi, wenye ustaarabu mkubwa na wa demokrasia ya kweli ndani ya Chama na Serikali, pasipo uhasama wala vurugu zozote tokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere alipong’atuka 1985, na tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanza upya 1992. Hakika hii ni historia pekee na ya kuigwa barani Afrika.

5. CCM ni Chama kilichomudu kuimarisha na kuviwezesha vyama vingine kukomboa nchi zao kusini mwa jangwa la Sahara. Mathalani FRELIMO cha Msumbiji na MPLA cha Angola (1975), ZANU-PF cha Zimbabwe (1980), NRM cha Uganda (1986), SWAPO cha Namibia (1991) na ANC cha Afrika Kusini (1994), na vinginevyo. Hakika huu ni mchango mkubwa na wa kipekee katika historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

6. CCM ni Chama chenye kutetea, kulinda na kuimarisha amani, utengamano na umoja wa kitaifa nchini, na kuleta maelewano baina ya vyama, sambamba na viongozi wake kujihusisha bega kwa bega katika kuyapatanisha makundi yanayohasimiana katika nchi jirani na kwingineko barani Afrika. Hakika huu pia ni mchango wa pekee barani Afrika!

7. CCM ni Chama chenye uzoefu mkubwa wa kuwekeza na kuendesha miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa mali zao. Hii ni pamoja na kulinda na kuhifadhi magari ya thamani kubwa pasipo kujali itikadi za wamiliki. Hakika huu ni uzalendo na utaifa wa pekee na wa kuigwa barani Afrika!

8. CCM ni Chama kilichoweza kutoa viongozi mahiri na waliotukuka katika ngazi ya kitaifa na Kimataifa kwenye nyanja mbalimbali. Mathalani kwa uchache, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Salim Ahmed Salim, Balozi Ali Mchumo, Rais wa Bunge la Afrika Getrude Mongella na wengineo. Hakika hii ni sifa ya pekee na ya kujivunia barani Afrika!

9. CCM ni Chama kinachohamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kila siku pasipo kusubiri nyakati za uchaguzi. Tunawaona viongozi wa CCM wakituhimiza kila siku kufanya kazi kwa bidii. Hakika jambo hili ni nadra sana kuliona kwingineko barani Afrika!

10. CCM ni Chama kilichoonesha dhamira ya kweli kuhusisha na kuutambua mchango wa wanawake katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, ikiwa pamoja na uwepo wa wanawake wa kutosha katika Baraza la Mawaziri na kuwapa vyeo vya juu jeshini. Hakika huu ni mfano pekee na wa kuigwa barani Afrika katika usawa wa kijinsia.

Na: Gwandumi G.A. Mwakatobe (0714 - 511622)
(Mfuatiliaji na Mchambuzi wa Masuala ya Kitaifa na Kimataifa)

Utafiti wa Aidani Ayakuze huu! Hahahaaa!
 
Ubora kwa wizi, rushwa na ufisadi pamoja na matumizi mabaya ya ofisi na rasilimali za Taifa ccm hawajambo.
 
ccm ni ukoo wa panya; 'baba mwizi, mama mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, babu mwizi, bibi mwizi, mkwe mwizi, shangazi mwizi, mjomba mwizi' BY Mh. Nassari
 
Alijisemea msemaji wa lowas alisema ccm ikishinda yeye hana shida kwasababu chadema hawawezi kuongoza serekali wanahitaji kusaidiwa. hivi nikumbe cdm hawana uwezo wa kuongoza serekali.....
 
umahiri wa kiongozi unapaswa kupimwa kwa kigezo cha uwezo wake wa kutatua kero za watu wake na kuhakikisha huduma zote za msingi zinapatikana na zinatolewa kwa kiwango bora na wakati stahili. sio hizo sifa za kijinga kiongozi anasifiwa kwa kuwahudumia jirani zake wakati watoto wake wanateseka kwa njaa maradhi ujinga umaskini na ufukara unaoongezeka kila uchao
 
Yaani nina hasira na ccm, natamani October ifike kesho nipige kura maana nahisi kama naweza pata ajali nikafa kabla ya kuchangia ukombozi wa nchi hii
 
Attachments

  • 1443614466560.jpg
    1443614466560.jpg
    17.4 KB · Views: 98
Sifa Kubwa 10 Kudhihirisha kuwa CCM ni Chama Bora Barani Afrika

