CCJ ni mradi wa CCM

Conclusion yako ingekuwa nzuri kama ungeweka data zinazo endana na analysis yake, kwani conclusion huwa inatokana na kuwa na data na kuzichambua na kufikia hitimisho - matokeo kwa kifupi, na iwe na logic. Je umetumia njia zipi za kitafiti kufikia conclusion yako? Fikra pia zinakubalika kufikia conclusion lakini lazima kuwe na back-up au evidence ya kutosha.

Mbona mimi naona CCJ sio cha CCM kwa sababu wakisajiliwa kitakuwa chama kingine cha siasa. Na umekwishasema kuwa CCM kuna makundi matatu, moja linataka kujitoa, sasa uoni kama kutabaki na makundi 2 yataendelea kuunda CCM na moja chama kingine na mwisho wa siku kuwa na vyama viwili tofauti. Mwanzo walisema vivi hivi kuwa kimeundwa na usalama wa taifa. Kama ni cha CCM mbona usajili wake unakuwa mgumu?

Labda unge-conclude kuwa CCJ asili yake ni CCM kwani kundi linalounda CCJ linatoka CCM baada ya kuwa na makundi matatu ambayo yanapingana na makundi mawaili ambayo yatabaki huko CCM. Pia labda uongezee kuwa wanachama waliopatikana kwa ajili ya usajili wa kudumu, wengi wao walikuwa CCM. Swali: je haya yanayobaki CCM yamekubaliana kuwa pamoja? Au baadae moja tena litatoka?
 
Ndio maana mimi kuwa nawashauri watu kutokurupuka...Maana kuna jamaa zangu mara sasa mkombozi kaja mara tumepata chama hasa.. mara hiki ndo kitakuwa cha upinzani wa kweli nakadhalika..Hivi watu hawaoni CHADEMA??
 
Ndugu, mara nyingi hoja haijengwi kwa kuanza na hitimisho. Kwa kawaida tunaanza na utangulizi (intro/background) ambayo hueleza hali halisi, halafu hufuatiwa na smukumo , kwa nini unaamini yale unayotaka kuyaandika (rationale) n.k. Sasa unaporukia tu conclusion, inakuwa vigumu kuona kuwa huna lako jambo.
Nono, asante kumpa Romos abc za kujenga hoja, kwa vile ni mgeni humu, kwanza Romos karibu JS. pili lengo la mada zote humu, ni ama kuhabarisha, kuelimisha, au kuburudisha. Tofauti na vyombo vingine vya habari, humu pia tunaibua mijadala. Ili hoja yako hii iweze kujadilika kwa afya na mashika, wewe usingetoa conclusion 'CCJ ni mradi wa CCM', ungeitoa kama swali au hojaji kama Je CCJ ni mradi wa CCM?. ungetoa hoja zako zilizopelekea kufiki hivyo na ungejibiwa kwa hoja kwa nini udhaniavyo ndivyo, sivyo, na kuna udhaniavyo sivyo, kumbe ndivyo.
Karibu JS ya JF.
 
Ninavyomfahamu Mpendazoe hawezi kutumiwa na CCM. Hayo ni mawazo potofu na si ajabu yanajengwa na CCM wenyewe ili kuizorotesha CCJ.
 
Ramos,
Kwa hiyo kwa huo ushahidi wa ki-mazingingira, je tunaweza hitimisha pia kuwa Mwanakijiji ni mpelekwa katika huo Mradi?
 
upande mmoja wanasema CCJ imekuja ili kudhoofisha upinzani; wakati huo huo wengine wanaona kuwa CCJ inakuja na inatishia CCM, na wengine wanaamini (katika fikra zao) kuwa CCM imejiundia chama cha kukidhoofisha mbele ya wananchi! Halafu wanaenda na kutoa matangazo hadi kwenye website zao kukipinga na hata kukitishia kukinyima usajili.. wakati mwingine mtiririko wetu wa kufikiri una matatizo sana..
 
"mtiririko wetu wa kufikiri una matatizo sana.. " kweli nakubaliana na wewe tumeshindwaje kweli kuona chama ambacho kimeanzishwa na watu wawili ambacho kigogo kutoka chama chenye sera nzuri ya ujamaa kinachotegemea vigogo watakaomeguka kutoka katika chama ambacho kina rekodi nzuri kabisa ya utendaji na kuja kujiunga katika hiki chama ambacho sisi hatukioni.

Hii ccj itatusaidi kuwajua watu vizuri
 
Ndio maana mimi kuwa nawashauri watu kutokurupuka...Maana kuna jamaa zangu mara sasa mkombozi kaja mara tumepata chama hasa.. mara hiki ndo kitakuwa cha upinzani wa kweli nakadhalika..Hivi watu hawaoni CHADEMA??

....ni kweli kuna watu wengi sana wana mawazo hayo, lakini jiulize ni wapi vyama vya upinzani vilivyopo vilipojikwaa?na kwanini havijirekebishi ili kubeba matarajio ya watu hawa?...labda ndio sikio la kufa.
 
vimekuwa na karibu miaka 15 kujirekebisha...
 
....ni kweli kuna watu wengi sana wana mawazo hayo, lakini jiulize ni wapi vyama vya upinzani vilivyopo vilipojikwaa?na kwanini havijirekebishi ili kubeba matarajio ya watu hawa?...labda ndio sikio la kufa.

Unauhakika kuwa havijirekebishi?umefuatlia trend yao au unasema tu?hivi unafikiri changes huwa zinatokea ndani ya siku moja?hata Roma haikujengwa kwa siku moja,reformation ndani ya taasisi yeyote ile huwa hafanyikikwa haraka kama unavyotaka,hata ndani ya familia huchukua muda...Mabadiliko ni mchakato Mkuu,sio rahisi kihivyo,kumbuka hizi ni taassisi za kisiasa sio MONGOs (My own NGOs)ambapo unaweza ukafanya mabadiliko ndani ya masaa 24 na mambo ya kawa sawa tu...Siasa ni ngumu inahitaji maandalizi na uchambuzi wa kina..
 
WanaJF mna maoni yeyote kuhusu hili?
Najaribu kujenga conclusion kuwa CCJ ni mradi wa CCM.

Najua kuwa CCM inafanya kila jitihada kuhakikisha haiondoki madarakani. Mojawapo wa mbinu wanazotumia ni 'wagawe uwatawale'. CCM wanajua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaokipinga chama chao hali inayohatarisha future yao katika siasa. yapo maeneo yanayoibukia kwa kasi katika kustawi kwa siasa za upinzani, moja wapo ikiwa kanda ya ziwa victoria. Kwa kuona na kutambua hatari hii inaonekana kundi moja la CCM (huwa naamini CCM ina makundi ma3) limeamua kuanzisha chama kitakachogawa nguvu ya upinzani nchini (hasa ya CHADEMA) kuhakikisha kuwa hakutakuwa na chama kitakachojenga nguvu ya kutisha.

Kama ni mfuatiliaji wa mambo ya CCJ utagundua kuwa chama hiki kimejijengea umaarufu mkubwa maeneo ya kada ya ziwa. Na pia utagundua kuwa huku ndiko CHADEMA kwa miaka ya karibuni imeanza kujizolea umaarufu na ukubaliwaji mkubwa.

Naamini CCJ kinaanzishwa katika mazingira ya ku-confuse akili za watanzania wapenda mabadiliko ambao wengi walishaanza kukifikiria CHADEMA kama chama muafaka ambacho kikiendelea kujipanga vizuri kitakuwa na uwezo wa kuchukua madaraka.

Nisiandike sana lakini pamoja na ushahidi mwangine wa kimazingira kama muda kilipoanzishwa, watu waliokianzisha na maeneo kinapojizatiti inatoa alarm kabisa kuwa CCJ ni chama mradi cha CCM...

Kwa hiyo unataka kusema kuwa Mwanakijiji ambaye ameshaweka wazi kuwa ni mwanachama wa CCJ ni kada wa CCM pia?
 
CCJ ni mtambo wa kuvuruga mawazo yetu watanzania wa CCM wanafanya janja za nyakati za kikomunisti za kutaka kuhodhi madaraka kwa namana yeyote ile,nitaona kama kuna watanzania wengi watakwenda CCJ hata wakipata usajili wa kudumu,
 
Unauhakika kuwa havijirekebishi?umefuatlia trend yao au unasema tu?hivi unafikiri changes huwa zinatokea ndani ya siku moja?hata Roma haikujengwa kwa siku moja,reformation ndani ya taasisi yeyote ile huwa hafanyikikwa haraka kama unavyotaka,hata ndani ya familia huchukua muda...Mabadiliko ni mchakato Mkuu,sio rahisi kihivyo,kumbuka hizi ni taassisi za kisiasa sio MONGOs (My own NGOs)ambapo unaweza ukafanya mabadiliko ndani ya masaa 24 na mambo ya kawa sawa tu...Siasa ni ngumu inahitaji maandalizi na uchambuzi wa kina..

.....Kama muda sio limit, yes kila kitu kinawezekana, sio kwa CHADEMA tu bali pia kwa CCM, lakini je tuendelee kusubiri kwa sababu kuna possibilty ya marekebisho kufanyika in the future,...la hasha.

...Wakati ni huu, yawezayo kutendwa na yatendwe haraka kabla treni mpya haijaanza safari, historia ni mwalimu mzuri sana, TADEA/DP/NCCR/TLP wanalijua hili.
 
kama wangetaka kuungana wangeungana miaka hiyo 15.. kama wangetaka sera mpya wangeweza kuzisahihisha in the past 15 years..
Mabadiliko katika siasa yanahitaji kujitolea na uvumilivu wa hali ya juu kwa sababu una dili na mawazo mbali mbali ya watu, mtaji wa siasa ni watu si kama NGO's ambazo mtaji wake ni pesa unazoweza kopa benki. Mtaji watu hauna grantee kuwa utakopa benki na baada ya miaka 15 utarudisha na faida juu kama mnavyotaka kulazimisha.

Kwenye siasa kama hautakuwa na uvumilivu utaishia kuhama hama vyama au utatafuta short cuts na kufanya mambo ya ajabu ambayo mwisho wake ni kuangamiza jamii nzima au kuingia msituni kama Mseven wa Uganda alivyofanya, so is up to you guys kwenda na flow au kutafuta course nyingine apart from political parties.
 
Back
Top Bottom