1. CCM ni Chama chenye mtandao mpana mpaka ngazi zote za chini nchi nzima. Kiongozi wa chini kabisa katika jamii yetu ni mjumbe wa shina wa CCM. Kabla ya kumwona kiongozi yeyote katika ngazi ya chini, wa kwanza kumwona ni kiongozi wa CCM. Hakika ni mtandao pekee mpana barani Afrika!
2. CCM ni Chama kilichohimili na kustahimili mikikimikiki na misukosuko ya mabadiliko ya kisiasa pasipo kuyumba wala kutetereka. Vyama vingine vikongwe vimesambaratika vibaya. Mathalani UNIP cha Zambia, MCP cha Malawi, KANU na NARC vya Kenya, NDC cha Ghana, Socialist Party (PS) cha Senegal na SLPP cha Sierra Leone, na vinginevyo. Hakika huu ni uimara na umadhubuti wa pekee barani Afrika!
3. CCM ni Chama kilichoonesha uwezo na ukomavu mkubwa katika kusuluhisha migogoro na tofauti ndani ya Chama kwa njia za amani, maelewano, maridhiano na kusameheana kupitia vikao halali vya Chama. Hakika hii ni demokrasia ya pekee na ya kuigwa barani Afrika!
4. CCM ni Chama kilichoweza kubadilishana viongozi kwa mchakato ulio wazi, wenye ustaarabu mkubwa na wa demokrasia ya kweli ndani ya Chama na Serikali, pasipo uhasama wala vurugu zozote tokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere alipong’atuka 1985, na tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanza upya 1992. Hakika hii ni historia pekee na ya kuigwa barani Afrika.
5. CCM ni Chama kilichomudu kuimarisha na kuviwezesha vyama vingine kukomboa nchi zao kusini mwa jangwa la Sahara. Mathalani FRELIMO cha Msumbiji na MPLA cha Angola (1975), ZANU-PF cha Zimbabwe (1980), NRM cha Uganda (1986), SWAPO cha Namibia (1991) na ANC cha Afrika Kusini (1994), na vinginevyo. Hakika huu ni mchango mkubwa na wa kipekee katika historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
6. CCM ni Chama chenye kutetea, kulinda na kuimarisha amani, utengamano na umoja wa kitaifa nchini, na kuleta maelewano baina ya vyama, sambamba na viongozi wake kujihusisha bega kwa bega katika kuyapatanisha makundi yanayohasimiana katika nchi jirani na kwingineko barani Afrika. Hakika huu pia ni mchango wa pekee barani Afrika!
7. CCM ni Chama chenye uzoefu mkubwa wa kuwekeza na kuendesha miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa mali zao. Hii ni pamoja na kulinda na kuhifadhi magari ya thamani kubwa pasipo kujali itikadi za wamiliki. Hakika huu ni uzalendo na utaifa wa pekee na wa kuigwa barani Afrika!
8. CCM ni Chama kilichoweza kutoa viongozi mahiri na waliotukuka katika ngazi ya kitaifa na Kimataifa kwenye nyanja mbalimbali. Mathalani kwa uchache, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Salim Ahmed Salim, Balozi Ali Mchumo, Rais wa Bunge la Afrika Getrude Mongella na wengineo. Hakika hii ni sifa ya pekee na ya kujivunia barani Afrika!
9. CCM ni Chama kinachohamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kila siku pasipo kusubiri nyakati za uchaguzi. Tunawaona viongozi wa CCM wakituhimiza kila siku kufanya kazi kwa bidii. Hakika jambo hili ni nadra sana kuliona kwingineko barani Afrika!
10. CCM ni Chama kilichoonesha dhamira ya kweli kuhusisha na kuutambua mchango wa wanawake katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, ikiwa pamoja na uwepo wa wanawake wa kutosha katika Baraza la Mawaziri na kuwapa vyeo vya juu jeshini. Hakika huu ni mfano pekee na wa kuigwa barani Afrika katika usawa wa kijinsia.
 
Sifa Kubwa 10 Kudhihirisha kuwa CCM ni Chama Bora Barani Afrika

1. CCM ni Chama chenye mtandao mpana mpaka ngazi zote za chini nchi nzima. Kiongozi wa chini kabisa katika jamii yetu ni mjumbe wa shina wa CCM. Kabla ya kumwona kiongozi yeyote katika ngazi ya chini, wa kwanza kumwona ni kiongozi wa CCM. Hakika ni mtandao pekee mpana barani Afrika!
2. CCM ni Chama kilichohimili na kustahimili mikikimikiki na misukosuko ya mabadiliko ya kisiasa pasipo kuyumba wala kutetereka. Vyama vingine vikongwe vimesambaratika vibaya. Mathalani UNIP cha Zambia, MCP cha Malawi, KANU na NARC vya Kenya, NDC cha Ghana, Socialist Party (PS) cha Senegal na SLPP cha Sierra Leone, na vinginevyo. Hakika huu ni uimara na umadhubuti wa pekee barani Afrika!
3. CCM ni Chama kilichoonesha uwezo na ukomavu mkubwa katika kusuluhisha migogoro na tofauti ndani ya Chama kwa njia za amani, maelewano, maridhiano na kusameheana kupitia vikao halali vya Chama. Hakika hii ni demokrasia ya pekee na ya kuigwa barani Afrika!
4. CCM ni Chama kilichoweza kubadilishana viongozi kwa mchakato ulio wazi, wenye ustaarabu mkubwa na wa demokrasia ya kweli ndani ya Chama na Serikali, pasipo uhasama wala vurugu zozote tokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere alipong’atuka 1985, na tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanza upya 1992. Hakika hii ni historia pekee na ya kuigwa barani Afrika.
5. CCM ni Chama kilichomudu kuimarisha na kuviwezesha vyama vingine kukomboa nchi zao kusini mwa jangwa la Sahara. Mathalani FRELIMO cha Msumbiji na MPLA cha Angola (1975), ZANU-PF cha Zimbabwe (1980), NRM cha Uganda (1986), SWAPO cha Namibia (1991) na ANC cha Afrika Kusini (1994), na vinginevyo. Hakika huu ni mchango mkubwa na wa kipekee katika historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
6. CCM ni Chama chenye kutetea, kulinda na kuimarisha amani, utengamano na umoja wa kitaifa nchini, na kuleta maelewano baina ya vyama, sambamba na viongozi wake kujihusisha bega kwa bega katika kuyapatanisha makundi yanayohasimiana katika nchi jirani na kwingineko barani Afrika. Hakika huu pia ni mchango wa pekee barani Afrika!
7. CCM ni Chama chenye uzoefu mkubwa wa kuwekeza na kuendesha miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa mali zao. Hii ni pamoja na kulinda na kuhifadhi magari ya thamani kubwa pasipo kujali itikadi za wamiliki. Hakika huu ni uzalendo na utaifa wa pekee na wa kuigwa barani Afrika!
8. CCM ni Chama kilichoweza kutoa viongozi mahiri na waliotukuka katika ngazi ya kitaifa na Kimataifa kwenye nyanja mbalimbali. Mathalani kwa uchache, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Salim Ahmed Salim, Balozi Ali Mchumo, Rais wa Bunge la Afrika Getrude Mongella na wengineo. Hakika hii ni sifa ya pekee na ya kujivunia barani Afrika!
9. CCM ni Chama kinachohamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kila siku pasipo kusubiri nyakati za uchaguzi. Tunawaona viongozi wa CCM wakituhimiza kila siku kufanya kazi kwa bidii. Hakika jambo hili ni nadra sana kuliona kwingineko barani Afrika!
10. CCM ni Chama kilichoonesha dhamira ya kweli kuhusisha na kuutambua mchango wa wanawake katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, ikiwa pamoja na uwepo wa wanawake wa kutosha katika Baraza la Mawaziri na kuwapa vyeo vya juu jeshini. Hakika huu ni mfano pekee na wa kuigwa barani Afrika katika usawa wa kijinsia.

Ushindi wa CCM ni asubuh sana
 
Attachments

  • 1443617185972.jpg
    1443617185972.jpg
    63.3 KB · Views: 131
"Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira". Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha "wateule" na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, "kulikoni?". Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya "malofa" wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: "Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?"Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza "nyomi" katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni "vijisenti", au "fedha ya mboga", wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa "Wapige mbizi" na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa "Ni heri wale nyasi"…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni "wapumbavu,amlofa na mbumbumbu". Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo."ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain"; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Back
Top Bottom